John Mnyika: Rais Samia "aidha amepotoshwa au ameamua kusema uongo”

John Mnyika: Rais Samia "aidha amepotoshwa au ameamua kusema uongo”

Kauli alizo zitumia Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika dhidi ya Rais zina ukakasi sana, zimekosa adabu na nidhamu kwa kiongozi wa nchi.

nadhani kwa utovu huu alio uonyesha Mnyika nimeshangaa kwa nn alipewe nafasi ya ukatibu mkuu lkn pia nitashangaa sana kama Mnyika hakuchukuliwa hatua kali kwa kauli za kifedhuli na dharau alizo zitoa.

hata kama hato chukuliwa hatua za kisheria lkn namshauri Mnyika ajivunze adabu na nidhamu ya uongozi, kwa nafasi yake hapaswi kuwa mlopokaji kama wapiga debe.
Yaani kwako Raisi unamuona kama Mungu,si ndoo hivyo ?

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
nadhani hata kwa wakati huu mali za Mbowe zote zinapaswa zizuiliwe pomja na acount zake.
lazima sheria ya Ugaidi ifuatwe kikamilifu.

Nilishangaa sana alipo fikishwa nakaona Mbowe anaruhusiwa kukumbatiana na jamaa zake!!
mahakamani lazima gaidi alindwe, nilishangaa pale kisutu inakuwaje Gaidi anapewa nafasi ya kukubatiana na watu mahakamani?!! hili halipaswi kujitokeza. ni muhimu vyombo vyetu vyote vikajifunza kutoka mataifa mengine namna ya kudili na watuhumiwa wa Ugaidi.
kamwe vyombo vyetu vya ulinzi na usalama visikubali kuhadaiwa au kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na mawakili au viongozi wa chadema, lazima sheria ifuatwe kikamilifu kama ilivyo kuwa inafuatwa kwa washitakiwa wengine.
nilishangaa kuwaona watuhumiwa wenzake wa Ugaidi wamefungwa pingu huku Mbowe akiwa hajafungwa pingu, sijafahamu kwa nn,!! kama hakuna ulazima basi wote wasifungwe pingu, sio baadhi wanafungwa wengine hawafungwi!!!
 
Chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kimesema rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan “aidha amepotoshwa au ameamua kusema uongo” katika baadhi ya mambo ambayo ameyatolea ufafanuzi katika mahojiano yake maalumu aliyofanya na BBC.

Kauli hiyo, imetolewa hii leo na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika pindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mnyika, amepinga baadhi ya hoja zilizotolewa a rais Samia ikiwemo zile zinazodai kwamba, Mbowe kwa muda mrefu alikuwa nje ya nchi baada ya kujua ana kesi inayomkabili, hivyo kusema, “hakuna wakati ambao kiongozi huyo ametoroka nchi au amekuwa nje ya nchi kinyume cha sheria.”

Mnyika ameongeza kusema kuwa, wakati ukifika, “chama kitatoa vielelezo vitakavyoonyesha uhalali wa safari hizo.”

Hata hivyo, rais Samia alipoulizwa iwapo kesi hiyo ya Mbowe ni ya kisiasa, alikataa kulitolea ufafanuzi wa kina kwa kusema kuwa, tayari kesi hiyo iko mahakamani, hivyo ni vyema kuachia mahakama kufanya kazi yake.

Lakini tayari Chadema inamlaumu rais Samia kwa madai kwamba ameingilia uhuru wa mahakama, na kusema, wameongeza na jopo la mawakili wao ili kuona ni hatua gani wanaweza kuchukua.

Aidha miongoni mwa mambo mengine ambayo Chama hicho kimeyajibu ni pamoja na kauli ya rais aliposema kuna tofauti kati ya demokrasia ya kisiasa na fujo za kisiasa, hivyo kuashiria kwamba, baadhi ya maandamano yanayoitishwa na vyama vya kisiasa kama fujo za kiasa.

Hata hivyo, kauli hii inaonekana kuwa mwiba kwa chama hicho cha upinzani ambapo Mnyika amesema kupiga marufuku mikutano hiyo ya hadhara ni kinyume cha katiba ya nchi na sheria za vyama vya kisiasa.

Chadema pia imedai kwamba rais Samia amepotosha umma pale aliposema kwamba, wananchi wamekubali tozo za simu, ila kiwango cha tozo ndio hawajakikubali.

Nchini Tanzania kumekuwa na maoni tofauti baada ya BBC kufanya mahojiano na rais Samia ambayo yamegusia nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na masuala mengine kadhaa.

Sorce: BBC Swahili
Huyu wala hapotoshwi bali nimegundua baada ya mwendazake ku practice udini na ukanda sasa yeye kaamua kuendeleza hyo precedence hasa ktk UDINI.
NI AKILI YA KIPUNGUANI UMETOKA KUWAACHIA MASHEHE HALAFU UNAKAMATA WANASIASA.
AMESEMA HAKUNA SIASA KTK KUMKAMATA MBOWE ILA MBONA HAKUSEMA KULIKUA NA NINI KTK KUWAACHIA MASHEHE

MAMA UTAONDOKA KWA AIBU NA UTAFANYA WANAWAKE WOTE WAONEKANE WA HOVYO
 
Rais kapotoshwa na nani?

