John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Nadhani inakubidi kwanza utafute maana au tafsiri ya neno UDINI, ukisha pata rudi tutajadili maanake napoteza muda wa kujadili mengine muhimu...
 
Mmmh na wewe mmbeya!....umekimbia maswali yangu hapa badala yake unashadidia bifu tu lol!
Babu nimekupa ushindi...mbona tunaharibiana starehe?..nishabeba sana maboksi ngoja na mimi nicheki muvi babuu dah!!
 

.
Chanzo cha habari yako p/se.
.
 
Kila mwanasiasa ni opportunist tu.Lengo kuu ni kupata cheo,whether kuteuliwa au kuchaguliwa
 
mwenye data amwage cv ya heche walau tumjue badala ya hii taarab inayoendelea hapa
 
Dikteta Saanane kaondolewa kabla ya kuingia kwenye kura.tumekaa tukafurahi,AENDE AKAGOMBEE UENYEKITI WA VIJANA WA ODM KENYA.AKAMSAIDIE KIPENZI CHAKE RAILA ODINGA.HECHE KUWA MAKINI NA HUYU ATAKUPINDUA.Hakikisha mnamdhibiti kweli kweli
 
Hongera Heche, ila ujue umepewa jukumu kubwa sana, kazi siyo kuchaguliwa kazi ni jinsi ambavyo itawaongoza na kufikia malengo kwadri ya matarajio yao
 
MUNGU aliyeko mahali pote.CHADEMA ni chama chenye mkono wa MUNGU.Shetani hana nafasi.

Wewe mbunge mzima acha kumsingizia "Mungu" kwenye mambo yenu ya kisiasa!.
Mungu yupi anayeongoza watu kupora wake wa wenzao?
Mungu yupi anayependelea unafiki?

Halafu wewe Regia ni Kama yule mama wa UWT kule CCM!
Mawazo yenu, IQ zenu mipasho vyote viko sawa kabisa!

Na nadhani mmeingia kwenye siasa kwa style zinazofanana!
Acha kujipendekeza Mheshimiwa!
 
Enh Thread imerudi? Kuna vitu hapa naona vimetolewa. Admin pale palikuwa hamna matusi bali majibizano ya kawaida kati mgombea wa Bavicha na Mbunge Regia. Kwanini wameondoa zile posts? Nizimwage hapa au ndio ban? Mie nilikopi nilijua Mbunge kachemka vibaya sn na mgombea ametuambia nn kiliendelea. Tafadhali admins tutajieni sababu vinginevyo mie nina paste hapa kilichozungumzwa ili kuweka kumbukumbu sawa. Hii ni hansard bwana, mtu ukitapika ndo watu wameshadaka hivyo.
 
Dikteta Saanane kaondolewa kabla ya kuingia kwenye kura.tumekaa tukafurahi,AENDE AKAGOMBEE UENYEKITI WA VIJANA WA ODM KENYA.AKAMSAIDIE KIPENZI CHAKE RAILA ODINGA.HECHE KUWA MAKINI NA HUYU ATAKUPINDUA.Hakikisha mnamdhibiti kweli kweli
mwenzako Regia alianza hivi hivi jana na hatimaye MODS wakamuokoa. Na wewe endelea tu na Saanane. Au ni kupm utumbo wao? I wish ni mjue yule mgombea aliyeibuka wa pili, maana alilalama saana rafu zimechezwa kwny uchaguzi. Kwamba zilipigwa simu na Mbowe akawaambiwa wahakikishe wanachinja majina. Regia akakurupuka kujibu hoja. Hilo ni dokezo kwa yaliyotokea kwahiyo nawe bora utulie tu.
 
Mods, kwanini mmeondoa ile thread ya mchujo ndani ya Chadema?
 
Regia,

Kwa heshima ya nafasi yako na wanawake wenzio tafadhali badilisha hiyo picha yako (avatar) kama ulivyoshauriwa kutumia paragraph wakati unagombea Ubunge!
 

..ww Mungu wako ni yupi? mfalme daud alipochukua mke wa askari wake Mungu alimwacha? kasome biblia vzr usiweke reference za Mungu kwa ubinafsi wako..unaona kijiti kwenye jicho la mwenzio wakati wewe una boriti.
Hongera Mh Mtema endelea mbele!
 
Watu wengi sasa wameanza kuulizia wakihitaji kumjua Kamanda Heche. Haya ni maelezo yaliyopatikana siku za nyuma kidogo katika mazungumzo naye. Wakuu mpiganaji huyu anastahili kupewa ushirikiano ili aiongoze BAVICHA kwa maslahi ya nchi na chama chake pia. MPAKA SASA record ya Heche katika uaminifu wake kwa maslahi ya Watanzania wanyonge, ambao chama chake kimejipambanua kuwasemea na kuwapigania, si ya kutiliwa wasiwasi. Kwa maneno na vitendo. Mwingine anaweza kuongeza. Nawasilisha wakuu.

