mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Ameandika Mrema kupotia ukurasa wake wa X,
"Nimejulishwa na mwenyekiti wa tawi langu, ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama!
"Nimeshangaa sana maagizo hayo na mpango huo ambao unaratibiwa na viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Segerea bwana Kitomary!
"Wanademokrasia, wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme! Wanataka kufukuza wengine uanachama ili wasisemwe!
"Demokrasia ni pamoja na uhuru wa mawazo na kutoa maoni! CHADEMA ndiyo chama changu, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote!
"Nawatahadharisha acheni ujinga huo!"
Soma>> Aliyetuhumiwa kupanga kumfukuza John Mrema CHADEMA akanusha