Pre GE2025 John Mrema: Wanataka kunifukuza uanachama. Wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme

Pre GE2025 John Mrema: Wanataka kunifukuza uanachama. Wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ulisikia kijembe alichomrushia Wenje wakati anamtangaza Mnyika kuwa Katibu Mkuu? Umesikia hotuba ya Naibu KM Bara akiwataka wale wote waliowasema vibaya waende wakaombe msamaha na kutubu kwa wale waliowakosea? Hawa ni watu wa visasi. Huko mbeleni itakuwa kazi ya kuwapaka matope wale wote waliotofautiana nao. Imani yao ni vidonda vyao peke yake ndio vinatakiwa kuponywa.

Wangeshindwa ingekuwa vurugu.

Amandla...

Kwani Mwamba hakuwa katuahidi yetu baada ya uchaguzi?

Au ilikuwa mkuki Kwa nguruwe?
 
Ameandika Mrema kupotia ukurasa wake wa X,

"Nimejulishwa na mwenyekiti wa tawi langu, ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama!

"Nimeshangaa sana maagizo hayo na mpango huo ambao unaratibiwa na viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Segerea bwana Kitomary!

"Wanademokrasia, wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme! Wanataka kufukuza wengine uanachama ili wasisemwe!

"Demokrasia ni pamoja na uhuru wa mawazo na kutoa maoni! CHADEMA ndiyo chama changu, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote!

"Nawatahadharisha acheni ujinga huo!"

john Mrema, kwani mtu hufukuzwa uanachama kama mbwa anayetaka kuiba nyama jikoni..?

Si kuna taratibu za kufuatwa ndugu kwa mujibu kanuni na katiba ktk kipengere cha mtu anawezaje kukoma/kuacha kuwa mwanachama..?

Kwanini una hofu hivyo? Kwanini unaanza kujihami kwa makelele ya mitaani tu..?

Cool down Mr John Mrema...

Kama kuna kosa lolote linaloweza wewe kufutiwa uanachama wako, basi subiri utajulishwa, utapata nafasi ya kujitetea na mwisho uamuzi utafanyika kwa haki kabisa...

I say again, CALM DOWN DUDE...
 
Uongozi mpya msiruhusu haya mambo ya kufukuzana mapema hivi. Haki ya kutoa maoni ni haki ya kila raia, ilindeni na muiishi demokrasia ambayo kila siku tunaihubiri.

Uongozi wa visasi si mzuri, mtakuwa mmeanza na mguu wa kushoto.

Tunafikiri hili jambo halitatokea.

Najikumbusha ahadi za Mwamba kushughulika na waliomkwaza baada ya uchaguzi.

Ya kuwa mkuki kwa nguruwe?
 
Kwani amemkosea Nini lissu mpaka atake kumfuta uanachama? Mbona sikuwahi kumsikia kwenye kampein akimsema vibaya lissu??

Kimsingi uchaguzi ushakwisha sasa ni muda wa kujenga chama, haya mambo ya kutishiana tishiana sio kabisa( kama ni kweli). Vinginevyo huyo jamaa anatafuta kiki ya kuondokea asipewe hiyo frusa
Umeongea point
 
Tundu Lissu achana na mipango hii kama ni kweli.. wewe ndio mwenyekiti, wapigie simu walio chini yako muyamalize
 
Muda wa kuzungumza umeisha saiv ni vitendo tu, hutaki hama chama tubaki na pure soldiers
 
Kama ni kweli anachoongea Mrema basi ni makosa, CHADEMA tunatakiwa tuheshimu freedom of Speech kwa vitendo.

Hukuelewa ulipoambiwa kuwa Lissu hafai uongozi wa juu, ila utaanza kuelewa kidogo kidogo kwa vitendo
 
Kama ni kweli anachoongea Mrema basi ni makosa, CHADEMA tunatakiwa tuheshimu freedom of Speech kwa vitendo.
Naam.

Na aitwe kwenye vikao taratibu zifuatwe ikiwemo haki ya kusikilizwa kwanza na hatua zote zifanyike umma ukijulishwa sio tuhuma za hewani tu .
 
Naafiki. Kwa umri na nafasi alokuwa nayo alipaswa kujua kuwa demokrasia hamaanishi uholela. Uhuru wa kutoa maoni ni lazima uratibiwe, vinginevyo ni kukaribisha vurugu
 
Ameandika Mrema kupotia ukurasa wake wa X,

"Nimejulishwa na mwenyekiti wa tawi langu, ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama!

"Nimeshangaa sana maagizo hayo na mpango huo ambao unaratibiwa na viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Segerea bwana Kitomary!

"Wanademokrasia, wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme! Wanataka kufukuza wengine uanachama ili wasisemwe!

"Demokrasia ni pamoja na uhuru wa mawazo na kutoa maoni! CHADEMA ndiyo chama changu, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote!

"Nawatahadharisha acheni ujinga huo!"

wanasahau kuwa hiyo ni chaggadema na wewe ndio miongoni mwa wenye mali
 
Uongozi mpya msiruhusu haya mambo ya kufukuzana mapema hivi. Haki ya kutoa maoni ni haki ya kila raia, ilindeni na muiishi demokrasia ambayo kila siku tunaihubiri.

Uongozi wa visasi si mzuri, mtakuwa mmeanza na mguu wa kushoto.

Tunafikiri hili jambo halitatokea.
Mbowe kasema CDM tusitukanane, na atakaetukana baada ya uchaguzi akione cha moto.
 
Ameandika Mrema kupotia ukurasa wake wa X,

"Nimejulishwa na mwenyekiti wa tawi langu, ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama!

"Nimeshangaa sana maagizo hayo na mpango huo ambao unaratibiwa na viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Segerea bwana Kitomary!

"Wanademokrasia, wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme! Wanataka kufukuza wengine uanachama ili wasisemwe!

"Demokrasia ni pamoja na uhuru wa mawazo na kutoa maoni! CHADEMA ndiyo chama changu, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote!

"Nawatahadharisha acheni ujinga huo!"

Kwani anataka kusema nini nayeye
 
Huyo ndiye Lissu-dikteta kama JPM.
Screenshot_20250123-203524.jpg
 
Ndiyo maana tumesema kuwe na Tume ya mapatanisho - kila upande umeumizwa ; ukiruhusu haya ya kufukuzana CDM haifiki mbali - muda ni mchache sana kuelekea uchaguzi Mkuu. Msiwape nafasi maadui wetu wapumue, inatakiwa pressing inanze kwa umoja wote, yaani ni kukabia juu.
Mkitaka ondokoni, mwende VACATION na mzee wenu.
 
Back
Top Bottom