john mnyika wa CHADEMA alipata Div ngapi?


Nadhani wakuu wengi hapa mnadhani na hate vile Mnyika alipata A zote.Wakuu niwahakikishie kuwa sina chembe ya chuki hata moja!Simpimi Mnyika kwa matokeo yake ya sekondari,na hata elimu yake.Sisemi Mnyika hafai kuwa Mbunge wa ubungo kwavile alipata point 7 au hakupata point 7.Kama elimu ya kwenye makaratasi ndiyo kuwa kichwa na kiongozi bora,mbona basi asiwe Mh.Chenge aliyesomea Harvard?Haya yote nayajua wakuu.Hoja yangu ni kwamba tusiite watu vichwa eti kwavile walipata A nyingi sekondari.Mbona ni rahisi tu wakuu,shida iko wapi?
 
Sasa usingeni quote basi.Vinginevyo ungejibu hoja at hand na siyo kuandika as if unajibu hoja ambazo nilizisema.
The really important question here to me is Mnyika kafanya nini na ana vision gani, chama chake kina policies gani zinazotekelezeka vipi.

Tuna ma legit Ph.D kwenye cabinet wanaendeshwa tu na kupiga mark time.Academics ni muhimu lakini si kila kitu, actually klkama mtu si discerning ukipanga unaweza kumpa mtu arrogance akatuangusha kama our mutual policy wonk aka Ben Mkapa.
 
Mmmh, huyu jamaa nakumbuka nilikuwa namuona pale mlimani chuo kikuu wakati huo nikiwa nimeajiriwa na kampuni moja ya usafi pale chuo!! Sasa kama alipata zero mlimani alipandaje? Au alikuwa anasoma twisheni?
 
Mimi kwanza nampa big-up huyu mshikaji, kama alipata zero basi ilikuwa
bahati mbaya katika kipindi chake cha elimu, huyu jamaa ni mpiganaji
whether alisoma tuition au alireseat sijui, ila lengo lake alikuwa nalo na alihitimu
Mlimani pale. Nafiri yeye kupata zero sio suala la kudiscuss kwa sasa ila
tudiscuss mustakabadhi mzima wa yeye kugombea ubunge 2010.

Success comes as a result of undefined ways.
 
Dr. William Shija
aliwahi kupata division zero ktk mtihani wa kidato cha nne, alipokuwa anasoma Bwiru Boys. Lakini baadae alijiandeleza akafanya Ph.D.

Kwa Tanzania kuna mazingira yasiyo sawia ktk misingi ya elimu na ndio maana lolote laweza tokea kwa wakati wowote.

Tanzania mtu kupata zero sio kwamba ni mjinga zaidi ya mtu aliyepata A zote, na aliyepata A sio kwamba ni mwelevu kuliko yule aliyepata zero.

Ndio maana kutokana na mazingira ambayo hayana pivot sawia ,utakuta watanzania wengi tunathirika kielimu tunapobadirisha ngazi moja hadi nyingine, kitu ambacho nafikiri nikinyume cha hali ya kawaida ya mwadamu.
 
wakuu, mstahiki amefanikiwa kuharibu hali ya hewa kwa njia rahisi sana

his comment ilikuwa ya authenticity ya elimu ya John, na John akajibu vizuri sana... lakini kama ilivyo ada, tukaingia kwenye ubunge, personal etc.

My points
Mnyika hakupata zero kama alivyosema
wanaosema kuhusu wizi wa mitihani, you have to be intelligent kufaulu huo mtihani hata kama umeiba... na John hahitaji mtihani wa wizi
Kuhusu la ubunge (ingawa mleta mada hakuweka wazi)... John deseerves to be Mbunge wa ubungo kwa sababu kuu mbili one, he is capable and the best candidate so far and secondly, he was robbed in 2005 na nyang'au Keenja
 
John Mnyika ni mbunge wa ubungo mpende msipende!
mtake msitake, acheni siasa za kuchafuana!

Salute Mkuu.This time presha zitawapanda na kushuka,lakini ukweli unabaki pale pale.Ubunge ni wa Mnyika!
 
🙁
Mstahiki,

Asante kwa swali lako, Jibu ni kwamba sio kweli. Turejee kwenye mijadala ya msingi kwa taifa letu.

JJ
Asante sana JJ, maswali magumu kama haya, huhitaji majibu yanayokwendana sawia. Huu ni mwanzo tuu, naomba ujiandae kwa mengi katika safari yako ya ukombozi wa jimbo la Ubungo, character asassinations za kila aina zitatumika kuhakikisha hausimami. Nakuhakikishia jimbo la Ubungo ni lako.. unless otherwise!.
 
Siasa haihitaji usomi tu.Hebu angalia wanasiasa hawa na linganisha waliyoyafanya maishani......

Wasomi
Prof.John Machunda(RIP)
Prof. Jumanne Maghembe
Prof. Philemon Sarungi
Prof.Jumanne Mikidadi
Prof.Idriss Mtuliya

Wasio wasomi
Abeid A.Karume
Rashid Kawawa
Edward Sokoine

Hata Mwalimu sidhani kama alipata hiypo Divisheni wani
 
Mstahiki,

Asante kwa swali lako, Jibu ni kwamba sio kweli. Turejee kwenye mijadala ya msingi kwa taifa letu.

JJ

Well said kiongozi. Short and clear. Kama ana maswali mengine sasa akuulize kwa PM.

Nakuahidi kura yangu.
 
It surely doesnt matter. Lililo wazi na kwamba ame-demonstrate kwamba ana leadership qualities zinazohitajika ili kulifanya jimbo lisonge mbele maana ameweza ku-define priorities na ku-identify shida zinazowakabili wapiga kura na hili halitegemei idadi ya digrii ambazo mtu anazo. Tumeshuhudia majimbo yanayoongozwa na maprofesa na performance yao katika kutatua kero ikawa so dismal. Hata hao waliomtangulia Mnyika jimboni ubungo walikuwa ni wasomi wazuri sana lakini kipi walichofanya? nadhani ufike wakati tuelewe kwamba idadi ya vyeti pekee haiwezi kuleta tija kama mtu hyuko pragmatic na hana mapenzi kwa wapiga kura wake.
 
N hasa hizo digrii zinapokuwa hazina uhusiano sana na kazi za siasa!
 
Ni bora kuongozwa na mtu wa kawaida mwenye mapenzi mema na watu wake/nchi yake kuliko kuongozwa na mtu aliyebobea kwenye elimu , mwney uchu, mzandiki na aliye na visheni ya kuhujumu nchi kwa ubinafsi wake. Unaweza soma na kumaliza digrii za huko Havard lakini ni mwizi nambari moja na bingwa wa kubaka mali za umma.
 
Mwacheni achukue ubunge wanaosema hajasoma ni haters kama GT ambao kila siku kuwashambulia wakristu,bora Mnyika hata kama ana zero kuliko Ncimbi mwenye PhD feki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…