John Malecela: Tuunge mkono juhudi za Rais Magufuli kwa maendeleo endelevu

John Malecela: Tuunge mkono juhudi za Rais Magufuli kwa maendeleo endelevu

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
305
Reaction score
728
Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, John Samuel Malecela amewataka watanzania kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika juhudi za kujenga uchumi imara na endelevu.

Mzee Malecela ameyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalum na Maafisa wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.

“Tumsaidie na kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri anayofanya ya kujenga uchumi usiyoyumbishwa ili Tanzania izidi kupiga hatua kubwa kimaendeleo”, alisema Malecela.

Alitaja sifa za Rais Magufuli kuwa ni kiongozi bora, mzalendo, mpinga rushwa na ufisadi, mwenye maono na mwenye kujali wananchi sambamba na kusimamia katiba na sheria za nchi.

Katika kuudhimisha miaka 59 ya Uhuru na 58 ya Jamhuri, Mzee Malecela alitoa tathmini yake ya kimaendeleo na kusema kuwa wakati Tanganyika inapata uhuru uchumi wa nchi ulikuwa chini sana ukitegemea kuuza nje mazao ghafi kama vile kahawa, pamba, chai, mkonge, korosho na pareto. Kwa sasa uchumi umekua kwani hata mazao yanayosafirishwa au kuuzwa nje yanakuwa yamechakatwa hivyo kuyaongezea thamani.

Aidha, alieleza kuwa nchi imepiga hatua kwa kuboresha miundombinu ya barabara, reli na umeme pamoja na kuboresha elimu na huduma za afya.

“Wakati tunapata uhuru tulikuwa na madaktari watanzania watano tu ambao ni Dkt. Kyaruzi, Mtawali, Mwaisela, Mwanjisi na Dkt. Akimu kwa sasa tuna madaktari maelefu kwa maelefu, haya ni maendeleo makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 59 ya uhuru” alisema Malecela.

Mzee Malecela aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kukuza uchumi na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati na kuongeza kuwa watanzania inabidi wafanye kazi kwa bidii na kushiriki shughuli zote za maendeleo.

1607346645041.png
 
Tumuunge mkono Rais JPM sio kwa kumsifu pekee isipokuwa kum-stretch ili afanye kazi na Watanzania ili kuikuza private sector.

Inasikitisha kila mwaka tunatoa takwimu za deficit ya mafuta ya kula ni zaidi ya tani laki 3,
deficit ya sukari
deficit ya mbolea na madawa ya kilimo na madawa ya mifugo
deficit ya saruji
deficit ya madawa ya binadamu
deficit ya maziwa ng'ombe
deficit ya nyama... the list goes on;

Wakati Mhe. Rais JPM anavunja Bunge la JMT nilitoa ushauri hapa chini.


Mpaka sasa bado naàmini ushauri wangu uko relevant na tutafute audience ili kumwomba Mhe. Rais tuone namna gani tutatumia strategic position ya Tanzania na assets zetu kujenga viwanda ili kuziba hizo deficits na kuzalisha surplus.

In the course tutazalisha ajira na kupanua tax base na kupunguza imports.

Kuna mambo ambayo tukifanya kimkakati, soko la ndani ni collateral kutuhakikishia mauzo mara tukizalisha ndani.
Kwenye diplomasia ya kiuchumi, sio rahisi Foreign investor akaja kuwekeza kwenye project ambayo ipo nchini kwake na imeajiri kwao ilo kuongeza mauzo ya nchi yao Tz ikiwa moja ya soko.

Hapa ndipo lazima tukae kitako na Rais wetu ili kumpa insights nini tufanye ili kuzifanya hizo deficits kama "potential assets" na lazima kuzitumia sasa.

Hii biashara ya kum-stretch Mhe. Rais tufanye asb na mapema kabla ya 2024 wakati michakato ya chaguzi za serikali za mitaa na baadae 2025 uchaguzi mkuu.

Wasalaam

Freddie
 
Back
Top Bottom