John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Regia huwa unagombana na watu hapa kwa sbabu ya kutofikiria unachoandika. Sasa wewe ni kiongozi wa chama, baada ya uchaguzi unatoka na kauli eti alikuwa chaguo langu. Huu ni upuuzi mwingine. Huoni kwamba unawajeruhi walioshindwa? Hivi kwanini usiamini uchaguzi umeisha na vimaneno vimeisha kwahiyo inatakiwa kusonga mbele.
Hivi huo mkono wa Mungu ukoje? Kina nani waliwaambiwa kuwa ni mkono wa Mungu? Wasio amini katika Mungu au huo mkono wana nafasi? Hebu angalia kauli zako na ziweke ziwe zenye kubeba maana ya kuwakilisha Watanzania wote na si watu wachache.
 

Heee,ulisha muandaa kugombea ubunge?
Taratibu mwenyekiti,nenda taratibu sana!
Tusubiri tuone anaweza kufanya nini ndo useme hayo,kwa sasa utakua unanyima
watu uhuru wa kuamua kugombea nafasi,huku ndo kupeana mwenyekiti na sio kuzuri
 
Sorry Mkuu sikuiona hii post nami nikawa najiandaa kumuweka sawa dada Regia. Anajisahau saana na kukibebesha lawama chama. Anahitaji kuwa mwangalifu saana kwenye kuandika na kuongea. Kama haiwezekani bora kuacha kabisa.
 
Bora wangempitisha















deogratius Kisandu na siyo huyo aliyesababisha jimbo likapotea
 
Hebu nipe udini kwenye statement hii na kama kuna udini imebase kwenye dini gani kama haijabase ni general statement hakuna udini hapo kwa taarifa yako tu Mungu hana dini.
Originally Posted by Regia Mtema
lakini kwakuwa chama hiki kina mkono wa MUNGU,MUNGU alitumia njia zake za asili kuwang'amua waliokuwa na nia mbaya.
Yaani siku hizi udini umekuwa sensitive hadi tuogope kumtaja Mungu NO WAY hatuwezi kuacha kumtaja Mungu kwa kuogopa kuitwa wadini.
 

Mkuu Regy,...
shikamoo kwanza na habari za siku!
Binafsi sio nilipenda mchange awe mwenyekiti,lakini kwa kua alienguliwa ina
ongeza credit kwenye imani yangu kwamba "TRUST NO POLITICIAN",...

Kwanini unaamini kwamba Heche sio msaliti?
Keep in mind kwamba kuna "professional actors " hujawahi shuhudia,unaweza
gundua ni msaliti baada ya kumaliza mission yake na sio mwanzo,...

All in all,tushukuru mwenyekiti kapatikana,anaipenda vipi chadema tutaona matokeo ya
uongozi wake,mara nyingi naona ni vyema mtu akapewa sifa mwishoni kabisa!

Naungana na wote wanao sifia mtu akifa,hapa wanakua wana fanya summation ya
ni jinsi gani mtu huyu alikua,

Heche tuta mpima uwezo wake wa uongozi na uaminifu wake kwa chama
baada ya mda wake wa uongozi kuisha!

Tulisifia viongozi wengi kweli wanapokua wanaanza kazi zao (JK kwa mfano),ila
matokeo yake ndo kama tunayo ona!

As for now,nampa support yote kufanya kazi yake vyema!
 

This is painfull to other candidates sister,don't show
your side now,it's even worse as we're still making the other kakaz
to come down
 
hongera dada. lkn anatokea mkoa gani huyo? na sisi wa\pwani pwani tutakumbukwa lini cdm? au tuhamie huko sote?

Ukanda hauna nafasi jombaa,
I trusted Mchange sio kwa kua ni mtu wa
pwani au kwa kua ni muislam
 
It is a balanced statement kweli kwenye politics kuna professional actors unaweza kumdhani ndiye kumbe siye, lakini in other hand trust nayo lazima i play part vinginevyo tukiwa na hisia nyingi tutamhisi kila mtu hatutafanyakazi, kibinadamu huwezi kumwamni mtu kwa 100% hata kama ni m/ke wako mnayelala naye kitanda kimoja kila siku, tuwape muda tuwaone ila trust yangu ilikuwa na bado iko kwa Heche.
 
Khaa!! jamani, hoja ijibiwe hapa,sio mnajaza sredi kwa post za ng.uruwe pori tu,mwenye details amwage tuone!!coz naona kama kuna hoja hapa!!

Sredi ndio kitu gani tena hicho?!
 

