John Heche: Vijana acheni uoga, tumieni nguvu zenu kudai mabadiliko

John Heche: Vijana acheni uoga, tumieni nguvu zenu kudai mabadiliko

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, amesema vijana ni nguvu kubwa katika jamii na wana uwezo wa kusababisha mabadiliko nchini.

Heche ameyasema hayo akizungumza na vijana, akiwahimiza kutambua nguvu waliyonayo na kuitumia katika kushiriki katika masuala yanayohusu mustakabali wa nchi.

"Nataka niwaambie nyie ni nguvu tena nguvu kubwa kuliko nguvu nyingine yoyote kwenye nchi hii. Nyie ni nguvu inayoweza kusababisha mabadiliko katika nchi hii"."

Lazima mfike sehemu muweke uoga pembeni na yeye ajue watanzania wamekataa kuogopa. Akilijua hilo atajirekebisha"."Vijana tulion nao kati ya umri wa miaka 15 mpaka 35 ni 34%. Nyie ni wengi kuliko kundi lingine lolote katika nchi hii"."

Inakuwaje mtu aliyeko Israel jangwani analima kwa uhakika kuliko mtu aliyeko Tanzania eneo lenye ziwa Victoria... na ziwa Tanganyika?"."Kijana ana elimu, kijana ana nguvu, kijana ana simu, kijana ana ubunifu, kijana ana hamu ya kufanya kazi. Lakini huyu kijana hana mtaji".

 
Kumbe jukwaa la siasa,

Bado nina machozi na maumivu kwa ajili ya rafiki yangu timu yake simba imefungwa leo
 
Back
Top Bottom