John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Regia keep it up! Achana na akina Ms wametumwa hao. Magamba A & B Wanatumia kila njia kujinasua ila palipo nuru watu wenye hekima wataona na penye giza ni giza tu hata ulete mambo haya ya akina MS haisaidi wanapoteza muda na magamba yao.
 
Dada Regia asante kwa jibu Malaria Sugu. Akirudi tena tutamshughulikia.

Naomba list ya baraza letu la wazee lile linalowekaga mambo sawa.
 
Duh!..basi kamweka ghadafi,mubarak,assad,kim jong il....kwanini awaweke hawa kuwatawala viumbe vyake?....wamemkosea nini?

Nikurejeshe kidogo kwenye historia kidogo, hujui kwamba hata Sauli alimweka yeye lakini kwa kuwatahadharisha waliokuwa wakimuhitaji, hakuzuii kuchagua kiongozi umtakaye atakushauri na kukupa sifa za kiongozi anayefaa. Kisha anakupa uhuru wa kuchagua aidha kwa sifa hizo au kwa zile unazozitaka wewe hatakuzuia. Mwishoni mwa siku bado yeye ndiye mwenye nguzu zote juu ya utawala huo haijalishi ni mwema au mbaya

"....basi kamweka ghadafi,mubarak,assad,kim jong il...." Ndio wote hawa na wengine ni mamlaka ambazo ziko chini yake kama mlizitaka nyinyi kwamba ndizo zinazowafaa na mkazienzi yeye hata siku moja hatawazuia kuzichagua japo anao uwezo huo. Hii haimwondolei sifa ya kuwa MTAWALA juu ya Mamlaka zote kama alivyo Mtawala juu ya Binadam wote wema au wabaya na hajasema ngoja niwaue wabaya niwamalize.

LAKINI EBU TURUDI KWENYE MADA YETU YA MSINGI, TUENDELEE KUMPONGEZA NA KUMTAKIA HERI NA KUMPA SUPPORT NDG. YETU JOHN HECHE. HONGERA JOHN!!!
 

.
Tehe tehe tehee; binti Abraham kumbe upo hapa jamvini?
Malaria sugu ni kuachana nae tu maana hata kikombe cha babu hakikuweza kuyaondoa malaria yake, yenye parasite wa kijani na njano.
.
 

Pamoja sana Dada Regia.
 
Hongera sana Heche Big up!

Pongezi ziende kwako binafsi kwa Wazee waliosimamia uchaguzi na chama kwa ujumla angalia mbele husilewe sifa/madaraka wala husiogope lawama. Chadema sasa hivi ni adui Mkubwa wa wale wenye mlengo wa kuwa kuipinga CCM ni kuatarisha amani na usalama wa nchni, Chadema imeingia vitani na Polisi wa Tanzania na UWT umeona ya Tarime, Arusha na hata Bungeni nk Juwa kuwa hayo yanayoonekana nje ni chembe tu ya mamilioni ya mipango inayofanywa gizani umekubali kuingia katika hiyo vita na sasa unakuwa mstari wa mbele katika hiyo vita kaza roho na jipe moyo tutashinda.

Kuwa tayari kula na kulala jela inapobidi kama Lissu na wengineo kwa ajili ya kudai haki ya Watanzani Mungu atakulipa na ukweli utawekwa wazi siku ya mwisho. Umeomba kutumikia Wanachni umepata nafasi onyesha utumishi wako sasa.
 
hongera mkuu kwa kuchaguliwa na chama chako kwa nafasi hio

inaonyesha jinsi gani chama chako wanvyokuamini, kwa hio usiwaangushe
 
mchawi mpe mtoto amlee!
 
Bibie inabidi ukubali kutopenda sana kutumia imani yako kuzungumzia chama kwa ujumla wake...
Yawezekana kabisa ndivyo ulivyofundishwa nyumbani lakini kama walivyosema wengine hapo nyuma. jaribu sana kuepuka kutumia dini ktk Siasa, wajinga wengi hawatakuelewa kwani kama walivyosema Mungu wako anaweza kuwa shetani kwao!. Kwa tafsiri ile ile ulotumia kumaanisha kwamba - Vyama vingine havina mkono wa Mungu isipokuwa Chadema!

