Hakuna cha salamu!
Huyu Katibu Mkuu ana sababu gani za kuendelea kukaa ofisini?
Kwa mambo yanayoendelea ndani ya chama, na kwa makanusho ambayo amekuwa akiyatoa tangu hatua za awali. Hadi kutimia kwake, bado anaendelea kukanusha!
Katibu Mkuu, umefanywa mjinga kiasi hicho au unaujua ukweli kisha unaamua kujitoa ufahamu na kuwafanya wanachama wajinga wasioelewa?
Sikuwahi kutilia shaka uwezo wa Mnyika, na hata ulipojiengua kugombea ubunge nilikupongeza na sababu zako unataka kujikita zaidi kitaifa kukijenga chama. Japo wengine walisema ni machale yako ulinusa harufu ya kushindwa kwa kishindo.
Sasa katika hili hapana, Mwenyekiti siwezi kumsemea. Yeye ni mwenye chama na hajatoa tamko lolote hadharani.
Iwe kwa kujua yanayoendelea, au kwa kuzungukwa na kufanyika kinyume nawe. Kwa heshima uliyokuwa nayo, hupaswi kuendelea kukaa ofsini.
Kujiuzulu ni chaguo sahihi ili kulinda heshima yako binafsi, kwa maana heshima ya chama tayari imeshatikiswa na haitarajiwi kurejea leo wala kesho.
Ncha Kali.