John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Regia keep it up! Achana na akina Ms wametumwa hao. Magamba A & B Wanatumia kila njia kujinasua ila palipo nuru watu wenye hekima wataona na penye giza ni giza tu hata ulete mambo haya ya akina MS haisaidi wanapoteza muda na magamba yao.
 
Dada Regia asante kwa jibu Malaria Sugu. Akirudi tena tutamshughulikia.

Naomba list ya baraza letu la wazee lile linalowekaga mambo sawa.
 
Duh!..basi kamweka ghadafi,mubarak,assad,kim jong il....kwanini awaweke hawa kuwatawala viumbe vyake?....wamemkosea nini?

Nikurejeshe kidogo kwenye historia kidogo, hujui kwamba hata Sauli alimweka yeye lakini kwa kuwatahadharisha waliokuwa wakimuhitaji, hakuzuii kuchagua kiongozi umtakaye atakushauri na kukupa sifa za kiongozi anayefaa. Kisha anakupa uhuru wa kuchagua aidha kwa sifa hizo au kwa zile unazozitaka wewe hatakuzuia. Mwishoni mwa siku bado yeye ndiye mwenye nguzu zote juu ya utawala huo haijalishi ni mwema au mbaya

"....basi kamweka ghadafi,mubarak,assad,kim jong il...." Ndio wote hawa na wengine ni mamlaka ambazo ziko chini yake kama mlizitaka nyinyi kwamba ndizo zinazowafaa na mkazienzi yeye hata siku moja hatawazuia kuzichagua japo anao uwezo huo. Hii haimwondolei sifa ya kuwa MTAWALA juu ya Mamlaka zote kama alivyo Mtawala juu ya Binadam wote wema au wabaya na hajasema ngoja niwaue wabaya niwamalize.

LAKINI EBU TURUDI KWENYE MADA YETU YA MSINGI, TUENDELEE KUMPONGEZA NA KUMTAKIA HERI NA KUMPA SUPPORT NDG. YETU JOHN HECHE. HONGERA JOHN!!!
 
Malaria Sugu.Mimi siziwezi siasa zako za udini na Ukabila.Hizo peleka Kanisani na Misikitini na Ukabila peleka huko Kenya sio hapa Tanzania.Hapa kwetu Tanzania kuna Makabila 120 Ukabila hautawezekana. Kama nyie mnachagua watu kwasababu ya Kabila zao au dini zao basi kwetu hakuna uchaguzi wa dini kwakuwa hapa sio kanisani wala msikitini na wala hakuna uchaguzi wa kabila kwakuwa hatuchagui machifu wala mamwinyi. Tunachgua watu kulingana na merits zao bila kujali dini,kabila wala uwezo kifedha.

Jumapili njema

.
Tehe tehe tehee; binti Abraham kumbe upo hapa jamvini?
Malaria sugu ni kuachana nae tu maana hata kikombe cha babu hakikuweza kuyaondoa malaria yake, yenye parasite wa kijani na njano.
.
 
Malaria Sugu.Mimi siziwezi siasa zako za udini na Ukabila.Hizo peleka Kanisani na Misikitini na Ukabila peleka huko Kenya sio hapa Tanzania.Hapa kwetu Tanzania kuna Makabila 120 Ukabila hautawezekana. Kama nyie mnachagua watu kwasababu ya Kabila zao au dini zao basi kwetu hakuna uchaguzi wa dini kwakuwa hapa sio kanisani wala msikitini na wala hakuna uchaguzi wa kabila kwakuwa hatuchagui machifu wala mamwinyi. Tunachgua watu kulingana na merits zao bila kujali dini,kabila wala uwezo kifedha.

Jumapili njema

Pamoja sana Dada Regia.
 
Hongera sana Heche Big up!

Pongezi ziende kwako binafsi kwa Wazee waliosimamia uchaguzi na chama kwa ujumla angalia mbele husilewe sifa/madaraka wala husiogope lawama. Chadema sasa hivi ni adui Mkubwa wa wale wenye mlengo wa kuwa kuipinga CCM ni kuatarisha amani na usalama wa nchni, Chadema imeingia vitani na Polisi wa Tanzania na UWT umeona ya Tarime, Arusha na hata Bungeni nk Juwa kuwa hayo yanayoonekana nje ni chembe tu ya mamilioni ya mipango inayofanywa gizani umekubali kuingia katika hiyo vita na sasa unakuwa mstari wa mbele katika hiyo vita kaza roho na jipe moyo tutashinda.

