John Heche: Tuna Tanzanite Peke yetu Duniani ila wataalamu wa kukata Tanzanite ni Waindia sababu watoto wetu wanafundishwa panzi ana miguu mingapi

John Heche: Tuna Tanzanite Peke yetu Duniani ila wataalamu wa kukata Tanzanite ni Waindia sababu watoto wetu wanafundishwa panzi ana miguu mingapi

uza shamba peleka watoto SOUTH AFRICA wakachukue shule acha kulalama hakuna mtu atakupa ulaji wa bure.Ingekuwa hao wahindi wamepelekwa na serikali ungefaa kulalamika ila wenzetu wanaona mbali tofauti na sisi mijitu mweusi.

Matajiri kibao wamigodini wanasomesha watoto wao vitu vya ajabu mara sijui udaktari,unesi ambazo ni kozi za walalahoi( hili ntalieleza siku nyingine),,,, badala ya kuangalia vitu vipya vyenye fursa.

Ukiangalia ngozi nyeusi ni hivi juzijuzi watu ndo wameshtuka kuwa kwenda hadi form six ni upotevu wa muda na kuna nchi zinatoa technical courses kama urubani hata kwa form four leaver wakati kwa Tanzania watu wengi walikuwa wanajua mpaka mtu asongoke apitie mchepuo wa PGM.

Waafrica badala ya kufuga vitambi na kununua magari ya mamilioni 500 pale tunapozifuma pesa ni mda muafaka sasa tuanze kujiwekeza kwenye teknologia na fani ambazo ni adimu humu nchini....tofauti na hapo tutaendelea kuwa walalamishi mpaka mwisho wa dunia.
 
Wazungu wanafundisha watoto wao fani za ufundi wakiwa wadofo. Huku kwetu Unamfundisha mtoto bindamu wa kwanza alikua ni nyani alafu tena anachora nyani na stage zake za kubadilika mpaka anakua mtu huku huku mtaani anaona ndugu zake nyani hawabadiliki kua binadamu mbaya zaidi akibalehe na akilala na wakiume au wakike anajikuta anabeba mimba.
 
Back
Top Bottom