Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JOHN LIMO WA TPC NA CHAKI WA COSMOPOLITAN
Picha ya kwanza ni ya John Limo na picha ya pili ni ya Chaki mbae katika miaka ya 1960 alikuwa golikipa wa Cosmopolitan na Timu ya Taifa na aliacha kucheza golini na kuja kucheza mbele kwa umahiri mkubwa sana.
Chaki ni huyo katika picha ya mwisho.
Nilikutana na Chaki New York mwaka wa 2011 na picha hii tulipiga msikiti wa Ijumaa bada ya kusali pamoja hapo.
John Limo tulipokutana Tanga katika miaka ya mwazoni 2000 nilimuuliza kama anazo picha zake wakati akisakata kandanda miaka ya 1960 hadi 1970 enzi za Gossage Cup akaniambia kuwa hakuwanazo.
Niliingia Maktaba a nikamtengenezea kijialbam kidogo cha picha zake na alifurahi sana.
Rafiki yangu Prof. Mohamed Khalil Timamy alipojua kuwa mimi kama yeye nilikulia na kusoma Moshi shule ya msingi na kuwa niliishi sana Tanga aliniuliza ikiwa namjua John Limo.
Prof. Timamy akaniambia kuwa baba yake akifanya kazi TPC ingawa alikuwa kutoka Kenya wakati ule John Limo yuko hapo akicheza mpira pamoja na wachezaji wakubwa wa wakati ule kama Mbwana Abushiri, Hemed Seif, Shariff Salim na Sembwana kwa kuwataja wachache.
Prof. Timamy alikuja Tanzania na nilikwenda kumpokea Tanga na akaniomba nimkutanishe na John Limo.
Prof. Timamy anasema hajapatapo kuona mtu anacheza mpira maridadi kama John Limo.
Akaniongezea kitu kingine.
Kanambia wakati yeye mtoto mdogo anachokumbuka kwa John Limo pale Arusha Chini ni kuwa kila alipokutananae alikuwa na tabasamu kwake.
John Limo alifurahi sana kumuona Prof. Timamy sasa si mtoto mdogo bali mtu mzima.