Kuwa tayari kula na kulala jela inapobidi kama Lissu na wengineo kwa ajili ya kudai haki ya Watanzani Mungu atakulipa na ukweli utawekwa wazi siku ya mwisho. Umeomba kutumikia Wanachni umepata nafasi onyesha utumishi wako sasa.
 
hongera mkuu kwa kuchaguliwa na chama chako kwa nafasi hio

inaonyesha jinsi gani chama chako wanvyokuamini, kwa hio usiwaangushe
 
mbona heche huyohuyo ndio analalamikiwa na wana chadema kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kulipoteza jimbo la tarime kwa ccm,na wengine wanadiriki kusema kwamba kuchaguliwa kwake kutapelekea jimbo la tarime liendelee kushikiliwa na ccm mwaka 2015?.....

Wape hongera wajumbe wa bavicha walioshiriki na kufanya uchaguzi badala ya hao wazee wa chadema na viongozi wa chadema,kuwapa hongera hao wazee na viongozi kutawafanya baadhi ya watu wahisi kwamba john heche kachaguliwa na wazee wa chadema na viongozi wa chadema kitu ambacho si kweli...

Mwisho naomba kumpongeza sana john heche kwa kuchaguliwa,cha msingi apewe tu ushirikiano,ni kiongozi mzuri sana huyu.
mchawi mpe mtoto amlee!
 
Hatimaye CHADEMA tumevuka tanuru jingine la uchaguzi huu.Namshukuru MUNGU sana.Ndugu zangu CHADEMA hivi sasa imekua na kuwa na maadui wengi sana.Tunapigwa na vyama vyote vya siasa iwe chama kilichopo maradarakani au vya upinzani.Uchaguzi huu ulikuwa ni mtihani mwingine kwa chama.Wagombea wengi sana walijitokeza katika nafasi mbalimbali zilizotangazwa.Mwanzoni tulifurahi sana tukijua kuwa chama kimekuwa sana lakini humo humo wagombea ambao hawakuwa na nia njema na CHADEMA walijitokeza.Katika kila nafasii kulikuwa na wagombea ambao hawakuwaserious na lengo la kuitaka nafasi hiyo,wengine walikuwa wapo kwaajili ya kugawa kura,wengine waliomba kwaajili ya kuuza sura na wengine waliomba kwaajili ya maslahi binafsi/maslahi ya watu binafsi na kuna wengine walikuwa wanadhamira njema kabisa ya kutaka kuwatumikia vijana na kukijenga chama kwa maslahi ya chama.Pamoja na kwamba CHADEMA hatuna Kitengo thabiti cha Intelejensia(Kwa maana ya watu wenye Taaluma hii ).lakini kwakuwa chama hiki kina mkono wa MUNGU,MUNGU alitumia njia zake za asili kuwang'amua waliokuwa na nia mbaya.Baadhi yao wakaenguliwa kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu za chama na baadhi walishindwa kwenye sanduku la kura. Binafsi nilikuwa naziangalia nafasi nyeti ili zipate viongozi wazuri wenye nia nzuri ya kujenga chama na waliogombea kwa ridhaa zao sio kwa kuwekwa au kushawishiwa na watu fulani.
Nafasi ya Uenyekiti nimefurahi ameshinda John Heche na ndio alikuwa chaguo langu tangu mwanzo 2009.Heche ana misimamo anaweza kusimamia misimamo yake na anamalengo mazuri na BAVICHA.Amegombea kwa ridhaa yake. HONGERA chalii Heche.
Nasubiri kuona tunapata Katibu Mkuu , Mwekahazina na Mratibu wa Uhamasishaji wazuri kwa maslahi ya chama.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.
Bibie inabidi ukubali kutopenda sana kutumia imani yako kuzungumzia chama kwa ujumla wake...
Yawezekana kabisa ndivyo ulivyofundishwa nyumbani lakini kama walivyosema wengine hapo nyuma. jaribu sana kuepuka kutumia dini ktk Siasa, wajinga wengi hawatakuelewa kwani kama walivyosema Mungu wako anaweza kuwa shetani kwao!. Kwa tafsiri ile ile ulotumia kumaanisha kwamba - Vyama vingine havina mkono wa Mungu isipokuwa Chadema!

