Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
John Heche akitoa salamu za Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu, akiwa Tarime amesema yeye pamoja na Lissu wapo tayari kufa kwa ajili ya kulinda msimamo wa Chama chao ilikutetea maslai ya Wananchi wa hali ya chini.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Lissu ametoa maelekezo na huo ndio utakuwa msimamo wetu, ambao mimi na Lissu tupo tayari kufa kwaajili ya kulinda msimamo wa Chama na tutawaongoza Wananchi, tunatambua ni watu tulio zaliwa na ipo siku moja tutaondoka duniani, tunataka tuondoke katika hali ambayo tutaacha nchi yetu ikiwa salama na madini yake na Rasilimali zake zinatumika kwa ajili ya watu wengine woto na sio kikundi cha watu wachache wanaojinufaisha, huku wengine mkiendelea kufa masikini na hamuwezi hata kula chakula"
"Tuna matatizo makubwa kwenye nchi hii, watu wetu hawana chakula wanalala njaa kwenye nchi tajiri, matibabu hakuna (tumemuona mama moja hapa anazungumza kwamba asaidiwe kutibu mtoto wake) sisi tunataka tujenge nchi ambayo wewe mwananchi utakuwa na uwezo wa kujisimamia utibiwe kama John Heche anavyoweza kwenda kutibiwa mahali popote kwasababu utakuwa na uchumi.
"Tunataka tujenge nchi ambayo wewe utalala kwenye nyumba nzuri kama ambayo analala mtoto wa Wasira kwasababu nchi hii ina uwezo huo. Tunataka kujenga nchi ambayo utatibiwa kwenye hospitali ambayo anatibiwa mtoto wa Samia Suluhu Hassan, hatutaki nchi yenye matabaka, tunataka nchi ambayo rasilimali zetu zinatumika kwaajili yetu sote"