Watu wengi wameanza kuuliza Heche ni mtu gani. Walau haya yamepatikana kutokana na mazungumzo naye siku za nyuma kidogo. Lakini upambanaji wa Heche na uwezo wake katika kusukuma hoja za wananchi (Watanzania) wanyonge, hoja za chama chake na maslahi ya nchi kwa ujumla, MPAKA SASA si wa kutiliwa shaka wakuu. Apewe ushirikiano katika kushirikiana na viongozi wenzake CDM, kwa maendeleo ya nchi yetu. KAZI SI KUCHAGULIWA, KAZI NI KUWAJIBIKA KUTIMIZA MATARAJIO YA WATU KWA WAKATI HUO.


JOHN HECHE SUGUTA

- Kuzaliwa – 1981 – katika kijiji cha Sirari, Tarime
- Shule 1989 – Nyamaharaga Primary
- Sekondari – 1997- Bulima Secondary
- Musoma Allience High School- 2001
- Stashahada ya Ualimu - 2004- 2006 Chuo cha Ualimu Bunda
- Shahada ya Sanaa na Elimu – 2006-2009 Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Nyegezi
Mwanza.

HARAKATI ZA KISIASA:
- Kujiunga na CHADEMA mwaka 2000
- Mmoja wa Waasisi na waanzilishi wa Tawi la CHADEMA Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Nyegezi Mwanza.
- Katibu wa Tawi la CHADEMA SAUT 2008

- Mgombea Udiwani katika Kata ya Tarime Mjini CHADEMA Uchaguzi Mdogo 2008 kuziba nafasi ya Marehemu Mh. Chacha Zakayo Wangwe na kushinda kiti hicho baada ya kumshinda Mfanyabiashara Tajiri Kanda ya Ziwa mwenye kumiliki Mabasi na Visima vya Mafuta.

- Mgombea Ubunge Kura za M aoni ndani ya CHADEMA Uchaguzi mkuu wa 2010 lakini kura hazikutosha ndani ya CHADEMA
- Mgombea Uenyekiti wa Vijana wa CHADEMA Taifa 2009, Uchaguzi ulioharibika
- Kushiriki katika operesheni mbalimbali za chama, Oparesheni Sangara 2008-2010,
- Mratibu msaidizi wa kampeni za mgombea urais CHADEMA Nchi nzima.
- Kuzunguka nchi nzima kwenye kampeni za mgombea urais CHADEMA
- Kushiriki maandamano ya Arusha kupinga uchaguzi wa umeya
- Kushiriki oparesheni ya kanda ya ziwa kupinga DOWANS na kupanda kwa gharama za maisha.

Kazi alizofanya katika kipindi chake cha udiwani

Kujenga shule ya sekondari kata ya Tarime mjini(nyamisangura sekondari)
- Kusimamia ujenzi wa barabara za Tarime Mjini
- Kusimamia upatikanaji wa maji safi katika kata ya Tarime mjini.
- Kusimamia na kutetea haki za wanyonge
- Kufanya mikutano ya kujenga chama mikoa ya Mara(Musoma mjini,MugumuTarime), Mwanza (Nyamagana na Ilemela,Magu), Shinyanga (Bukombe) na Dar es Salaam.

MALENGO YAKE YA SASA:
Kwani nini aligombea uenyekiti
- Kuifanya BAVICHA kuwa taasisi imara itakayo toa viongozi makini wa chama na taifa kwa ujumla.
- Kuunganisha nguvu za vijana wa taifa hili katika kudai uhuru katika mapambano haya ya awamu ya pili, yanayolenga kusimamia rasilimali za nchi kutumika kwa maslahi ya Watanzania, kwa ajili ya kuwainua kiuchumi na kupunguza umaskini wao. Pia haki na usawa kwa Watanzania wote ili kujenga amani na utulivu wa kweli ulio imara.
- Kupigania ushiriki wa vijana katika siasa za Tanzania na nafasi za uongozi katika taifa
- Kuongoza BAVICHA kuisimamia serekali kuiwajibisha na kuihoji kuhusu maisha (ustawi) ya Watanzania na nchi kwa ujumla.
- Kuandaa tasisi itakayo tetea na kulinda chama na mali zake
- Kuunda taasisi itakayo waandaa vijana kuwa na uzalendo wa kitaifa uliopotea na kupigania maadili
- Kuunda baraza litakalo piga vita ufisadi, wizi na upendeleo kwa nguvu zote
- Kupigania kuunda baraza la vijana la taifa


VIONGOZI WANAOMVUTIA KISIASA
- Mwl Nyerere, Dr Slaa, Mbowe, Zitto
- Nelson Mandela na Franklin Roosevelt
KINACHOMCHUKIZA
- Ufisadi na siasa za udini.
- Kuhusu ufisadi, yeye hupenda kusema "Waafrika Kusini wakati wa ubaguzi wa rangi walikuwa na msemo unaosema "we want aperthaid removed not aperthaid reformed" wakiwa na maana wanataka kuondoa ubaguzi wa rangi sio kuurekebisha ubaguzi wa rangi na sisi vijana wa CHADEMA tunalengo la kuuondoa ufisadi na sio kuurekebisha ufisadi."

