- Source #1
- View Source #1
Wakuu wa JamiiCheck hii uhalisia wake upoje??
===
JOHN MNYIKA APONGEZA JESHI LA POLISI KWA KULINDA DEMOKRASIA NCHINI AMEYASEMA HAYO LEO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUELEKEA MEI MOSI 2025.
LEO TAREHE 30 APRILI, 2025, MAKAO MAKUU YA CHADEMA.
===
LEO TAREHE 30 APRILI, 2025, MAKAO MAKUU YA CHADEMA.
- Tunachokijua
- John Mnyika ni katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Tanzania (CHADEMA), Aliyeteuliwa kuendelea kutumikia nafasi hiyo mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho January, 2025 ambapo Tundu Lissu aliibuka kidedea akimshinda aliyekuwa mshindani wake Freeman Mbowe.
Mnamo tarehe 30, Aprili 2025 Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika alifanya mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya chama jijini Da es salaam ambapo pamoja na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kuelezea matukio ya kukamatwa na kuteswa kwa wanachama na viongozi wa chama hicho.
Kutokana na mkutano huo kumeibuka taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii na ikidaiwa kuchapishwa na Jambo TV kuwa John Mnyika amepongeza jeshi la Polisi kwa kulinda demokrasia.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (KeWorSearch), imebainika kuwa Taarifa hiyo Si ya Kweli, ni ya kutengenezwa kwani haikuchapishwa katika kurasa zao rasmi za Jambo TV.
Aidha Kupitia Mkutano wake na waandishi wa habari Aprili 30, 2025 Mnyika hakutoa kauli yoyote ya kulipongeza jeshi la polisi bali alitumia nafasi hiyo kuonesha ushahidi wa video akidai kuhusika kwa jeshi hilo katika tukio la ukamataji na kuteswa kwa wanachama na viongozi wa CHADEMA Aprili 24, 2025.
"Tutaonesha kwa muhutasari matukio ya msingi yenye kuthibitisha kwamba jeshi la polisi lilikamata viongozi na wanachama wa CHADEMA, lilihusika kupiga viongozi na wanachama wa CHADEMA, lilihusika kufanya uharamia wa kudhalilisha utu wa viongozi na wanachama wa CHADEMA, na baada ya kuonesha matukio haya tutaeleza hatua ambazo chama tutachukua" - alisema John Mnyika.
Kadhalika Mnyika alitaja hatua ambazo chama kilihitaji zichukuliwe kutokana na kile ambacho CHADEMA ilidai kuwa Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro imetoa taarifa za uongo kuhusu madai ya viongozi na wanachama wao kukamatwa, kupigwa na hata kuteswa.
Moja ya hatua hizo CHADEMA ilisema "Kamanda wa Polisi Jumanne Muliro kwa kuongoza zoezi hilo na kwa kusema uongo hadharani mamlaka yake ya uteuzi na nidhamu imchukulie hatua ya kumuondoa kwenye Kanda Maalum ya Dae es Salaam"