Pre GE2025 John Mrema: Wanataka kunifukuza uanachama. Wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme

Pre GE2025 John Mrema: Wanataka kunifukuza uanachama. Wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Press baada ya uchaguzi ni kuingiza fujo. Hali idhibitiwe ili kutoa nafasi kwa utawala mpya kujenga umoja.
 

Ameandika Mrema kupotia ukurasa wake wa X,

"Nimejulishwa na mwenyekiti wa tawi langu, ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama!

"Nimeshangaa sana maagizo hayo na mpango huo ambao unaratibiwa na viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Segerea bwana Kitomary!

"Wanademokrasia, wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme! Wanataka kufukuza wengine uanachama ili wasisemwe!

"Demokrasia ni pamoja na uhuru wa mawazo na kutoa maoni! CHADEMA ndiyo chama changu, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote!

"Nawatahadharisha acheni ujinga huo!"


Huko Chadema watu wa Tawi au kata tu wanaweza kumfuta mtu uanachama ? Au ni mbinu kukichafua çhama chini ya Lissu kimtindo.
 
Ukichagua lissu, umechagua u stronger katika chama.

Ukichagua mbowe umechagua u togetherness katika chama.
 
Mwenyekiti anautaka uongozi wa nchi, na hakuna kipindi ganda la ndizi kama kipindi hiki katika kinyang'anyiro(in mwasha kububujikwa'z voice).

Hivyo hatokubali/hawezi kukubali matabaka ndani ya chama na hilo analiweza, mie namkubali, amenyooka kama Magufuli japo waligombanishwa(so sad )

Akiruhusu makundi,
Atawatumia watu wa ndani kama kombora kumwangamiza singida one
 
Uongozi mpya msiruhusu haya mambo ya kufukuzana mapema hivi. Haki ya kutoa maoni ni haki ya kila raia, ilindeni na muiishi demokrasia ambayo kila siku tunaihubiri.

Uongozi wa visasi si mzuri, mtakuwa mmeanza na mguu wa kushoto.

Tunafikiri hili jambo halitatokea.
Mpaka sasa hivi ni kauli yake tu hatujasikia mwingine akisema, ila mbona kuna watu kama Yericho Mengele akina Ntobi kina Wenje mbona hatusikii maneno?

Huo mkutano wa waandishi wa habari anaotaka kuufanya baada ya uchaguzi una heri? Kwa nini asifanye mkutano na uongozi?
 
hivi huyu mrema anasema "... wanataka ...." wameshinda" kwani yeye hayuko CHADEMA?!
 
LISSU KAANZA KAZI YAKE .
WANAOMPENDA LISSU HAPO HAJASHIKA TZ ....
AKISHIKA SIMNASEMA CCM INAWAUZA HUYU KILA BAYA MLILOKUWA MNALIOTEA TAZ HUYU ATATIMIZA NA ZAIDI .
HUYU MTU NI MBINAFSI , ROHO MBAYA IPO NA HAITATOKAGA . SASA ANAWANYIMA UHURU WENZAKE WA CHADEMA. ELEWENI HUYU NI JOTO na BADO ANASHANGILIA YANGA TUTAKOMA
 

Attachments

  • Screenshot_20250125_101735_Facebook.jpg
    Screenshot_20250125_101735_Facebook.jpg
    266.6 KB · Views: 2
Hata mwezi haujafika tokea uchaguzi,anataka kuzungumza nini?
 
Back
Top Bottom