Yeah,ndo maana nikasema pamoja na kumuamini,asidhani Heche ni "Malaika aloshushwa na Mungu kuongoza bavicha"
Ampe support lakini ategemee lolote!

Simwamini Heche,lakini haimaanishi pale ntakapo takiwa kumpa support sitafanya hivo,
nita muunga mkono ila ni juu yake kuonesha kwamba anastahili kuaminiwa kweli!

Bado kidonda cha Tarime kwenda ccm naamini kime sababishwa na Heche,hii tu inatosha
kunifanya nisi muamini kabisaaaaaa!

But,twende mbele,tutasahau ya nyuma soon!
 

Nadhani siyo sawa sana maana aliyevuruga ule uchaguzi ni yule aliyegombea kwa ticket ya CUF baada ya kukosa nafasi ya kugombea kwa ticket ya Chadema labda jaribu kufuatilia hilo swala upya naona kama unalichukulia juu juu kama wanavyoliongelea watu humu kwenye thread za kampeni za BAVICHA
 
Originally Posted by Mkandara
Bibie inabidi ukubali kutopenda sana kutumia imani yako kuzungumzia chama kwa ujumla wake...
Yawezekana kabisa ndivyo ulivyofundishwa nyumbani lakini kama walivyosema wengine hapo nyuma. jaribu sana kuepuka kutumia dini ktk Siasa, wajinga wengi hawatakuelewa kwani kama walivyosema Mungu wako anaweza kuwa shetani kwao!. Kwa tafsiri ile ile ulotumia kumaanisha kwamba - Vyama vingine havina mkono wa Mungu isipokuwa Chadema!

Na ninewasoma sana humu wana Chadema wakipenda sana kutumia dini kuzungumzia ama kukielezea chama lakini hao hao wepesi kupinga Udini ili hali matumizi ya lugha zao huwafanya watu wengine kujiuliza maswali magumu. Wewe kama ni mchungaji na unaongozwa na roho mtakatifu, hii ni imani yako wewe lakini sii vizuri kuaminisha wananchi kwamba Chadema ina mkono wa Mungu jambo ambalo sisi wengine hatuamini kabisa kwamba Mungu kaweka mkono wake Chadema au baraka zake ziko Chadema - Wanabarikiwa ni wanadamu na sii chama.

Nitarudia kusema statement kama hizi hazifai na ningeomba sana na kuishauri hata serikali ule mtindo wa viongozi wetu wa kiserikali na kisiasa ktk kufungua mikutano wakisema Asalaam Aleikum, kisha - Bwana Asifiwe ni mwanzo wa kuleta Dini ktk siasa kwani mnajiweka ktk imani mbili za dini. Na hakika kisiasa inajenga nguvu mbili za mapambano ya kiimani ktk siasa hivyo vyama vyote vya kisiasa vinafungwa ktk imani hizi.

"Binafsi sielewi kwa nini kiongozi aseme Asalaam Aleikum neno la kiarabu ambalo tafsiri yake kwa kiswahili ni - Amani iwe juu yenu, kama halihusiani na dini fulani au Bwana asifiwe - huyu bwana nani?..

Jamani wengine tunaamini Mungu na matumizi yake yasitumiwe ovyo ovyo hata pale mnapotoa ahadi za uongo ama hamna hakika na myasemayo. Kuendesha hotuba za kisiasa kwa kuzitumia dini zetu ni makosa makubwa sana na inajenga Udini kwani kama utaongopa ili hali umeanza kwa kumsifia Mwenyezi Mungu -haya ni matusi makubwa wa waumini wa dini hiyo..."


Siasa zibakie siasa na maswala ya Mungu yapelekwe huko Makanisani na misikitini..

Sorry Mkuu sikuiona hii post nami nikawa najiandaa kumuweka sawa dada Regia. Anajisahau saana na kukibebesha lawama chama. Anahitaji kuwa mwangalifu saana kwenye kuandika na kuongea. Kama haiwezekani bora kuacha kabisa.

Hizo nia tafasiri zenu tu Wakuu. Hivi Mungu anakomea mpaka upi katika maisha ya Binadamu? Hivyo mnataka kutwambia kwamba Mungu ni miskitini na Makanisani tu basi. Kwa kuwafahamisha tu japo sitaki kuingia kwenye malumbano nanyi lakini kama kuna sehemu muhimu sana ambapo Binadam anamwitaji sana Mwenyezi Mungu au Allah ni katika uongozi na usimamizi wa watu au umma (hii sisi tunasema siasa kama labda mnakwazwa na neno siasa). Habari ya viongozi kusalimia kwa salamu zote za dini sioni tatizo na imekuwa desturi yetu watanzania miaka yote na pale viongozi wanaposalimia watu wote huitikia kwa pamoja kuonyesha umoja na upendo walio nao kwa pamoja miongoni mwao. Sijaona ilipoongelewa IMANI ya mtu hapa labda unipostie nione.

