John Mnyika ana elimu gani? Uwezo wake wakujibu hoja unatokana na mafunzo ya maprofesa wa bongo au akili za kuzaliwa?

John Mnyika, namkubali sanaa huyu baba.
[emoji122][emoji122]
Uzimzeeshe bwana,Mnyika ni baba lakini kwa vitoto vya 15yrs kushuka chini.Kwako wewe Mnyika ni Kaka [emoji3][emoji3]
 
Unamfahamu Mzee Mangula wewe? Hivi unamjua Kinana! Kwa Slaa sawa
 
Mfano mzuri ni pale alipokiri kwamba yeye binafsi alikataa kumpokea Lowasa,
Ni kweli JJ tulikuwa naye kwenye kundi la wakataaji mpaka dakika ya mwisho. John ni miongoni mwa walioamua kuunga mkono juhudi za mbowe, sisi wengine tukagoma kugeuka mawe, tukajiondoa! Hata lisu alikuwa kundi letu mpaka alipokatiwa cha juu ndo akaamua kutusaliti. Mungu anamuona.
 
Mliojiondoa ni wasaliti period, kwenye kujenga jambo suluhu sio kujiondoa bali nikupima fact , na kukubali mawazo ya wengi na kusonga mbele, stupid
 
Baada ya kusema hayo alipaswa aulizwe kuwa kughushi ni kosa la jinai, baada ya yeye kugundua hao wabunge 19 wameingia Bungeni kwa barua ya kughushi alipaswa afanye nini?. Ofisi yoyote haipaswi kuonyesha nyaraka yoyote ya kiofisi kwa yeyote, hao NEC wamuonyeshe Mnyika barua ya kutoka Chadema kama nani?.

Chadema na Mnyika walichopaswa kufanya baada ya kugundua kuna forgery
1. Kuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike.
2. Uchaguzi ungethibitisha jinai ya forgery
3. Baada ya jinai ya forgery kuthitishwa, NEC wange withdrawal zile barua za uteuzi
4. Bunge lingewafuta ubunge
5. Nafasi 19 za viti maalum Chadema zingetangazwa kuwa wazi.
6. Chadema waligoma kupeleka majina ya wabunge wake wa viti maalum kwa hoja ya hawayatambui matokeo ya uchaguzi, hawamtambui mshindi na hawalitambui Bunge!.
7. Baada ya maridhiano, walikubaliana kugawana kitu kinachoitwa nusu mkate, hivyo sasa wanayatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020, wanamtambua rais wa JMT na wanalitambua Bunge na wanapokea ruzuku yao toka ofisi ya Msajili wa vyama.

The Best Way Forward
Kutoendelea na kesi, kuwasamehe hao 19, kujipanga kwa uchaguzi wa 2025 kama walivyo shauriwa hapa CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
- J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake

Kwa wale ambao bundle sio issue, kipindi chenyewe ni hiki
View: https://youtu.be/owBvx8H2H68?si=2kaPHEBJkcQoObcS
1. JJ. Mnyika ametoa maoni ya jumla ya Chadema, wametaka miswada yote iondolewe kwanza, serikali ilete kwanza marekebisho madogo ya katiba, minimum reforms, katiba ifanyiwe mabadiliko kwanza ndipo miswada hiyo iletwe.
View: https://youtu.be/CRLiQjOQpro?si=6xgfm7aBX7Lvo0wQ
2. JJ Mnyika amethibitisha jinsi maridhiano na CCM yalivyo isaidia Chadema, ambapo mwanzo waligoma kuutambua uchaguzi na kuyatambua matokeo, lakini kupitia maridhiano sasa Chadema inautambua uchaguzi, inayatambua matokeo ya uchaguzi, inamtambua mshindi halali wa uchaguzi huo, inalitambua Bunge na kumtambua Mbunge wake mmoja tuu, Aida Kenani.
View: https://youtu.be/x5yFws4dc1U?si=Vi0dqREdT7AIhtme
3. Kufuatia Chadema kumtambua rasmi Mhe. Aida Khenani kama mbunge wake rasmi, JJ. Mnyika ameomba Mhe. Aida apewe muda wa kutosha kuchangia, na maoni yake yazingatiwe kama maoni ya kambi rasmi ya upinzani
View: https://youtu.be/r-SmiYZUOXc?si=HOrGl7qHppPYeF5v
4. Pia JJ Mnyika amejitahidi kujibu hoja mbalimbali za mwandishi Pasco Mayalla, zikiwemo hoja kuhusu wale wabunge wake 19, likiwemo jibu la swali ”Kwanini Chadema mpaka leo haijaripoti polisi kuhusu jinai ya kughushi ya wabunge hao 19?”
View: https://youtu.be/-M8HnYQgtAc?si=mBlAuAvub0JcokXp
5. JJ Mnyika, amesema Chadema ina uthibitisho wa uhusika wa mamlaka za nchi katika jinai ya kughushi uteuzi wa wabunge 19, serikali ikihusika na jinai, jeshi la polisi halifanyi uchunguzi!. Hata shambulio la Lissu, mamlaka ilihusika ndio maana mpaka leo hakuna uchunguzi wowote wa kijinai
View: https://youtu.be/CH1amKvbsQc?si=4_QhuIr4MXrYpv5J
6. Pia JJ Mnyika amethibitisha Chadema iliwatimua wabunge wake 19, kihalali kabisa kwa mujibu wa katiba ya Chadema, na Mahakama imethibitisha,

View: https://youtu.be/aJWb6Vkdx_s?si=E0oxq3R74CsGySah
Kipindi kilichopita nilizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema.
Wale ambao hamkukiona na bundle sio issue, mnaweza kukiangalia hapa

Vipindi vijavyo, kwa Chadema, nitamtafuta Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,kwa ACT Wazalendo ,nitamtafuta Zitto na OMO, na kwa CCM Makonda atatosha.