Na ninewasoma sana humu wana Chadema wakipenda sana kutumia dini kuzungumzia ama kukielezea chama lakini hao hao wepesi kupinga Udini ili hali matumizi ya lugha zao huwafanya watu wengine kujiuliza maswali magumu. Wewe kama ni mchungaji na unaongozwa na roho mtakatifu, hii ni imani yako wewe lakini sii vizuri kuaminisha wananchi kwamba Chadema ina mkono wa Mungu jambo ambalo sisi wengine hatuamini kabisa kwamba Mungu kaweka mkono wake Chadema au baraka zake ziko Chadema - Wanabarikiwa ni wanadamu na sii chama.

Nitarudia kusema statement kama hizi hazifai na ningeomba sana na kuishauri hata serikali ule mtindo wa viongozi wetu wa kiserikali na kisiasa ktk kufungua mikutano wakisema Asalaam Aleikum, kisha - Bwana Asifiwe ni mwanzo wa kuleta Dini ktk siasa kwani mnajiweka ktk imani mbili za dini. Na hakika kisiasa inajenga nguvu mbili za mapambano ya kiimani ktk siasa hivyo vyama vyote vya kisiasa vinafungwa ktk imani hizi.

Binafsi sielewi kwa nini kiongozi aseme Asalaam Aleikum neno la kiarabu ambalo tafsiri yake kwa kiswahili ni - Amani iwe juu yenu, kama halihusiani na dini fulani au Bwana asifiwe - huyu bwana nani?..

Jamani wengine tunaamini Mungu na matumizi yake yasitumiwe ovyo ovyo hata pale mnapotoa ahadi za uongo ama hamna hakika na myasemayo. Kuendesha hotuba za kisiasa kwa kuzitumia dini zetu ni makosa makubwa sana na inajenga Udini kwani kama utaongopa ili hali umeanza kwa kumsifia Mwenyezi Mungu -haya ni matusi makubwa wa waumini wa dini hiyo...
Siasa zibakie siasa na maswala ya Mungu yapelekwe huko Makanisani na misikitini..
 
Malaria Sugu.Mimi siziwezi siasa zako za udini na Ukabila.Hizo peleka Kanisani na Misikitini na Ukabila peleka huko Kenya sio hapa Tanzania.Hapa kwetu Tanzania kuna Makabila 120 Ukabila hautawezekana. Kama nyie mnachagua watu kwasababu ya Kabila zao au dini zao basi kwetu hakuna uchaguzi wa dini kwakuwa hapa sio kanisani wala msikitini na wala hakuna uchaguzi wa kabila kwakuwa hatuchagui machifu wala mamwinyi. Tunachgua watu kulingana na merits zao bila kujali dini,kabila wala uwezo kifedha.

Jumapili njema
Dada Regia kuna wengine ambao kwao mambo ya udini yako kwenye damu hawawezi kuishi bila hilo ni kuwa potezea.

Hongera sana viongozi na Chadema kwa ujumla binafsi nimefarijika sana kwa mpambanaji Heche kuchaguliwa naujua uwezo wake namjua alivyo committed sisemi wagombea wengine hawakuwa na uwezo hapana ila whatever the case bado alitakiwa mtu mmoja tu.

Ombi langu kwenu viongozi,

Wapeni ushirikiano mzuri wagombea wote waliochaguliwa leo najua kila kiongozi (mtu) alikuwa na pendekezo lake kichwani lakini demokrasia imefuata mkondo wake ipeni heshima yake ili itawale hatutaki CDM iwe na makundi kama wenzenu wanavyoonekana sasa. Najua Heche na wengine ni wachanga kwenye mambo mengi ya siasa watajaribu kuja na plan zao ambazo zingine zitaoneka mpya kwenu zingine zitaonekana za ajabu kwenu lakini hebu mjitahidi kuwaelewa na kuwaelekeza panapostahili na si kuwakatisha tamaa.

