Mchezo wa kugalagala kwenye matope, usidhani kambale atauchukia, ndio kwanza anapata mzuka. Na bado, Kisutu wakitoa uamuzi wowote ule, na wenyewe unakatiwa rufaa.
Lengo main case ya uhaini isisikilizwe tubaki na maombi madogo na rufaa zilizojaa kila mahali, na mtuhumiwa akibaki anabeba mitondoo kusubiri kesi ndogo na rufaa zilizojaa mahakama za juu. Kwa wataalamu wa kufanya wiring ya mambo ya kisheria, na kutegesha sehemu ili shoti ya umeme itokee, wanaweza kumkalisha Lissu mpaka 2027 magereza.
Lissu atabaki akitoa mihadhara ya academics mahakamani, lakini haitasogeza hata vumbi kwa hatua moja