John Mnyika aitwa Polisi kwa uchunguzi mauaji ya Ally Mohamed Kibao

John Mnyika aitwa Polisi kwa uchunguzi mauaji ya Ally Mohamed Kibao

Sio mbaya, ila ubaya ni kua hizi propaganda hushia hewani mwisho wa siku hamna anaetuhumiwa kwa hayo mauaji..

Inaumaga sana ile kitu unajua ni fulani kafanya na huana kitu unaweza mfanya kwa wakati huo.
Ndio hii sasa.
 
Bila mnyika kuitwa kuhojiwa ilikua haijaonekana kama uchunguzi tayari umeanza sasa ndo naamini uchunguzi umeanza maana yeye ndo alikua first responder kuna kitu atasaidia na itajulikana pakuanzia hatuwezi kuishi kwenye nchi watu wanatoana roho kama wanachinja kuku.
Uchunguzi juu ya kupotea Ben Saanane November 2016 umefikia wapi?

Uchunguzi kwa waliompiga Lissu risasi 32 , 2017 umefikia wapi?

Uchunguzi wa waliomteka Mohamed Dewji 2018 umefikia wapi?

Uchunguzi wa kifo cha mfanyabiashara wa madini Mtwara 2022 umefikia wapi?
 
Bila mnyika kuitwa kuhojiwa ilikua haijaonekana kama uchunguzi tayari umeanza sasa ndo naamini uchunguzi umeanza maana yeye ndo alikua first responder kuna kitu atasaidia na itajulikana pakuanzia hatuwezi kuishi kwenye nchi watu wanatoana roho kama wanachinja kuku.
Watuwanatoana roho au Serikali inawatoa roho raia?
 
Sijui ni mihemko au upeo wetu ni mdogo. Tujue kutofautisha kushikiliwa na Polisi kwa kosa la mauaji na kuitwa kutoa taarifa saidizi katika kosa la mauaji. Naona wengi tunatukana kwa kushindwa kutofautisha hili vitu viwili.
 
Asikilize wito na baada yakutoka Kwenye wito atuambie wanalitaka kujua nn kwakee hao police CCM ..

Ila awe makini maana anaweza kwenda kusikiliza wito kumbe ndio hatutamuonaa tenaa..
Nahisi kama anaenda kupewa yeye kesi ya mauaji
 
Jeshi la Polisi Tanzania limemuita Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika kufika katika Ofisi ya Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na mauaji ya Ally Mohamed Kibao.

Kulingana na barua rasmi iliyotolewa tarehe 16 Septemba 2024, na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni wito huo umetolewa kwa lengo la kusaidia uchunguzi wa mauaji hayo.
Barua hiyo yenye kichwa cha habari "Wito wa Kufika Polisi," iliyosainiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kinondoni, SSP Davis J. Msangi, inamtaka Mnyika kufika katika ofisi hiyo tarehe 18 Septemba 2024 saa nne asubuhi bila kukosa.

"Ofisi hii inafanya upelelezi kuhusiana na jalada tajwa hapo juu. Ili kukamilisha uchunguzi, nimelazimika kukuita kwa ajili ya mahojiano kwani kuna masuala ambayo wewe unayafahamu yanayoweza kusaidia katika upelelezi wa shauri hili," inaeleza barua hiyo.

Soma pia: Mnyika: Mzee Kibao alitekwa na Kuuawa akiwa ametoka kuendesha Mafunzo ya Maandalizi ya Uchaguzi Serikali za Mitaa. Tutaendeleza Majukumu aliyoyaacha!

Wito huo unatokana na hatua ya uchunguzi unaofanywa kuhusu kifo cha Kibao, ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye alitekwa kisha kuuawa Septemba 2024. Tukio hilo limekuwa gumzo nchini, likiwakera wanasiasa, wanaharakati, na wananchi kwa ujumla.
Mnyika ameitwa chini ya kifungu cha 10(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura ya 20 na kifungu cha 32 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi, sura ya 322.

Soma zaidi:

==> Rais Samia: Nia yako njema ya uchunguzi mauaji ya kibao lakini ninashauri iundwe tume huru kuchunguza na sio Polisi
==> Familia yaomba uchunguzi wa haraka Kifo cha Ali Kibao, Waziri Masauni akabidhi Tsh. 5m ya Rambirambi
==> Freeman Mbowe: Iundwe Tume ya kijaji kuchunguza kifo cha Ali Kibao, Polisi hawawezi kujichunguza

View: https://x.com/fatma_karume/status/1836003251243581886?t=JZm3SLc7B_-O_XuXWWn8ng&s=19
 
YAPO YA KUSHANGAZA KUPITA KIASI MFANO YULE ALIYETEKWA AKAMTAMBUA MTEKAJI WAKE NA KUTOKUWEPO KWA HATUA ZOZOTE ZINAZOENDELEA, INANISTAAJABISHA KWELI KWELI.
 
Back
Top Bottom