Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameeleza kuwa chama hicho kimejipanga vema kukabiliana na kile alichokieleza kama dhamira ovu ya kuhamisha orodha haramu ya wapiga kura wasiokuwa halisi. Mnyika amedai kuwa mbinu hii inatekelezwa kupitia mtandao wa mabalozi, ambao wamewekewa kikanuni kwamba waandikishaji ni watumishi wa umma.
Ameonya kuwa baadhi ya watumishi wa umma wasio waadilifu wanaweza kushawishiwa na mbinu hizi haramu kwa lengo la kuwahamisha wapiga kura wasio halali na kuwaingiza katika daftari la wapiga kura.
Kwa kukabiliana na hali hiyo, Mnyika amesema kuwa CHADEMA itakuwa na mawakala wao katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya kuhakikisha uangalizi wa karibu na kuhakikisha haki inatendeka.
• Mnyika: Tukitaka kuongeza idadi ya wapiga kura imani katika mifumo ya uchaguzi iongezeke
• Mnyika aitupia lawama TAMISEMI, adai ni Mpango wa CCM na TAMISEMI kutohamasisha Uandikishaji wa Wapiga Kura
• Vyama vya siasa hamasisheni wapiga kura wenu wajitokeze kujiandikisha au kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura.
• Jaji Mwambegele: Mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika Vituo vya Kuandikisha Wapiga Kura