John John Mnyika mmea uliokosa Ardhi yenye rutuba

John John Mnyika mmea uliokosa Ardhi yenye rutuba

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,830
Reaction score
972
Wanajamvi,

Tunao wanasiasa ambao ukiwaangalia unaona kitu ndani yao. Binafsi, namuona John Mnyika Kama mwanasiasa wa upinzani asie na mawaa. I stand to be corrected.

Hatahivyo, Mnyika kwasasa hayuko sehemu sahihi. Pamoja na kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA bado kwa jicho la ndani namuona John akiwa amavaa koti linalompwaya. Ameduwaa na kunyongea mno. John bado anajitafuta, John hayuko sawa.

Hata kwenye mpira wa miguu, mchezaji mzuri anashamirishwa na uwepo wa wachezaji wengine wazuri. Combination ni kitu muhimu sana. Mnyika aliendana sana na Balozi Dkt. Slaa na sio kitu cha kushangaza kuwa tangu kuondoka kwa Balozi Dkt. Slaa kwenye chama hicho, John has never been the same.

John, wajina wako anafanya kile mlisimamia na Balozi Dkt Slaa, tafadhali njoo CCM, njoo uwatumikie Watanzania.

Mimi sina uwezo wa kuteua hata Mwalimu wa darasa ila nina uhakika ukija huku ng'ambo ya pili, Rais Magufuli atakuteua kwenye nafasi ambayo utawatumikia Watanzania kwa vizuri zaidi.

John, hima toka huko, ukatengwe nao. Njoo huku kwenye nuru ili uangaze. Wewe ni mmea mzuri ila upo kwenye udongo usio na rutuba. Maji unayomwagiwa, hayasaidii.

Amani Msumari
Tanga
 
Hivi babu yako akifa maisha yanasimama?
Slaa ni sawa na mfu kisiasa
 
John, wajina wako anafanya kile mlisimamia na balozi Dkt Slaa, tafadhali njoo CCM, njoo uwatumikie Watanzania.
Mkuu siyo bure utakuwa umetumwa kuja kupima kina cha maji. Yawezekana mradi wa kununua na kutelekeza wa Polepole umefufuliwa tena.
 
Back
Top Bottom