Paskali
 
Mmmm....hapo P umebagaza ....kwenye kesi ya msingi zimepigwa dana dana nyaraka hazikuletwa NEC hakuna kulindana hapo ? ......nini tafsiri ya ile kesi ? Naona Jaji amejikita baraza kuuu Chadema na Cc yake ....hakusema ule mchakato na supporting Docs zake......
 
Naunga mkono hoja, JJ Mnyika ni kichwa cha ukweli!, juzi kati kuna member humu katika bandiko hili Mnyika kutoa somo la Katiba Mpya kupitia clouds Media alimzungumzia Mnyika
Mkuu Umkonto, UmkhontoweSizwe, utakuwa humjui vizuri JJ. Mnyika!, he is one of the very few fine and the good ones Chadema has!. JJ. Mnyika is very good kwenye data collection ila sio kwenye kushindilia misumari, ili Mnyika afanye vizuri he needs a team mzuri to play with, kwa sasa team play hiyo haipo Chadema!. Zamani JJ. Mnyika akiwa Bungeni huku Zitto Kabwe, kule Tundu Lissu, Mnyika ataibua hoja full of dataz, Zitto ambaye ni mjenga hoja mzuri, ataiongezea momentum kisha Lissu ambaye ni mlipuaji mzuri, atabutua!, Spika chali!. Hata mfugaji mzuri wa ambao, hawezi kufunga kama hakuna mtu wa kumpelekea mipira ya kubutua na kufunga mabao!.

Enzi zile wakati PPR ilikuwa ni PPR kweli, wakati vikao vya Bunge vikiendelea Dodoma, nikapenyezewa dossier fulani vyeti, kesho yake nilikwea the first flight to Dodoma, kumfuata JJ. Mnyika kumkabidhi Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Hata ule moto ambao Tundu Lissu huwa anawasha Bungeni from time to time, the data collector ni JJ Mnyika!, ilifikia kipindi tulimuomba Lissu apunguze kumpelekea moto Madam Speaker, Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!.

Kwenye uchaguzi Mkuu wa 2010 JJ Mnyika ndie alikuwa mgombea wa kwanza kujihakikishia ushindi na aliyeutangaza ushindi wa JJ Mnyika sio mwana jf mwingine bali ni huyu huyu Elections 2010 - Mchakato Majimboni: JJ. Myika, Ubungo Yako, Njia Nyeupe

JJ Mnyika is damm good!, but hana team work nzuri to play with na kwa maoni yangu Chadema hii haina team work, angalia hapa Lissu anavyowaita viongozi wenzake Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Kiukweli kabisa uchaguzi wa 2025 upinzani wana kazi kweli kweli to regain back the control of what it used to have!.

P
 
Muovu,mjinga na mkatili.r.i.h
 
Mkuu Lambardi , kesi ya msingi ni kuhusu Baraza Kuu, walipaswa kwanza wapinge uamuzi wa CC kuwatimua kisha uamuzi wa Baraza Kuu kukubali uamuzi wa CC, Mahakama imewapa kile tuu walichoomba, hii maana yake uamuzi wa CC kuwatimua ni uamuzi halali!.

Kama hakuna any documentary evidence ya jinai ya forgery, hiyo CC ya Chadema iliwatimua based on what?. Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?

P
 
Pascal bravo! Nina bandiko humu la kuitaka CHADEMA iridhiane, kina Halima Mdee wasamehewe, ngoma ianze upya. Wanahitajika kwa sasa kuliko wakati wowote ule wa huko nyuma. Hivi sasa waanze mchakato mapema wa kuandaa wagombea majimbo yote. Sina maana waiondoe CCM 2025,ila wasaidie kuijenga nchi.
 
kazee kana matamko mengi kinoma mfu.....

Utaskia Tunataka serikali ifute zuio mikutano ya kisiasa...
Tunaipa serikali siku 5 itekeleze blalaablaa....
Tunaitaka serikali kuwaachia wafungwa wa kisiasa bila masharti

Sikuizi kamepoa kameona hakaskizwi wala kutiliwa maanani
 
Mkuu Kididimo , asante, Chadema wasaidiwe to do the right thing.
P
 
Mnyika ni genius. Nasikia alisomea Seminary na masomo yote ya Form six alipata A zote. Ukoo wao ni genius. Baba yake ni Msukuma alikuwa genius na hata Baba yake mdogo Prof. Batibo ni genius. Uelewa wa Mnyika na kupambanua hoja ni mkubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…