Hapa naona nyie ndo mna tatizo fulani, ".......lakini kwakuwa chama hiki kina mkono wa MUNGU,MUNGU alitumia njia zake za asili kuwang'amua waliokuwa na nia mbaya......" hapa sioni anaposema vyama vingine havina mkono wa Mungu au kwamba Mungu hawabariki watu. Kumbuka unaposema chama unasema watu, CHADEMA au CCM au CUF ni watu. Ukisema Mungu amebariki familia hii au ukoo huu au kabila hili au kazi zetu n.k. hao wote na watu. Au kwa hiyo kwako wewe mtu akikiri uwepo wa mkono wa Mungu au Msaada wa Mungu au Baraka za Mungu bas amemtumia Mungu ovyo. Mungu anatuamru tumkiri yeye kwanza na kumtegemea kwa kila jambo na kisha kumkiri tena kwa kumshukuru baada ya kutufanikisha. Kwa hiyo tuseme hata vikao vya Bunge waache kabisa kuwa wanafungua kwa kumtaja na kumwomba Mungu eti kwa sababu wanafanya kazi ya siasa (UONGOZI), ebu tujaribu kuwa tuna tafakari nini tunaongea sio kutuwekea post za kutuchafulia hali ya hewa. Wapi ambapo umeongelewa udini, kilichoogelewa ni uhusiano kati ya Mungu na uongozi wa mwanadamu, au huu ndo udini unaotaka kulazimisha au udini ni kumwongelea au kumzungumza Mungu ndo udini et!!

WanaCHADEMA ni WATANZANIA NA SIO DINI usichanganye hisia zako na mada.

EBU ONDOENI MITAZAMO YA KIDINI DINI HAPA, WATANZANIA WOTE TUNAHESHIMIANA PAMOJA NA DINI ZETU ZIPO PALE PALE.

Anayway mada ni:-

CHEERS!!! JOHN HECHE!!!
HONGERA SANA!!
 
Nimeandika katika ile thread ya awali (Iliyo tangulia hii ikiongelea majina na uchujaji wa majina) kuwa nataka kusikia kutoka kwa Habib Mchange baada ya Uchaguzi popote alipo tunahitaji kusikia anaongea nini!
 

Tarime ni kwetu,..
najua jinsi gani Heche ana nguvu kwa wananchi wa kawaida,..
ila najua pia hakua na ushawishi kwa viongozi wa chadema wilaya
(ambao hawa kumpitisha)

Laiti kama angeshiriki kwenye kampeni,naamini chadema ingeshinda achilia mbali yule kichaa wa cuf
kwanza hakua na kura nyingi kiasi hiko,...
Kususia kwake kampeni ndio sababu ya waitara kupungukiwa kura (ingawa ziliibwa pia)!!

Najua atatetewa kwa kushiriki kwenye team ya Dr.Slaa ila huo sio utetezi kwangu,
aliomba kwenda huko kwa maana ya kumkomoa Waitara!!!

Naposema simwamini najua nachosema sio kwa hoja za humu JF
 
Hongera sana mkuu,

Sikujui hata kwa sura, sijui ilikuwa na title gani lakini ujasiri wako unanipa kila sababu ya kuamini utakuwa mwiba kwa magamba na wale wanafiki ambao tumbo linawaongoza.

Tuendeleze mapambano.

Bwana selous sijakuelewa, ulianza kwa kusema Slaa ni mnafiki sasa unamsifia mwenyekiti mteule, nafikiri ungetujuza unafiki wa Slaa
 
Nimeandika katika ile thread ya awali (Iliyo tangulia hii ikiongelea majina na uchujaji wa majina) kuwa nataka kusikia kutoka kwa Habib Mchange baada ya Uchaguzi popote alipo tunahitaji kusikia anaongea nini!

Hiyo nayo ni point,lakin assume Habib ni mwana JF,
afu akaingia kwenye thread hii akakakutana na post hii hapa!
Unadhani itamfanya aseme nini?


 
Ni rahisi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko heche kuwa mbunge wa Tarime. Jimbo la Tarime ni la CDM kupoteza na litapotea kama Heche na Waitara watarudishwa, mtu yeyote anaweza kusinda isipokuwa, Heche, Waitara, Chambili na Current waste of space CCM MP
 

Mhhhh,ko bora nikagombee mimi eh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…