- Tanzania hakuna udini, kuna viongozi wachache wanaoficha udhaifu wao wa kiuongozi kwenye kapeti la udini, Watanzania ni wamoja wanashirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii, kisiasa na kimaendeleo kwa pamoja.

WITO
- Vijana wajiunge na CHADEMA kwa wingi kwa sababu CHADEMA ni chama pekee kinachopigania haki za wanyonge, kutetea rasimali za nchi na ndiyo tumaini jipya kwa Watanzania

- Anawaomba Vijana wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kupitia CHADEMA katika chaguzi mbalimbali kuanzia ndani ya chama na za kiserekali vijijini,vitongoji na uchaguzi mkuu ujao

- Anawaomba Watanzania wote kuiunga CHADEMA mkono na kuikataa CCM kwa kuwasababishia watanzania umasikini mkubwa kwa zaidi ya miaka 50.
 

Mkuu, this is very good!
Hivi kwanini mtu asiseme tu kwamba jamani habari za kazi, au atumie uhamasishaji unaofuatana na mauddhui ya mkutano/kika. Kwa mfano mtu kama yuko kwenye mkutano wa vijana, basi hata aseme : Vijana Juu! na siyo mambo ya Bwana asifiwe au asalaam Aleikum....
 

...Duuh!Almanusra kachozi kaniporomoke baba wa watu! Ungeendelea kama paragraph moja ungeniaibisha, maana niko moto sana.....
 

..anayeamini kwamba Mungu yupo na ni Mkuu kuliko vyote hasiti kutaja jina la Mungu! huo ndio ukweli! Mungu anaweza kubariki chama, nchi, mtu nk kuna tatizo gani kueleza hisia hizo km mtu anaamini hivyo..? mbona katiba inataja jina la Mungu? hata bunge letu huanza na sala kwa kutaja jina la Mungu hatujasikia mkisema waache! nijuavyo ni shetani na kundi lake tu ndio hukerwa jina la Mungu linapotukuzwa hata kwa kutamka tu!
 
JOHN HECHE SUGUTA

- Kuzaliwa – 1981 – katika kijiji cha Sirari, Tarime
- Shule 1989 – Nyamaharaga Primary
- Sekondari – 1997- Bulima Secondary
- Musoma Allience High School- 2001
- Stashahada ya Ualimu - 2004- 2006 Chuo cha Ualimu Bunda
- Shahada ya Sanaa na Elimu – 2006-2009 Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Nyegezi
Mwanza.

HARAKATI ZA KISIASA:
- Kujiunga na CHADEMA mwaka 2000
- Mmoja wa Waasisi na waanzilishi wa Tawi la CHADEMA Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Nyegezi Mwanza.
- Katibu wa Tawi la CHADEMA SAUT 2008

- Mgombea Udiwani katika Kata ya Tarime Mjini CHADEMA Uchaguzi Mdogo 2008 kuziba nafasi ya Marehemu Mh. Chacha Zakayo Wangwe na kushinda kiti hicho baada ya kumshinda Mfanyabiashara Tajiri Kanda ya Ziwa mwenye kumiliki Mabasi na Visima vya Mafuta.

- Mgombea Ubunge Kura za M aoni ndani ya CHADEMA Uchaguzi mkuu wa 2010 lakini kura hazikutosha ndani ya CHADEMA
- Mgombea Uenyekiti wa Vijana wa CHADEMA Taifa 2009, Uchaguzi ulioharibika
- Kushiriki katika operesheni mbalimbali za chama, Oparesheni Sangara 2008-2010,
- Mratibu msaidizi wa kampeni za mgombea urais CHADEMA Nchi nzima.
- Kuzunguka nchi nzima kwenye kampeni za mgombea urais CHADEMA
- Kushiriki maandamano ya Arusha kupinga uchaguzi wa umeya
- Kushiriki oparesheni ya kanda ya ziwa kupinga DOWANS na kupanda kwa gharama za maisha.
 
Hongera sana kaka,kaza buti,jua chama ni watu,sou should work for pipo,not for yourself.
 
..ww Mungu wako ni yupi? mfalme daud alipochukua mke wa askari wake Mungu alimwacha? kasome biblia vzr usiweke reference za Mungu kwa ubinafsi wako..unaona kijiti kwenye jicho la mwenzio wakati wewe una boriti.
Hongera Mh Mtema endelea mbele!
Kwa hiyo biblia inaruhusu watu wachukuliane wake kama daudi siyo?
Au ukichukua mke wa mtu ndio unatimiza andiko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…