Ndugu zangu wanaJF,
Nilikuwa nafuatilia mchakato wa uchaguzi uliokuwa ukiendelea ndani ya Baraza la Vijana Chadema Taifa, nimeshtushwa sana na kauli na maneno ya baadhi ya makada wa CCM, CUF, NCCR, UPDP,UDP ect. za kutaka baadhi ya vijana wawe viongozi.
Napingana na hawa wanasiasa uchwara ambao wana kazi ya kupandikiza viongozi ndani ya CDM kwa maslahi yao binafsi. Ukikuta CCM au chama kingine cha upinzani kinamshabikia sana kiongozi fulani ndani ya CDM au anagombea nafasi ya uongozi ujue kuna mawili, kwanza ni ama huyo anayemtaka awe kiongozi ni kipandikizi chake/mamluki au ana uwezo mdogo wa akili/ hana msimamo.
Nashukuru viongozi wetu wa CDM hasa Mwenyeki na Katibu wake hili wanalifahamu vizuri. Tunakumbuka uchaguzi wa Bavicha uliopita, tumeona Kafulila ambaye walikuwa wakimpigia debe eti ndio kiongozi mzuri leo yuko wapi? hana msimamo.
Kumbuka wakati tunataka Dr. Slaa agombee urais walijitokeza watu wengi sana wakitaka asigombee, kwa sababu gani? Ukifuatilia jibu liko wazi na walikuwa wanajua atashinda na atawashughulikia. Hata sasa bado wanamuogopa sana huyu bwana.
Kumbuka wakati Zitto anachukua fomu za kugombea umwenyekiti jinsi walivyompigia debe eti anafaa, ukiangalia na kitu alichokifanya mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kafanya nini, mnashindwa nini hapa? swala ni kwamba CCM hawakotayari kuona CDM inapata viongozi waadilifu na wenye misimamo ya kweli ya kuwatetea wananchi.
Juzi kwenye kuiunda kambi ya upinzani bungeni eti CCM wanashabikia Mbowe asiwe Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, lengo ni nini, wanajua kuwa mbowe ana msimamo wa weli.
Hadi juzi kuna wadau humu JF na kwenye media zingine nawaona wakijaribu kuwabeba na kuwachafua baadhi ya wagombea.
Kitu ambacho nawashauri wana CDM ni kuwa makini sana pale wanapokuta CCM, CUF, UDP, NCCR, UPDP, etc wanawaunga mkono baadhi ya viogozi au wagombea ndani ya CDM, ikiwezekana kufanyika kwa uchunguzi mkali kwa hao wanaoungwa mkono na wapinzani wao kisiasa.