Na ninewasoma sana humu wana Chadema wakipenda sana kutumia dini kuzungumzia ama kukielezea chama lakini hao hao wepesi kupinga Udini ili hali matumizi ya lugha zao huwafanya watu wengine kujiuliza maswali magumu. Wewe kama ni mchungaji na unaongozwa na roho mtakatifu, hii ni imani yako wewe lakini sii vizuri kuaminisha wananchi kwamba Chadema ina mkono wa Mungu jambo ambalo sisi wengine hatuamini kabisa kwamba Mungu kaweka mkono wake Chadema au baraka zake ziko Chadema - Wanabarikiwa ni wanadamu na sii chama.

Nitarudia kusema statement kama hizi hazifai na ningeomba sana na kuishauri hata serikali ule mtindo wa viongozi wetu wa kiserikali na kisiasa ktk kufungua mikutano wakisema Asalaam Aleikum, kisha - Bwana Asifiwe ni mwanzo wa kuleta Dini ktk siasa kwani mnajiweka ktk imani mbili za dini. Na hakika kisiasa inajenga nguvu mbili za mapambano ya kiimani ktk siasa hivyo vyama vyote vya kisiasa vinafungwa ktk imani hizi.

Binafsi sielewi kwa nini kiongozi aseme Asalaam Aleikum neno la kiarabu ambalo tafsiri yake kwa kiswahili ni - Amani iwe juu yenu, kama halihusiani na dini fulani au Bwana asifiwe - huyu bwana nani?..

Jamani wengine tunaamini Mungu na matumizi yake yasitumiwe ovyo ovyo hata pale mnapotoa ahadi za uongo ama hamna hakika na myasemayo. Kuendesha hotuba za kisiasa kwa kuzitumia dini zetu ni makosa makubwa sana na inajenga Udini kwani kama utaongopa ili hali umeanza kwa kumsifia Mwenyezi Mungu -haya ni matusi makubwa wa waumini wa dini hiyo...
Siasa zibakie siasa na maswala ya Mungu yapelekwe huko Makanisani na misikitini..
 
Dada Regia kuna wengine ambao kwao mambo ya udini yako kwenye damu hawawezi kuishi bila hilo ni kuwa potezea.

Hongera sana viongozi na Chadema kwa ujumla binafsi nimefarijika sana kwa mpambanaji Heche kuchaguliwa naujua uwezo wake namjua alivyo committed sisemi wagombea wengine hawakuwa na uwezo hapana ila whatever the case bado alitakiwa mtu mmoja tu.

Ombi langu kwenu viongozi,

Wapeni ushirikiano mzuri wagombea wote waliochaguliwa leo najua kila kiongozi (mtu) alikuwa na pendekezo lake kichwani lakini demokrasia imefuata mkondo wake ipeni heshima yake ili itawale hatutaki CDM iwe na makundi kama wenzenu wanavyoonekana sasa. Najua Heche na wengine ni wachanga kwenye mambo mengi ya siasa watajaribu kuja na plan zao ambazo zingine zitaoneka mpya kwenu zingine zitaonekana za ajabu kwenu lakini hebu mjitahidi kuwaelewa na kuwaelekeza panapostahili na si kuwakatisha tamaa.

Wosia kwa Heche na waliochaguliwa,

Uongozi ni dhamana watu wamewaamini wameweka matumaini yao kwenu ili muweze ku deliver kwa niaba yao mkishindwa kufanya hilo watu hao hao waliowapa kura leo watawaondoeni, kwa hiyo leo mnafurahia kura zao na mmewaona wa maana sana naomba kesho watakapoamua kuzichukua kura zao muwaone wa maana vile vile, i mean, wanachama ndio waajiri wenu siku wakiwafukuza kazi kwa kutotekeleza walichowatumeni msianze kulalamika na kujenda makundi, fanyeni kazi mliyotumwa mkaijenge Chadema na taifa.

