John Mnyika amaliza utata pesa za Join the Chain. Ataja kiasi kilichopatikana na kazi zilizofanya. Asema wajumbe wote wa kamati kuu walikuwa wanajua

John Mnyika amaliza utata pesa za Join the Chain. Ataja kiasi kilichopatikana na kazi zilizofanya. Asema wajumbe wote wa kamati kuu walikuwa wanajua

Ndugu zangu Watanzania,

Siweki neno lolote lile zaidi ya kuweka taarifa ya John Mnyika katibu Mkuu wa CHADEMA.👎

#JoinTheChain ilikuwa ni kampeni Maalum iliyofanywa na CHADEMA kukusanya fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Chama kati ya mwezi Februari mpaka Mei 2022.

Kwa wakati huo kipaumbele cha kwanza ilikuwa ni kugharamia Mkutano wa Baraza Kuu 2022 ambalo pamoja na agenda nyingine lilisikiliza rufaa za #Wasaliti19 waliofukuzwa uanachama. Baada ya hapo fedha za ziada zingetumika kwenye operesheni za Chama ikiwemo za madai ya #KatibaMpya .

Fedha ambazo Makao Makuu tulipokea kupitia akaunti ya benki na nambari za simu tulizotangaza hapo chini wakati huo zilikuwa shilingi milioni 114. Fedha hizo ziligharamia sehemu ya gharama za Mkutano wa Baraza Kuu la Chama la Mei 2022.

Soma Pia: Ezekiel Wenje: Kuhusu zilipoenda pesa za Join The Chain muulizeni Godbless Lema. Yeye ndo alikuwa Mwenyekiti!

Aidha, pamoja na fedha taslimu kampeni hiyo iliunganishwa pia na ulipaji wa ada na kadi kidigitali ambapo mapato yote kwa ujumla yalikuwa shilingi milioni 371.

Taarifa ya kiwango cha makusanyo na matumizi ilitolewa kwa Kamati Kuu katika vikao vitatu tofauti kwa nyakati mbalimbali hivyo hakuna mjumbe wa Kamati Kuu anayepaswa kusema hafahamu. Majibu sahihi yanapaswa kuwa ama mjumbe hana mamlaka ya kusemea masuala ya fedha au amesahau takwimu.

Nimelazimika kuandika kuhusu suala hili kwa kuwa naona limejirudia rudia mitandaoni na kwenye vyombo vya habari lakini mara zote ambazo Katibu Mkuu nimefanya press conferences halijawahi kuulizwa. Mahesabu ya mwaka husika wa fedha ikiwemo yaliyohusu mapato na matumizi kutoka kampeni #JoinTheChain yalikaguliwa na Mkaguzi wa Mahesabu (CAG) na Chama kikapata hati safi. #StrongerTogether #mkutanomkuuchadema2025

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili
We mwanasm,waaachie chendema mambo Yao!
 
Tuna imani na Rais Samia na tunaweza kubadilisha hata katiba ili atawale mpaka achoke Mwenyewe.
Imani unayo wewe na familia yako na labda aitawale familia yako hadi achoke ila sio Tanganyika wewe kunguni wa bibi wa Unguja.
 
Imani unayo wewe na familia yako na labda aitawale familia yako hadi achoke ila sio Tanganyika wewe kunguni wa bibi wa Unguja.
Tutabadilisha katiba na hutakiwa na chochote kile cha kutufanya wala kutuzuia.
 
Mchanganuo wanaujua wajumbe wa kamati kuu.hapo ametoa kwa ufupi kuonyesha uadilifu wa Mwamba ambaye aliongoza zoezi hilo. Ndio maana wajumbe wamejiandaa kumpigia kura za ndio Mwamba na Jabali la siasa za upinzani hapa Nchini Mheshimiwa Freeman Mbowe kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima
Hapo sasa wewe utakuwa unatofautiana na wenje maana yeye ndio alisema kuwa pesa hizo aulizwe lema
 
Back
Top Bottom