Huyu ni Rais gani anayepotoshwa kila mara namna hii?

Kila akiboronga, ni kapotoshwa!

WTF 😳.

Ina maana ni mweupe kiasi hicho cha kuweza kupotoshwa kila mara?

Hili nalo neno.Si hakika lakini nafikiri “kupotoshwa” ni aina ya utamaduni mpya uliozuka pengine kupunguza ukali wa maneno kama”Kadanganya”.
 
Kauli alizo zitumia Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika dhidi ya Rais zina ukakasi sana, zimekosa adabu na nidhamu kwa kiongozi wa nchi.

nadhani kwa utovu huu alio uonyesha Mnyika nimeshangaa kwa nn alipewe nafasi ya ukatibu mkuu lkn pia nitashangaa sana kama Mnyika hakuchukuliwa hatua kali kwa kauli za kifedhuli na dharau alizo zitoa.

hata kama hato chukuliwa hatua za kisheria lkn namshauri Mnyika ajivunze adabu na nidhamu ya uongozi, kwa nafasi yake hapaswi kuwa mlopokaji kama wapiga debe.
Wapi Mnyika kakosea? Jibu hoja kwa kuijibu hoja kwa hoja..sio kuleta uvyama
 
Kauli alizo zitumia Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika dhidi ya Rais zina ukakasi sana, zimekosa adabu na nidhamu kwa kiongozi wa nchi.

nadhani kwa utovu huu alio uonyesha Mnyika nimeshangaa kwa nn alipewe nafasi ya ukatibu mkuu lkn pia nitashangaa sana kama Mnyika hakuchukuliwa hatua kali kwa kauli za kifedhuli na dharau alizo zitoa.

hata kama hato chukuliwa hatua za kisheria lkn namshauri Mnyika ajivunze adabu na nidhamu ya uongozi, kwa nafasi yake hapaswi kuwa mlopokaji kama wapiga debe.
Da, watu bado hamtaki kuacha tabia mbovu ya kulamba watu makalio. Yule mlimuabudu kuliko Mungu hadi Mungu akaona huu sasa ni ujinga akamshusha 6 feet, sasa mmenza tena na huyu lakini Mungu hajaribiwi na alisema yeye ni Mungu mwenye wivu.
 
Kesi iko mahakamani sasa Mnyika ana shida gani tena kumfokea raisi wetu!! Au CDM wanamtest mama!

Mama ukicheka na nyani utavuna mabua ndo maana mtangulizi ilifika mahali akaamua kwenda nao sawa.

Wanamwambia atii utawala wa sheria huku wanamuambia aingilie mahakama kwa kuifuta kesi!

Kama Mbowe Hana hatia mbona CDM hawataki trial mahakamani badala yake wanataka ifutwe kinyemela?
Unajua kesi inaweza kutumia hata miaka 5 au zaidi kabla ya hukumu?Tatizo ni kuwa haina dhamana hivyo mwanya huo unaweza kutumiwa na watawala kuwakomoa wapinzani!
Tumeshaona kesi za namna hiyo nyingi tu na ikikaribia hukumu,DPP anasema hana nia ya kuendelea na kesi!Wakati huo huo mtu alishasota sana!
Viongozi wa CDM wamekuwa na kesi nyingi mahakamani,ila wanapata dhamana na hivyo kesi kuendelea bila maumivu na nyingi huwa wanashinda!
Hizi zisizo na dhamana ni style mpya ya kuwakomoa!
 
Rais kapotoshwa na nani?

Huyu ni Rais gani anayepotoshwa kila mara namna hii?

Kila akiboronga, ni kapotoshwa!

WTF [emoji15].

Ina maana ni mweupe kiasi hicho cha kuweza kupotoshwa kila mara?
Hii taasisi ya urais awamu inaashiria ni mradi hewa
 
Rais kapotoshwa na nani?

Huyu ni Rais gani anayepotoshwa kila mara namna hii?

Kila akiboronga, ni kapotoshwa!

WTF [emoji15].

Ina maana ni mweupe kiasi hicho cha kuweza kupotoshwa kila mara?
Pain is beautiful.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Kauli alizo zitumia Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika dhidi ya Rais zina ukakasi sana, zimekosa adabu na nidhamu kwa kiongozi wa nchi.

nadhani kwa utovu huu alio uonyesha Mnyika nimeshangaa kwa nn alipewe nafasi ya ukatibu mkuu lkn pia nitashangaa sana kama Mnyika hakuchukuliwa hatua kali kwa kauli za kifedhuli na dharau alizo zitoa.

hata kama hato chukuliwa hatua za kisheria lkn namshauri Mnyika ajivunze adabu na nidhamu ya uongozi, kwa nafasi yake hapaswi kuwa mlopokaji kama wapiga debe.
Taka wew
 
Tafadhali wenye Ukweli kamili wa Kuwazidi hawa Wawili juu ya lini Ndugu Freeman Mbowe alikamatwa na Kufunguliwa Kesi yako huko Polisi mtuwekee hapa ili tumalize Utata na pia tujue kati ya Rais Samia na Katibu Mkuu CHADEMA Mnyika nani ni Muongo na hafai tena Kuaminiwa na Watanzania.
 
Back
Top Bottom