John Pambalu: Nimekuandikia tena, Rais Samia unadanganywa

John Pambalu: Nimekuandikia tena, Rais Samia unadanganywa

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Mhe. Rais tarehe 28.04.2023 nilikuandikia makala yangu niliyoipa jina la "Sikiliza mama", katika makala ile nilieleza namna ambavyo utawala wako umeshindwa kutatua kero na matatizo ya wananchi, nilidhani wasaidizi wako wangechukua yenye heri wakushauri walibaki kunishambulia tu.

Mfano Dr. Mollel naibu waziri, lakini nikikumbuka namna alivyoudanganya umma kuwa watu wanatoka Ulaya kuja kutibiwa Tanzania nikasema kama maneno haya aliyouambia umma huwa anakwambia na wewe boss wake, basi sio tu kwamba unadanganywa bali unadanganywa sana, mimi nimechagua kumpuuza.

Mhe. Kwenye ile makala yangu nilieleza namna ambavyo utitiri wa Kodi unavyoumiza wafanyabiashara, Jana wafanyabiashara wa Kariakoo wamegoma na katika mgomo ule wameeleza namna utitiri wa kodi unavyowaumiza. Sitaki kupoteza muda kurejea niliyoyasema kwenye makala yangu wacha niweke link hapa.👉



Mhe. Rais Zamani watawala walikuwa wakipita njiani tulitolewa madarasani na kushikishwa matawi ya miti huku tukiimbishwa nyimbo za kuwapa utukufu hata kama walikuwa waovu nao walipozisikia nyimbo zile walivimba kichwa na kujiona wazalendo hata kama walikuwa mafisadi, siku hizi ka utaratibu kamebadilika ni mwendo wa mabango tu nchi nzima yenye maneno matamu huku maisha yakiwa machungu, "Watanzania sio wajinga", alijesemea Marehemu.

Nikitazama namna ambavyo wamachinga wa Makoroboi Mwanza walivyoandamana bila kuambiwa andamaneni, wafanyabiashara wa Kariakoo walivyogoma bila kuambiwa gomeni, nasema enzi imefika ukingoni.

Ukisikiliza namna ambavyo wakulima wanaomboleza kwa namna ambavyo tumaini la kupewa mbolea ya ruzuku lilivyozika matumaini yao kwa kuunguza mimea yao shambani huku wakisubiri mbolea isiyofika ni wazi kuwa wanaokwambia unapendwa huku wananchi wako wakifuta machozi, wanakudanganya.

Mhe. Waliokuzunguka wanakusifia badala ya kutatua kero za wananchi, ningekuwa Mimi Rais ningewaeleza sifa njema ni mimi Rais kutopata kelele kutoka kwenye eneo nililokuamini kulisimamia kwa niaba yangu. Sasa wao wanashangilia raia wanalia ni kama kuna nchi mbili tofauti, nchi ya wala bata inayoamini kuwa nchi ya makabwela nao wanakula bata kama wao, mama unadanganywa.

Mhe. Rais hebu fikiria ulipotoa amri ya kufungua media zilizofungwa walijitokeza wasaidizi wako wakasema wanafungua YouTube tu na sio magazeti, uliposema wasiue raia kwenye vituo vya polisi wao wakasema polisi wakiuawa je, nani awasemee?, uliposema wasitoze Kodi za miaka ya nyuma wakasema hilo ni tangazo la kisiasa tu wao mwendo mdundo, ukiona uliowateua hawatii tena amri zako unadhani unaowaongoza watakuheshimu?.

Sikuchonganishi na uliowateua ninakueleza vile sisi raia tunajisikia kuhusu utawala wako ukiona ni maneno ya hovyo yaone kama ya mkosaji tu.

Mhe. Rais, Roma alisema rimoti iko msoga, hata kama sio kweli raia wanajiuliza waliotajwa katika ma skendo ya wizi wa mali za umma enzi za utawala wa JK mbona ndiyo wale wale wanaofisadi na kwako halafu wanadunda tu na mipasho kibao mara hamieni Burundi nk. Wanaiondolea heshima serikali yako. Lakini utafanyaje masikini ya Mungu, Masud Kipanya alichora mikino ya mwanamke imeshika usukani halafu mikono mikubwa ya Mwanaume imeshika mikono ya mwanamke mithiri ya mtu anayefundishwa kuendesha gari.

Ninachokielewa waliokaribu yako wanakudanganya kwa hakika. Umelindwa muda wote ni ngumu kujua watu wanajisikiaje juu ya utawala wako, nikiambiwa nikushauri neno nitakueleza hitimisha Katiba Mpya, aga maana sioni wa kukuchagua tena.

Mhe. Leo niliwiwa kukueleza haya lakini ipo siku nitakueleza ya wachimbaji wadogo maana niko huku Busanda Geita wanaomboleza bila msaada.

Mungu Ibariki Africa
Mungu Ibariki Tanzania
John Pambalu
Mkt Bavicha Taifa
jpambalu@gmail.com
 
Lakini makala yote hii ni kutafuta uteuzi tu na sio kingine 😁😁😁 Mtanzania Akiongea ukweli ni kwasababu ya majungu tu.
 
Pale USA kiliundwa kikosi maalum Cha kupambana na madawa ya kulevya,yaani serikali iliamua lije jua,ije mvua linatekelezeka walilopanga Kwa gharama yoyote Ile.

Kile kikosi kilisheheni watu wa kazi,kilipewa nyenzo zinazowawezesha kufika popote pale duniani kasoro mbinguni TU.
Kosa walilolifanya baada ya kukabidhiwa majukumu Yao ni kuweka kikao na Shetani.
 
Huwezi kuongoza serikali iliyojaa mafisadi na wewe isiwe fisadi. Ukweli lazima usemwe
 
[emoji23][emoji23] mbona ni kama uandishi wa kujipendekeza au sijaelewa [emoji1745]
 
Back
Top Bottom