John Mnyika: Watu wenye silaha wamemchukua Mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA)

John Mnyika: Watu wenye silaha wamemchukua Mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA)

CHADEMA

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
490
Reaction score
2,471
Mbunge wa Kibamba kupitia CHADEMA, John Mnyika kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter amesema kuwa Chadema Mdude amechukuliwa na Watu wenye silaha

Aidha, yeye mwenyewe amesema CHADEMA inafuatiloa suala hilo na taarifa zaidi itatolewa muda si mrefu

======

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA ZA AWALI KUHUSU TUKIO LA MDUDE NYAGALI (MDUDE CHADEMA)


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika hali ya dharura, kinafuatilia kwa karibu, taarifa za Mdude Nyagali (Mdude Chadema) kuvamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawajatambulika, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, majira ya jioni ya leo (saa 12 kuelekea saa 1) yalifika magari mawili katika eneo la ofisini kwa Mdude, Vwawa mjini, kisha wakatelemka takriban watu wanne, ambao walimkamata kijana mmoja aliyekuwa nje ya ofisi hiyo wakampeleka kwenye mojawapo ya magari waliyokuja nayo huku wengine wakiingia ndani ya ofisi, alikokuwa Mdude.

Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi kulisikika purukushani, watu hao wakijaribu kumkamata Mdude huku wakimpiga na yeye akipiga kelele za kupinga kitendo hicho na kuomba msaada.

Taarifa za awali ambazo Chama kimezipata kutoka kwa mashuhuda hao zimedai kuwa baada ya kusikika kwa purukushani na kelele hizo, baadhi ya wananchi walijitokeza kutaka kujua kinachoendelea na kutoa msaada, ghafla watu hao waliokuwa wakimpiga Mdude wakatoa silaha aina ya bastola na kuwatishia wananchi hao, kitendo kilichowaogofya wananchi na kukimbia kwa hofu. Imedaiwa kuwa watu hao walimuingiza Mdude kwenye 'buti' ya mojawapo ya gari hizo, wakamuachia yule kijana mwingine kisha wakaondoka na Mdude kuelekea kusikojulikana.

Tayari CHADEMA kupitia kwa Viongozi wa Chama katika eneo husika na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Pascal Haonga, kimevitaarifu vyombo vya dola mkoani Mbeya, kwanza kutoa taarifa ya tukio hilo lenye mazingira ya utekaji pia kutaka kujua kama kuna askari waliopewa kazi ya kwenda kumkamata Mdude.

Hadi sasa haijulikani Mdude yuko wapi! Tupaze sauti zetu sote kulaani tukio hili na kutaka Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama.

Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

1556988236858.jpg



Zaidi, soma;




 
Wasiojulikana kile kitengo maarufu cha Dikteta pale Ikulu ili kuwanyamazisha wanaomkosoa kwa kuwateka, kuwatesa na hata kuwaua kimeibuka tena kwa kasi ya kutisha.
 
Watawakana kumteka kisha baada ya mwezi waseme alikua anahojiwa.

Wiki nzima wakili wa arusha alikua anatafutwa bila mafanikio, baada ya jamii kuanza kupiga kelele ndo wanajitokeza kusema hakutekwa bali ana hojiwa .

Kama nia yao ni nzuri kwanini wawavizie katka ukamataji. ? . Kwanini iwe siri. ? kwanini watumie magari yasiyo na namba za utambulisho? .


Kwanini serikali isihusishwe na utekaji. ?
 
Wasiojulikana kile kitengo maarufu cha Dikteta pale Ikulu ili kuwanyamazisha wanaomkosoa kwa kuwateka, kuwatesa na hata kuwaua kimeibuka tena kwa kasi ya kutisha.
Ni kitengo maalumu cha Ccm na wala hakipo ikulu
 
Back
Top Bottom