John Heche usiwaondoe watanzania kwenye reli

John Heche usiwaondoe watanzania kwenye reli

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
John Heche ni moja ya wanasiasa wanaoheshimika sana kwa misimamo yake na kupenda kusema ukweli hilo halina ubishi, kwa sasa wananchi wanayo maeneo wanayolalamikia sana ambayo wanahitaji sauti za pamoja ili kuyatatua.

Suala la Umeme linavyoathiri biashara za wananchi, ufisadi ulioibuliwa bungeni hivi majuzi na mikataba iliyosababisha ndege yetu kudakwa ulaya, kupanda kwa gharama za maisha mfumko wa bei, viongozi waliopewa dhamana na Mh Rais kuwadharau wananchi, Bunge kuruhusu mijadala ya kuwabagua na kuwadharau wenye Phd za heshima..

Tuitegemea Heche angepita kwenye maeneo hayo badala yake anazungumzia Mafao ya wabunge waliolipwa mwaka 2020 na yeye akiwa mmoja wapo wa waliolipwa nadhani huo ni mkakati wa kuwahamisha wananchi kwenye ajenda kuu zilizopo na kuwarudisha kujadili mambo ambayo sio kipaumbele kwa sasa.

Kama alitaka kuzungumzia hoja ya wastaafu na kikotoo angebaki na hoja hiyo bila kuchanganya mambo ya wabunge.
 
Back
Top Bottom