John Mnyika awajibu kisheria wanaohoji kuhusu CHADEMA kutokusaini kanuni za maadili ya uchaguzi 2025

Tutajie kesi ambazo chadema wameshitakiwa na kutiwa hatiani ni serikali yako ya ccm.

Lissu ameshitakiwa kesi nyingi za kubumba tutajie moja tu aliyofungwa na viongozi wengine wa chadema.
Alafu mtajie mafisafi ambao walijitamba kabisa bungeni wa ccm na hamna kitu wamefanywa
 
Atakula majibu yake dadeki CCM tumeamua hatucheki na kima

USSR
Soma vifungu vya Sheria alivyoambatanisha na uache kukunja uso! Hayo maadili yalikuwa gazetted lini? Huoni Kama tume inawahujumu ccm kwa kufanya kazi bila kuzingatia Sheria? Nina uhakika anaetoa maelekezo hajui Sheria ndio maana tume inaacha matobo ili wenye akili wakapate haki mahakamani!
Tume imeingilia kazi ya Mutungi ambaye kimsingi ndiye mwenye vyama vya siasa. Sijui Kama unayaona hayo matobo au bado una wenge la no election!
 
Tunaongozwa na akili ndogo.
Akili ndogo haiwezi kamwe kuiongoza akili kubwa. Ukiona hivyo huyo anayejiita akili kubwa ni akili kubwa uchwara. Hakuna ng'ombe atachunga kundi la masai. Yaani miaka 40+ akili ndogo iongoze akili kubwa?
 
Amechemka, maagizo ya chama akazuie hiyo hatua ya uchaguzi, sio kususia kama alivyofanya. Nilitaraji aende hata akatoe protest statement ukumbini, au akachanechane makaratasi ya Tume ukumbini zoezi lishindikane, au awachape ngume waliokuwa ukumbini
No need. Kuchana makaratasi ya tume na kuwapiga ngumi? CHADEMA haina uendawazimu huo. What for?

Mkuu kwanza furahi basi kwa CHADEMA kuwa disqualified kushirki uchaguzi. Hii ni win win situation. CCM mtashinda uchaguzi wote asubuhi mapemaa. Polisi wenu watapaki magari ya washa washa na kuwasaidia kusambaza mabegi ya kura ready-made vituoni. Amani mnayoihubiri kila siku itakuwa ya kumwaga nchi nzima.
 
Anaandika JJ Mnyika Katibu Mkuu.

Kujibu andiko la Wakili Msomi Jonathan Mndeme
———————

Kabla ya vifungu vya 162(2) na (3) vya Sheria ulipaswa kuanza na 162 (1).

Kifungu cha 162(1) kinaeleza Tume baada ya kushauriana na vyama vyote vya siasa na Serikali itandaa na kuchapisha katika Gazeti la Serikali Kanuni za Maadili ya Uchaguzi.

Kwa kifungu hiki anayendaa Kanuni za Maadili ya Vyama Vya Siasa ni Tume sio kikao kikao kati ya Tume na Vyama na Serikali. Kikao ni sehemu tu ya Tume kutekeleza jukumu la kushirikisha. Baada ya kushirikisha huko Kanuni za Maadili hazipati nguvu ya kisheria mpaka kwanza chapishwe katika Gazeti la Serikali.

Strictly speaking Vyama vilipaswa kutakiwa kusaini Kanuni za Maadili baada ya kuwa kwanza Tume imekaa kikao cha Tume, imezipitisha na zimechapishwa kwenye Gazeti la Serikali.

Soma Pia: Mnyika: Sitakuwepo kuwakilisha Chama kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi 2025 kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi

Hivyo, Serikali na Vyama kusaini kwenye mchakato wa kushirikishwa kama ilivyokuwa tarehe 12 Aprili 2025 hakuzuii Chama ambacho haikusaini wakati huo kusaini baada ya kuwa Maadili ya Vyama vya Siasa kuwa yameshachapishwa kwenye Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Kifungu cha 162(2) cha Sheria.

Ili mradi kusaini huko kufanyike kabla ya kushiriki uchaguzi kwa mujibu wa masharti mabaya(yaliyo kinyume cha katiba na sheria) yaliyoko kwenye Kanuni za Maadili kipengele cha 1.5 (a). Ndio maana hata Kanuni za Maadili zenyewe kuanza kutumika kwake kwa mujibu wa kipengele cha 1.3 kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 ni kuanzia siku moja baada ya tarehe ya uteuzi wa wagombea. Hivyo, Chadema ikiamua kusaini kabla ya uchaguzi inayo nafasi kisheria na haki kufanya hivyo. Nafasi kama hiyo imewahi kutolewa kwenye Uchaguzi Mkuu mmoja wapo wa miaka ya nyuma sikumbuki vizuri mwaka hapa nilipo.

Kwa upande mwingine, kwa taathira ya No Reforms No Election Reforms zikitokea za kikatiba au za kisheria zitasababisha pia reforms za Kikanuni ikiwemo Kanuni ya Maadili ya Uchaguzi na kupelekea mchakato kusaini kufanyika tena.
Tlaatlaah atakuwa amelala huku anajamba tu mda huu...akiamka utasikia , gentleman
 
Washangilie upuuzi mwisho wa siku mtatulia kama pop corn kuishia mdomoni!
 
CCM imejaa wasomi wengi tu sema njaa na kutokuwa wazalendo ndo tatizo....watu wanaangalia ugali wao tu matumbo yao yavimbe ila deep inside their brains wanajua CDM ni big brains.
 
Attachments

  • IMG-20250414-WA0011.jpg
    IMG-20250414-WA0011.jpg
    43.3 KB · Views: 14
Back
Top Bottom