Wosia kwa Heche na waliochaguliwa,

Uongozi ni dhamana watu wamewaamini wameweka matumaini yao kwenu ili muweze ku deliver kwa niaba yao mkishindwa kufanya hilo watu hao hao waliowapa kura leo watawaondoeni, kwa hiyo leo mnafurahia kura zao na mmewaona wa maana sana naomba kesho watakapoamua kuzichukua kura zao muwaone wa maana vile vile, i mean, wanachama ndio waajiri wenu siku wakiwafukuza kazi kwa kutotekeleza walichowatumeni msianze kulalamika na kujenda makundi, fanyeni kazi mliyotumwa mkaijenge Chadema na taifa.

Wosia kwa wagombea ambao hawakubahatika kuchaguliwa,

Kipindi hiki ndicho cha kuonesha ukomavu wa akili sote tunajua katika ushindani hakika mshindi lazima awe mmoja kwa hiyo si busara kuanza kunung'unika pembeni kama una malalamiko genuine ni bora ukaufahamisha uongozi zaidi ya hapo utaonekana hukuwa na malengo kama yao ulikuwa na malengo yako na ikiwa utaendelea kunung'unika pembeni hakika nakuambia ndio utakuwa mwanzo na mwisho wako kisiasa hata kama ukiamua kuhamia chama kingine watakupokea si kwa kuwa wewe ni jasiri ni kwa sababu ya malengo yao wakitimiza watakusahau, jijengeeni heshima kwa kuwapa ushirikiano walioshinda mapambano ni sehemu yeyote si lazima wote tuwe viongozi leo wao kesho mtakuwa nyie tena inawezekana kwa ngazi za juu zaidi.
 
Ndugu zangu wanaJF,

Nilikuwa nafuatilia mchakato wa uchaguzi uliokuwa ukiendelea ndani ya Baraza la Vijana Chadema Taifa, nimeshtushwa sana na kauli na maneno ya baadhi ya makada wa CCM, CUF, NCCR, UPDP,UDP ect. za kutaka baadhi ya vijana wawe viongozi.

Napingana na hawa wanasiasa uchwara ambao wana kazi ya kupandikiza viongozi ndani ya CDM kwa maslahi yao binafsi. Ukikuta CCM au chama kingine cha upinzani kinamshabikia sana kiongozi fulani ndani ya CDM au anagombea nafasi ya uongozi ujue kuna mawili, kwanza ni ama huyo anayemtaka awe kiongozi ni kipandikizi chake/mamluki au ana uwezo mdogo wa akili/ hana msimamo.
Nashukuru viongozi wetu wa CDM hasa Mwenyeki na Katibu wake hili wanalifahamu vizuri. Tunakumbuka uchaguzi wa Bavicha uliopita, tumeona Kafulila ambaye walikuwa wakimpigia debe eti ndio kiongozi mzuri leo yuko wapi? hana msimamo.

Kumbuka wakati tunataka Dr. Slaa agombee urais walijitokeza watu wengi sana wakitaka asigombee, kwa sababu gani? Ukifuatilia jibu liko wazi na walikuwa wanajua atashinda na atawashughulikia. Hata sasa bado wanamuogopa sana huyu bwana.

Kumbuka wakati Zitto anachukua fomu za kugombea umwenyekiti jinsi walivyompigia debe eti anafaa, ukiangalia na kitu alichokifanya mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kafanya nini, mnashindwa nini hapa? swala ni kwamba CCM hawakotayari kuona CDM inapata viongozi waadilifu na wenye misimamo ya kweli ya kuwatetea wananchi.

Juzi kwenye kuiunda kambi ya upinzani bungeni eti CCM wanashabikia Mbowe asiwe Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, lengo ni nini, wanajua kuwa mbowe ana msimamo wa weli.

Hadi juzi kuna wadau humu JF na kwenye media zingine nawaona wakijaribu kuwabeba na kuwachafua baadhi ya wagombea.

