Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
“Kuna watu wengi jana na leo wamenipigia kuhusu yanayoendelea kwenye teuzi za CCM na wengi wanasema kutokana na vurugu, kuumizana, migogoro na chuki ambazo ziko ndani ya CCM kwamba hii ni fursa kwetu kupata wabunge wengi kama CHADEMA,” amesema John Heche Makamu mwenyekiti Chadema.
Hata hivyo, Heche amesisitiza kuwa chama chake hakina mpango wa kufaidika na migawanyiko ya CCM.
“Sisi hatutaki kushinda uchaguzi kwa sababu CCM wamegombana. Hatutaki kuwa na wabunge bungeni kwa sababu wabunge wa CCM wameumizana au kwa chuki zao wakakimbilia kwetu. Tunataka kushinda uchaguzi kwa haki,” ameongeza.
Heche pia ameeleza kuwa CCM haishindi kwa sera bora wala wagombea imara, bali kwa msaada wa mifumo mibovu ya uchaguzi inayolindwa na dola.