LGE2024 John Mnyika: Takwimu alizotoa Waziri Mchengerwa kuhusu zoezi la uandikishaji wapiga kura ni za uongo!

LGE2024 John Mnyika: Takwimu alizotoa Waziri Mchengerwa kuhusu zoezi la uandikishaji wapiga kura ni za uongo!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
addict wa malalamiko inafaa uwe sobar house saivi wewe for rehabilitation 🐒
Nasema hivi, huo uchaguzi ni upuuzi kama upuuzi mwingine. Na wananchi wameonyesha dhahiri kuwa hakuna uchaguzi bali ukhanithi.
 
Screenshot_2024-10-20-20-16-11-1.png


😆😆😆😆😆
 
Katibu wa CHADEMA, John Mnyika leo akiongea na waandishi amemkaanga Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kwa kusema kuwa takwimu alizozitoa waziri huyo hivi karibuni ni za uongo.

Mnyika amesema kuwa kauli ya Mchengerwa alidanganya aliposema kuwa kuna mwamko mkubwa wa wananchi katika zoezi la andikishaji na kwamba asilimia 45 ya watu walikuwa wameshajiandikisha kwenye daftari.

Soma pia: Zoezi la Uandikishaji wa wapiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umefikia asilimia 45. Tanga yaongoza!

"Mwamko wa wananchi kwenda kujiandikisha ni mdogo. Hata takwimu alizotoa Waziri kwamba watu wameajiandikisha ni asilimia 45 ya watu waliopaswa kujiandikisha ni takwimu uongo. Waziri ametoa takwimu za uongo. Sasa kwa sababu Waziri ametoa takwimu za uongo kwamba mwamko ni mkubwa sana kiasi kwamba nusu ya wananchi wamejiandikisha wameanza kutoa maelekezo huko chini"

Source: Jambo TV



Chadema mambo mengine mnafeli Sana

So wakijitokeza wengi au wasipojitokeza kabisa Nani anapata faida au Nani anapata hasara?

Chadema mna Hamu kusikia ni 2% Tu wamejiandikisha eeh nyie mnabenefit na nini?

Okay let's say watu hawajakwenda kujiandikisha na uchaguzi hautofanyika so viongozi waendelee

Eeh nyie mna wenyeviti wangapi?
 
Back
Top Bottom