GE2025 John Mnyika: Tutamshauri Lissu tukatie rufaa maamuzi ya ''Mashahidi wa Siri''

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema wao kama chama hawajaridhishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu kuhusu mashahidi wa siri dhidi ya kesi ya Tundu Lissu.

Kuhusu maamuzi, soma Mahakama Kuu yapigilia msumari uamuzi kufichwa kwa mashahidi wa Jamhuri katika kesi ya Tundu Lissu

Amesema kuwa wataangalia namna ya kushauriana na Tundu Lissu waangalie namna wanavyoweza kukatia rufaa maamuzi hayo.

Labda kwa minajiri ya kuweka rwkodi sawa lakini sioni matumaini kwa hicho wanachofanya.
 
Ukifuatilia vizuri kesi hii, utaona kuwa Jamhuri hawana mashtaka yoyote yenye mashiko ya kumshtaki na kumshikilia Lissu. Hivyo, wanazua jambo ambalo litasababisha aendelee kukaa ndani.
Ukiteguka mtego huu, wanakuja na mwingine. Kwa sasa wamekuja na suala hili la mashahidi, wakijua upande wa mshtakiwa hawatakubaliana nalo, hivyo utazuka ubishani wa kisheria, ambao maamuzi yake yatachukua siku kadhaa. Likiisha hilo, watakuja na lingine, ambalo nalo litaleta ubishani, ambao utachukua siku kadhaa, kupata ufumbuzi. Na vyote waviletavyo, wanaruhusiwa kisheria
Hii kesi, inaweza kufika mwaka kesho, labda waamue kuifuta tu! Kama kumtesa tu, kwa kweli wamefanikiwa! Na huyo, ni gwiji wa sheria. Je 'mbumbu wa sheria' kama mie, si ningefia tu mahabusuni!!!
Hawana mashtaka na wala hawana dhamira ya kumshtaki zaidi ya kumzuia kwenye Ndoto yake ambayo nayo haina mwisho mpaka itimie.
 
Lisu anaenjoy zaidi kuishi korokoroni ukonga kuliko uhamishoni ubeligiji.

uropokaji unaokiuka sheria, ujuaji wa kijinga na ubishi wa kilofa vinamsulubisha vizuri sana.
ni Lazima atanyooka tu 🐒
TAL ataachiwa. Hii kesi Jamhuri haitakuwa na haja ya kuendelea nayo huko mbeleni maana kumnyonga haiwezekani.
 
Ukifuatilia vizuri kesi hii, utaona kuwa Jamhuri hawana mashtaka yoyote yenye mashiko ya kumshtaki na kumshikilia Lissu. Hivyo, wanazua jambo ambalo litasababisha aendelee kukaa ndani.
Ukiteguka mtego huu, wanakuja na mwingine. Kwa sasa wamekuja na suala hili la mashahidi, wakijua upande wa mshtakiwa hawatakubaliana nalo, hivyo utazuka ubishani wa kisheria, ambao maamuzi yake yatachukua siku kadhaa. Likiisha hilo, watakuja na lingine, ambalo nalo litaleta ubishani, ambao utachukua siku kadhaa, kupata ufumbuzi. Na vyote waviletavyo, wanaruhusiwa kisheria
Hii kesi, inaweza kufika mwaka kesho, labda waamue kuifuta tu! Kama kumtesa tu, kwa kweli wamefanikiwa! Na huyo, ni gwiji wa sheria. Je 'mbumbu wa sheria' kama mie, si ningefia tu mahabusuni!!!
Pia upande wa mashtaka wanatumia udhaifu wa Lissu kupenda kuongea kwa muda mwingi mahakamani. Kwa hiyo wanaibua hoja chokonozi, Lissu ataijibu kwa masaa matatu, kuja kushtukia saa nane,muda umeisha, kesi inaahirishwa
 
Hivi kweli watanzania tumeshindwa kuandamana kwa kiwango kikubwa kumhusu Lissu? Aise mimi moyo unateseka mno ..tumerelax mno hvi Nyerere angejibweteka namna hii leo tungekuwa wapi?
Natamani nipajue anapoishi wakili wanserikali kwa kesi ya TL..sambaza petrol jumba zima mfyu😞
 
Kwahiyo unaona raha mwenyewe ...!
 
Rufaa tena? Aisee uchaguzi utapita Lissu akiwa jela. Halafu watamwachia baadaye!
 
Hivi kweli watanzania tumeshindwa kuandamana kwa kiwango kikubwa kumhusu Lissu? Aise mimi moyo unateseka mno ..tumerelax mno hvi Nyerere angejibweteka namna hii leo tungekuwa wapi?
Natamani nipajue anapoishi wakili wanserikali kwa kesi ya TL..sambaza petrol jumba zima mfyu😞
Hatuna haja ya kuandamana TAL ni Mtu wa Mungu
 
Pia upande wa mashtaka wanatumia udhaifu wa Lissu kupenda kuongea kwa muda mwingi mahakamani. Kwa hiyo wanaibua hoja chokonozi, Lissu ataijibu kwa masaa matatu, kuja kushtukia saa nane,muda umeisha, kesi inaahirishwa
Mkuu, upo sahihi. Anajikuta anajikaanga mwenyewe! Na wao, wanalijua hilo, kuwa ANACHOKOZEKA!
 
Hivi kweli watanzania tumeshindwa kuandamana kwa kiwango kikubwa kumhusu Lissu? Aise mimi moyo unateseka mno ..tumerelax mno hvi Nyerere angejibweteka namna hii leo tungekuwa wapi?
Natamani nipajue anapoishi wakili wanserikali kwa kesi ya TL..sambaza petrol jumba zima mfyu[emoji20]
Mkuu, maandamano ya sisi Watanzania!!? Alipigwa risasi mchana kweupeeeee, tukabaki kulaani mitandaoni. Amekuja kukamatwa kweupeee, tena kwenye mkutano wa hadhara, 'PEOPLES' kibao wakishuhudia,hakuna aliyejitokeza kumpigania !!!! Leo hii, tumeshiba ugali, na tumeridhika na maisha tuliyonayo, tunaweza kuingia mitaani kuipinga DHURMA?
Tumuombe Mwenye Enzi Mungu, atufumbue akili na macho!
 
Kama inawezekana, kata rufani Court of appeal. Huko bado kuna ka harufu ya haki, wanaweza kukaidi maagizo. Huyu binti ilitegemewa , hawezi kukaidi maagizo!

Hakuna hakimu ataenda kinyume na maelekezo , nyie mwombeeni tu MTU wenu labda Mungu aingilie kati.
Wala msipoteze muda yeye angekaa tu huko gerezani azoee tu maisha ya huko. Aachane na mambo ya mahakamani kujifanya anajua sheria, hivi pale mnavyoona inatumika sheria au utashi?

Hivi chadema hawajifunzi tu, wale COVID. 19 si mlewapeleka mahakamani, nini kilitokea sihao mpaka wamemaliza ubunge wao. Tujifunze kuwa siasa katika afrika ni kitu kichungu ukubaliane na yote la sivyo uwe mnafiki. Mzandiki au shetani kabisa.

Rejea kauli ya Rostam kuhusu mahakama
 
Back
Top Bottom