Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa John Heche, anawatakia Watanzania wote heri ya mwaka mpya wa 2026.
Tunapoingia mwaka mpya, tunatambua maumivu, hofu na uchovu uliowagusa wananchi wengi. Tunawatakia uponyaji wa mioyo, faraja kwa waliopoteza wapendwa wao, na matumaini mapya kwa kila kijana, mkulima, mfanyabiashara na familia ya Kitanzania. Kama Maandiko Matakatifu yanavyotukumbusha:
"Bwana yu karibu na waliovunjika mioyo, huokoa waliopondeka roho." (Zaburi 34:18)
Mwaka 2026 uwe mwanzo wa kuponya Taifa kwa msingi wa ukweli na haki. Taifa haliwezi kuponywa kwa maneno matamu bila kukiri makosa. Amani ya kweli haiwezi kujengwa juu ya uongo, hofu au kuficha ukweli. Maridhiano ya kweli huanza pale mamlaka inapokiri ukweli, kuwajibika, na kurejesha haki kwa waliodhulumiwa. Kama Qur'ani Tukufu inavyotuonya:
"Hakika Mwenyezi Mungu hawabadilishi ya watu mpaka wabadilishe yaliyo ndani ya nafsi zao." (Qur'an 13:11)
Mheshimiwa John Heche atatoa Hotuba ya Kufungua Mwaka tarehe 3 Januari 2026, hotuba itakayobeba masuala ya msingi ya Taifa, msimamo wa ukweli, na wito wa mabadiliko ya haki kama nguzo ya amani ya kudumu.
Mwaka Mpya, Taifa Jipya la Haki, Ukweli na Ujasiri wa Kubadilika.