Magari mawili aina ya Nissan Patrol na Toyota Landcruzer (yasiyo na namba za usajili) yakiwa na watu kadhaa wenye silaha za moto wamevamia eneo la kazi la Ndugu Mpaluka Mdude Nyagali, maarufu kama Mdude Chadema dakika chache zilizopita. Mdude ni fundi wa Computer na masuala ya IT na ofisi yake ipo maeneo ya Vwawa, huko Mbozi.
Watu hao wamefyatua risasi moja hewani na kuwaamuru watu wote waliokuwemo kulala chini kisha wakamchukua Mdude na kuondoka nae kwa mwendo wa kasi. Baada ya kuondoka mashuhuda wa tukio hilo wameenda kutoa taarifa kituo cha polisi Vwawa lakini bado hawajachukua hatua yoyote.
Nimezungumza na baadhi ya mashuhuda waliokua eneo la tukio, Mbunge wa Viti maalumu Songwe mama Sophia Mwakagenda, na Mgombea ubunge wa Vwawa Ndg.Fanuel Mkisi ambao wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Tunaomba tupaze sauti kwa nguvu ili Mdude apatikane akiwa salama.!