Kitu ambacho nawashauri wana CDM ni kuwa makini sana pale wanapokuta CCM, CUF, UDP, NCCR, UPDP, etc wanawaunga mkono baadhi ya viogozi au wagombea ndani ya CDM, ikiwezekana kufanyika kwa uchunguzi mkali kwa hao wanaoungwa mkono na wapinzani wao kisiasa.
Acaha kutafuta sifa za kijinga. Nani anamuda wakufuatilia uchaguzi wa uongozi wa chadema? Kweli ujinga ni mzigo.
 
Malaria Sugu.Mimi siziwezi siasa zako za udini na Ukabila.Hizo peleka Kanisani na Misikitini na Ukabila peleka huko Kenya sio hapa Tanzania.Hapa kwetu Tanzania kuna Makabila 120 Ukabila hautawezekana. Kama nyie mnachagua watu kwasababu ya Kabila zao au dini zao basi kwetu hakuna uchaguzi wa dini kwakuwa hapa sio kanisani wala msikitini na wala hakuna uchaguzi wa kabila kwakuwa hatuchagui machifu wala mamwinyi. Tunachgua watu kulingana na merits zao bila kujali dini,kabila wala uwezo kifedha.

Jumapili njema
Yaani Nape Nnauye kama angekuwa na hoja za hekima na busara kama zako wewe!....hakika hata yeye tungemuheshimu sana! Lakini yeye kila hakiingia hapa jamvini ni kumwaga utumbo tuuu kisha anatokomea. lol!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Bibie inabidi ukubali kutopenda sana kutumia imani yako kuzungumzia chama kwa ujumla wake...
Yawezekana kabisa ndivyo ulivyofundishwa nyumbani lakini kama walivyosema wengine hapo nyuma. jaribu sana kuepuka kutumia dini ktk Siasa, wajinga wengi hawatakuelewa kwani kama walivyosema Mungu wako anaweza kuwa shetani kwao!. Kwa tafsiri ile ile ulotumia kumaanisha kwamba - Vyama vingine havina mkono wa Mungu isipokuwa Chadema!

Na ninewasoma sana humu wana Chadema wakipenda sana kutumia dini kuzungumzia ama kukielezea chama lakini hao hao wepesi kupinga Udini ili hali matumizi ya lugha zao huwafanya watu wengine kujiuliza maswali magumu. Wewe kama ni mchungaji na unaongozwa na roho mtakatifu, hii ni imani yako wewe lakini sii vizuri kuaminisha wananchi kwamba Chadema ina mkono wa Mungu jambo ambalo sisi wengine hatuamini kabisa kwamba Mungu kaweka mkono wake Chadema au baraka zake ziko Chadema - Wanabarikiwa ni wanadamu na sii chama.

Nitarudia kusema statement kama hizi hazifai na ningeomba sana na kuishauri hata serikali ule mtindo wa viongozi wetu wa kiserikali na kisiasa ktk kufungua mikutano wakisema Asalaam Aleikum, kisha - Bwana Asifiwe ni mwanzo wa kuleta Dini ktk siasa kwani mnajiweka ktk imani mbili za dini. Na hakika kisiasa inajenga nguvu mbili za mapambano ya kiimani ktk siasa hivyo vyama vyote vya kisiasa vinafungwa ktk imani hizi.

Binafsi sielewi kwa nini kiongozi aseme Asalaam Aleikum neno la kiarabu ambalo tafsiri yake kwa kiswahili ni - Amani iwe juu yenu, kama halihusiani na dini fulani au Bwana asifiwe - huyu bwana nani?..

Jamani wengine tunaamini Mungu na matumizi yake yasitumiwe ovyo ovyo hata pale mnapotoa ahadi za uongo ama hamna hakika na myasemayo. Kuendesha hotuba za kisiasa kwa kuzitumia dini zetu ni makosa makubwa sana na inajenga Udini kwani kama utaongopa ili hali umeanza kwa kumsifia Mwenyezi Mungu -haya ni matusi makubwa wa waumini wa dini hiyo...
Siasa zibakie siasa na maswala ya Mungu yapelekwe huko Makanisani na misikitini..