Wosia kwa wagombea ambao hawakubahatika kuchaguliwa,

Kipindi hiki ndicho cha kuonesha ukomavu wa akili sote tunajua katika ushindani hakika mshindi lazima awe mmoja kwa hiyo si busara kuanza kunung'unika pembeni kama una malalamiko genuine ni bora ukaufahamisha uongozi zaidi ya hapo utaonekana hukuwa na malengo kama yao ulikuwa na malengo yako na ikiwa utaendelea kunung'unika pembeni hakika nakuambia ndio utakuwa mwanzo na mwisho wako kisiasa hata kama ukiamua kuhamia chama kingine watakupokea si kwa kuwa wewe ni jasiri ni kwa sababu ya malengo yao wakitimiza watakusahau, jijengeeni heshima kwa kuwapa ushirikiano walioshinda mapambano ni sehemu yeyote si lazima wote tuwe viongozi leo wao kesho mtakuwa nyie tena inawezekana kwa ngazi za juu zaidi.
 
Acaha kutafuta sifa za kijinga. Nani anamuda wakufuatilia uchaguzi wa uongozi wa chadema? Kweli ujinga ni mzigo.
 
Yaani Nape Nnauye kama angekuwa na hoja za hekima na busara kama zako wewe!....hakika hata yeye tungemuheshimu sana! Lakini yeye kila hakiingia hapa jamvini ni kumwaga utumbo tuuu kisha anatokomea. lol!
 
Reactions: LAT

Asante kwa mtazamo wako na si kila mmoja atakubalina na hoja yako.Kwa hili tunaweza kupingana mpaka asubuhi.Mi nadhani tukubaliane kutokukubaliana.I respect you alot ndio maana sitaki kubishana na wewe.


HONGERA SANA CHalii Heche.
Nakutakia week end njema...
 
Haya kobello unalingine?....siku zenu zinahesabika mkuu! kaeni chonjo jahazi la magamba linazama
Kwa taarifa yako,mimi nipo kwenye kundi linalopigwa sana vita ndani ya CCM....too radical!
Rais wangu akiapishwa 2015,wageni waalikwa hawatakuwa kina museveni na kibaki,bali Chavez,morales,lula......
 
Mkandara kama haya ndiyo mawazo yako nafikiri hujui tofauti ya dini na udini kusema mimi nimesaidiwa na Mungu si udini, jaribu kutofautisha anayosema Malaria Sugu na aliyosema Regia tena Regia kamwambia wazi MS yeye haziwezi siasa za makanisani na misikitini ulikuwa unataka asitaje neno Mungu ndipo uone hana udini sikuelewi otherwise labda niseme ulikuwa na sababu zako za kusema hivyo, tuseme basi na wewe wakati unaelezea kwenye statement yako uliposema Asalaam Aleikum, - Bwana Asifiwe ni mdini.
 
Bibie hata mimi naku respect na sidhani kama hili linahusu sana ktk kujieleza ama kujenga hoja. Kama hukubaliani nami ni vizuri kunielimisha unavyoelewa wewe ili nami nijipime ktk maelezo yangu. Pengine fafanua haya maneno yako ulikuwa na maana gani?... kwani inanitatiza sana kuelewa ikiwa sintotumia msahafu wa imani ya dini..

lakini kwakuwa chama hiki kina mkono wa MUNGU,MUNGU alitumia njia zake za asili kuwang'amua waliokuwa na nia mbaya.
 
Kwa taarifa yako,mimi nipo kwenye kundi linalopigwa sana vita ndani ya CCM....too radical!
Rais wangu akiapishwa 2015,wageni waalikwa hawatakuwa kina museveni na kibaki,bali Chavez,morales,lula......
Ok nimekuelewa....kwa maana hiyo wewe uko kundi la mapacha 3 a.k.a Rachel? Na kwanini wageni waalikwa wawe Chavez,Morales nk?
 
Mkuu nimekemea matumizi ya maneno hayo ktk siasa, hivyo kukemea na kutumia ni vitu viwili tofauti. Bibie aliposema Kwa kuwa chama hiki kina Mkono wa Mungu hii ni kuaminisha watu kwamba Mungu anakilinda chama jambo ambalo ktk imani yangu halipo.. Hivyo unanifanya mimi mifikirie kama wewe au kupinga hata hojha nzima kuwa ni propaganda za kidini. Na sijui kama nimesema makosa ya Regia Mtema ni Udini ila nimemuomba sana kutopenda kutumia imani yake ya dini ktk maswala ya kisiasa kwa sababu Wajinga hawataelewa... Hapa nikiwa na maana wajinga ni wale wasioamini au kuelimika ktk imani ya dini yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…