Pre GE2025 John Mnyika: Bunge limepuuza maoni ya wadau, linajipanga kupitisha miswada mibovu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndiyo maana yakaitwa maoni. Maoni ni fikra tu za mtu au watu kuhusu jambo fulani.

CHADEMA ni nani ambao lazima maoni yao yafuatwe?


..maoni yaliyopuuzwa sio ya Chadema peke yao.

..hata maoni ya viongozi wa madhehebu ya Kiislamu na Kikristo yamepuuzwa.

..maoni ya kikosi kazi kilichoundwa na Rais nayo yamepuuzwa.

..Kamati ya Bunge imeshindwa kuishauri serikali kutupatia Tume Huru ya Uchaguzi ktk kiwango ambacho wadau na wanazuoni wamekuwa wakipendekeza.
 
Tunahitaji kujenga jamii na taifa lenye raia au wananchi wanaojielewa, wanaoheshimiana, wanaojua jema na baya kimantiki, badala ya kujitoa ufahamu kwa mlengo wa kisiasa.
Hizi fikra kama za wanyama kwa sababu tu ya siasa ziondoke.
Kuna tofauti kubwa sana ya loyalty kati ya wanyama kama mbwa kwa binadamu, na binadamu kwa binadamu.
CCM kama chama tawala na kilichopigania Uhuru, tunatakiwa kuongoza katika kueneza elimu hii (kupigania na kuendeleza Uhuru wa fikra za ki binadamu zaidi).
 
Tunasubiri maazimio ya UN tuliyowakabidhi nyaraka zetu,dadadeki nchi tuipiganiwe wenyewe maamuzi tukapangiwe na UN tokeni tena chadema jogging!
Tatizo lako ni kutokupata elimu tarajiwa, Tanganyika ilikuwa mikononi mwa UN, mwingereza alipewa jukumu la kuisimamia tu na si kuitawala, uhuru wetu uliidhinishwa na UN ambako mwalimu Nyerere alikuwa akienda kujieleza, kwa kifupi hatukuwahi kudai uhuru toka kwa mfalme wa uingereza.
 
Tunasubiri maazimio ya UN tuliyowakabidhi nyaraka zetu,dadadeki nchi tuipiganiwe wenyewe maamuzi tukapangiwe na UN tokeni tena chadema jogging!
Tuendelee kujipanga na maandamono ya kwenda Dodoma kufukuza wapuzi wanajiita wabunge. Tukawaulize wanamwakilisha Nani kama maoni yetu wameyapuuza.
 
Chadema haipaswi susia uchaguzi maana ndo itajipoteza yenyewe.
Dawà ya adui ni kwenda naye kwa njia anazotaka yeye
 
1. Kuandama kwenda UN mlipoteza maboya. Mngeandamana kwenda viwanja vya kawe na mtoe maneno kwa wananchi. Nyie mkaenda kwa weupe.
2. Mnakosa moral push ya kulalamika kwakuwa inabidi msubiri majibu ya barua yenu.
3. Mnatakiwa kuwakumbusha UN wajibu barua yenu
 
Kamati ya Bunge ndiyo iliyoaminiwa kuyapima na kuangalia kama yanafaa. Tuishi hapo
 
Nyie subirini majibu ya umoja wa mataifa, si mlipeleka malalamiko huko? Haya, msubiri kama Gaza inavyosubiri UN iwajibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…