PreGE2025 John Heche: Wanaoondoka CHADEMA ni matokeo ya mabadiliko ya uongozi, si ubaguzi

PreGE2025 John Heche: Wanaoondoka CHADEMA ni matokeo ya mabadiliko ya uongozi, si ubaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara, John Heche amesema ndani ya chama hicho hakuna ubaguzi bali ni mabadiliko ya kawaida ya viongozi.

Heche amesema hayo leo Alhamisi, Mei 8, 2025 mkoani Kagera katika mikutano ya operesheni ya No reforms, no election 'bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Heche ametoa kauli hiyo siku moja baada ya waliokuwa wajumbe wa sekretarieti katika utawala wa mwenyekiti aliyepita Freeman Mbowe, kutangaza kukihama chama hicho wakidai hakifuati katiba yao na kuna ubaguzi.

Walioondoka ni waliokuwa naibu katibu mkuu, Benson Kigaila (Bara), Salumu Mwalimu (Zanzibar), Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano, John Mrema, katibu wa sekretarieti, Julius Mwita na Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Catherine Ruge.
View attachment 3328122
huenda ni malofa wasio na maono wala malengo ndio pekee wanaweza kubaki au kusalia kwenye chama ambacho hakishiriki chaguzi wala kua na malengo ya kushika dola 🐒
 
Heche. Kama wameondoka kwa amani basi waacheni waende. Kwanza ilitakiwa kuwashukuru kwa sehemu yao waliyoifanya.

Kila binadamu anauhuru binafsi.

Sioni sababu ya kuendelea kupigana vijembe mkuu.
Mke ni mke unamhudumia kila kitu mwisho wa siku anakuacha na matusi juu et unakibamia.
Unajuuuliza ina maana alifata kibamia au kujenga familia?
 
sidhani kama ni vijembe, wakati mwingine uongo inabidi ujibiwe ili ukweli ujulikane, wakikaa kimya kuna watu wataamini wanaonewa
 
Asiye na akili atawasikiliza, mwenye kufiri na kuchanganua mambo atakataa maneno yako
Why? Mlivyofanya kampeni za kumtukana, kumdhihaki, kumsingizia, kumbagaza Mbowe sisis tulijua mwisho wa uropokaji huo utakuwa huu!
It was as if you were waging a war with Mbowe!
Lakini mambo field yapo tofauti na unacho kisema, Chadema inakua zaidi kuliko mwanzoni, yaani is like imerudi ile Chadema ya enzi zile za Dr. Slaa akiwa katibu mkuu! Tokea awamu ya 5 na ya 6 ni kama Chadema ilidumaa sana, imefufuka upya. Hi ni kwa mujibu wa ninayo yaona mtaani sasa hvi though mimi sio mwana chama wao
 
Heche. Kama wameondoka kwa amani basi waacheni waende. Kwanza ilitakiwa kuwashukuru kwa sehemu yao waliyoifanya.

Kila binadamu anauhuru binafsi.
Mkuu, unamshukuruje wakati amekutuhumu vikali kiasi kile?

Ama mwenzetu hufuatilii?

NB: Jambo la msingi, haya mambo yasiwatoe kwenye reli.

Nadhani wapinzani wao wanafurahia sana mpasuko huu; wasitumie muda mwingine kuhangaika nao.
 
Heche. Kama wameondoka kwa amani basi waacheni waende. Kwanza ilitakiwa kuwashukuru kwa sehemu yao waliyoifanya.

Kila binadamu anauhuru binafsi.

Sioni sababu ya kuendelea kupigana vijembe mkuu.
Mke ni mke unamhudumia kila kitu mwisho wa siku anakuacha na matusi juu et unakibamia.
Unajuuuliza ina maana alifata kibamia au kujenga familia?
Heche hapigi vijembe bali anaweka records sawasawa kwani wale Njaa 55 jana walisema uongo mwingi sasa usipokanushwa itaaminika hivyo.
 
Lakini mambo field yapo tofauti na unacho kisema, Chadema inakua zaidi kuliko mwanzoni, yaani is like imerudi ile Chadema ya enzi zile za Dr. Slaa akiwa katibu mkuu! Tokea awamu ya 5 na ya 6 ni kama Chadema ilidumaa sana, imefufuka upya. Hi ni kwa mujibu wa ninayo yaona mtaani sasa hvi though mimi sio mwana chama wao
Good observation
 
Hao jamaa ni wachumia tumbo ndiyo maana huyo Mrema kwenye moja ya press alisema tusiposhiriki tutakosa ruzuku,hao wanasaka fursa tu siyo kupigania haki.
Ruzuku kwani siyo moja ya malengo ya chama?

Au mie ndiye sielewi vizuri?

Au tubaki na Tone-tone! 🙂
 
huenda ni malofa wasio na maono wala malengo ndio pekee wanaweza kubaki au kusalia kwenye chama ambacho hakishiriki chaguzi wala kua na malengo ya kushika dola 🐒
Anayeshiriki uchaguzi kwa sheria zilizopo ni mjinga wa mwisho.
 
Kweli huelewi. Lengo la chama cha siasa ni kushika Dola ili kiweze kutekeleza sera zake
Ndiyo maana G55 wanauliza mtaishikaje dola wakati uchaguzi mnaupiga chini?

^Tutashinda uchaguzi mkuu kwa Tume hii hii.^~ TAL.
 
Anayeshiriki uchaguzi kwa sheria zilizopo ni mjinga wa mwisho.
ni muhimu zaid siku ya uchaguzi matakatifu malofa machache na masusaji chaguzi yakakaa nyumbani ili hatimae mamilioni ya wananchi na waTanzania wote kwa ujumla washiriki uchaguzi Mkuu kwa Amani 🐒
 
huenda ni malofa wasio na maono wala malengo ndio pekee wanaweza kubaki au kusalia kwenye chama ambacho hakishiriki chaguzi wala kua na malengo ya kushika dola 🐒
Mkuu walishiriki uchaguzi 2019, 2020 na 2024, walienguliwa una uhakika gani kuwa uchaguzi huu hayatafanyika yaliyofanyika Huko nyuma
 
Back
Top Bottom