Kamanda Asiyechoka
JF-Expert Member
- Sep 13, 2020
- 3,366
- 5,209
Kama msimamizi wa DAR MPYA MEDIA LIMITED (Darmpya Blog&Tv Online) nasisitiza habari iliyoandikwa kumhusu N/W Katambi kuhusu kauli yake kwa vijana wa Tanzania ni maneno yake na hatuwezi kuomba radhi kwa sababu hatujakosea
Ushauri: asipoteze muda kutishia Media.
John Marwa
CEO
========
UPDATE: Disemba 20, 2025
Mmiliki wa blogu ya Darmpya.com alikuwa John Marwa
Mnamo Juni 2018, blogu hiyo ilisitisha utoaji wa huduma zake kutokana na agizo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) lilitaka blogu zote kulipa gharama za leseni ili kuendelea na shughuli zao. John Marwa alieleza kuwa gharama hizo za leseni ndizo zilizowashinda na kusababisha kufungwa kwa blogu hiyo.

- Kufungiwa na Kubadili Jina: Mnamo Julai 2022, TCRA ilikipiga marufuku kituo hicho kuchapisha maudhui mtandaoni, ikidai kushindwa kufanya upya leseni yake kama inavyotakiwa na kanuni za maudhui mtandaoni. Kutokana na hali hiyo, DarMpya ilibadili jina na kuwa ZamaMpya, baadaye, Marwa alibadili mwelekeo na kuanzisha Jambo Media, ambayo inajulikana kama "Jambo Online TV" kwa sasa
- Uamuzi wa Kamati: Kumekuwa mara kwa mara na malalamiko yanayowasilishwa kwa Kamati ya Maudhui ya TCRA dhidi ya DarMpya, ZamaMpya na sasa Jambo Online TV. Uongozi wake mara nyingi umekuwa ukiitwa mbele ya kamati ili kutoa maelezo ya utetezi wao dhidi ya tuhuma hizo. Mara kadhaa, wamepigwa faini au kupewa maonyo (kwa mujibu wa John Marwa)
- Utaratibu wa Leseni: TCRA inatoa leseni mbalimbali za huduma za mawasiliano na utangazaji. Mchakato wa kupata leseni unafanywa kidijitali kupitia mfumo wa Tanzanite Portal. Kutoa huduma za mawasiliano au utangazaji bila leseni halali kutoka TCRA ni kosa kisheria nchini Tanzania