Asante kwa mtazamo wako na si kila mmoja atakubalina na hoja yako.Kwa hili tunaweza kupingana mpaka asubuhi.Mi nadhani tukubaliane kutokukubaliana.I respect you alot ndio maana sitaki kubishana na wewe.

HONGERA SANA CHalii Heche.
Nakutakia week end njema...
 
Haya kobello unalingine?....siku zenu zinahesabika mkuu! kaeni chonjo jahazi la magamba linazama
Kwa taarifa yako,mimi nipo kwenye kundi linalopigwa sana vita ndani ya CCM....too radical!
Rais wangu akiapishwa 2015,wageni waalikwa hawatakuwa kina museveni na kibaki,bali Chavez,morales,lula......
 
Mkandara kama haya ndiyo mawazo yako nafikiri hujui tofauti ya dini na udini kusema mimi nimesaidiwa na Mungu si udini, jaribu kutofautisha anayosema Malaria Sugu na aliyosema Regia tena Regia kamwambia wazi MS yeye haziwezi siasa za makanisani na misikitini ulikuwa unataka asitaje neno Mungu ndipo uone hana udini sikuelewi otherwise labda niseme ulikuwa na sababu zako za kusema hivyo, tuseme basi na wewe wakati unaelezea kwenye statement yako uliposema Asalaam Aleikum, - Bwana Asifiwe ni mdini.
 
Asante kwa mtazamo wako na si kila mmoja atakubalina na hoja yako.Kwa hili tunaweza kupingana mpaka asubuhi.Mi nadhani tukubaliane kutokukubaliana.I respect you alot ndio maana sitaki kubishana na wewe.

HONGERA SANA CHalii Heche.
Nakutakia week end njema...
Bibie hata mimi naku respect na sidhani kama hili linahusu sana ktk kujieleza ama kujenga hoja. Kama hukubaliani nami ni vizuri kunielimisha unavyoelewa wewe ili nami nijipime ktk maelezo yangu. Pengine fafanua haya maneno yako ulikuwa na maana gani?... kwani inanitatiza sana kuelewa ikiwa sintotumia msahafu wa imani ya dini..

lakini kwakuwa chama hiki kina mkono wa MUNGU,MUNGU alitumia njia zake za asili kuwang'amua waliokuwa na nia mbaya.
 
Kwa taarifa yako,mimi nipo kwenye kundi linalopigwa sana vita ndani ya CCM....too radical!
Rais wangu akiapishwa 2015,wageni waalikwa hawatakuwa kina museveni na kibaki,bali Chavez,morales,lula......
Ok nimekuelewa....kwa maana hiyo wewe uko kundi la mapacha 3 a.k.a Rachel? Na kwanini wageni waalikwa wawe Chavez,Morales nk?
 
Mkandara kama haya ndiyo mawazo yako nafikiri hujui tofauti ya dini na udini kusema mimi nimesaidiwa na Mungu si udini, jaribu kutofautisha anayosema Malaria Sugu na aliyosema Regia tena Regia kamwambia wazi MS yeye haziwezi siasa za makanisani na misikitini ulikuwa unataka asitaje neno Mungu ndipo uone hana udini sikuelewi otherwise labda niseme ulikuwa na sababu zako za kusema hivyo, tuseme basi na wewe wakati unaelezea kwenye statement yako uliposema Asalaam Aleikum, - Bwana Asifiwe ni mdini.
Mkuu nimekemea matumizi ya maneno hayo ktk siasa, hivyo kukemea na kutumia ni vitu viwili tofauti. Bibie aliposema Kwa kuwa chama hiki kina Mkono wa Mungu hii ni kuaminisha watu kwamba Mungu anakilinda chama jambo ambalo ktk imani yangu halipo.. Hivyo unanifanya mimi mifikirie kama wewe au kupinga hata hojha nzima kuwa ni propaganda za kidini. Na sijui kama nimesema makosa ya Regia Mtema ni Udini ila nimemuomba sana kutopenda kutumia imani yake ya dini ktk maswala ya kisiasa kwa sababu Wajinga hawataelewa... Hapa nikiwa na maana wajinga ni wale wasioamini au kuelimika ktk imani ya dini yake.
 
Back
Top Bottom