Johnny Depp adai hata angepewa offer ya $300 milion, hawezi kuwa tena Jack Sparrow

Johnny Depp adai hata angepewa offer ya $300 milion, hawezi kuwa tena Jack Sparrow

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Najua wengi wenu wapenzi wa franchise ya The pirates of the carribean.

Na najua bila shaka mnaipenda kwasababu ya Captain Jack Sparrow ambayo ni character inayochezwa na Johnny Depp.

Ila kwanza watengeneza movie walikuwa washaamua kwamba hatahusika tena katika movie hiyo kutokana na scandal alizonazo ikiwemo matumizi ya madawa na unyanyasaji. Haya yote yameibuka kutokana na mgogoro unaoendelea baina yake na aliyekuwa mke wake Amber Heard.

Amber Heard ambaye mwaka juzi inasemekana alikuwa na mahusiano na Bwana Elon Musk pia ni mcheza movie mashuhuri. Kabla ya kuachana walikuwa katika ugomvi mkubwa huku kila mmoja akimwinda mwenzake kupata ushahidi wa makosa anayofanya.

Ilifika kipindi wanategesheana hadi camera za siri, vinasa sauti, mwingine anamprovoke mwenzake alipuke amrekodi.

Kuna hadi picha za kinyesi kitandani ambapo kila mmoja anasema aliyekiporomosha ni mwenzake.

Mgogoro umeenda mbele zaidi ambapo sasa Johnny alifungua madai akitaka Amber amlipe $50 kwa kuchafua jina lake nje ya makubaliano yao kuwa baada ya taraka hawatazungumzia yaliyotokea kwenye ndoa.

Sasa akiwa mahakamani alisema kuwa hata angepewa ofa ya $300 milion dollars, asingekubali kucheza tena filamu ya pirates of the carribean. Ila wakili alimuonyesha ushahidi kuwa watengeneza Movie wenyewe walishasema kuwa hatohusika tena, yeye akajibu hakuwa na taarifa hiyo.

Johnny inadaiwa aliingiza kiasi $650 kutokana na movie hizo.

images (21).jpeg

This day will be remembered as the day that you almost caught captain Jack Sparrow
 
Hii kesi nimekua nikiifuatilia, and i gotta say, ukiwa na roho nzuri, haifichiki. Ukijaribu kuangalia mashahidi woote wanamtetea Johny Depp. Imefika a point hata mawakili wa Amber Herd wanakua kama wanajichanganya. Possibility ya Depp kushinda ni kubwa sana
Lakini wanasema itakuwa ngumu kushinda kwasababu kwanza Amber hakumtaja jina, pia anasema kamchafua ndo maana kapigwa chini project mbili na ushahidi unaonyesha watengeneza movie walifanya huo uamuzi hata kabla ya interview ya amber.

It seems anatumia sana drugs. Ulibahatika kusikia au kusoma kisa chake na Amber wakiwa mapumzikoni Australia walichofanya kwenye nyumba waliokuwa wamepanga?
 
Lakini wanasema itakuwa ngumu kushinda kwasababu kwanza Amber hakumtaja jina, pia anasema kamchafua ndo maana kapigwa chini project mbili na ushahidi unaonyesha watengeneza movie walifanya huo uamuzi hata kabla ya interview ya amber.
It seems anatumia sana drugs. Ulibahatika kusikia au kusoma kisa chake na Amber wakiwa mapumzikoni Australia walichofanya kwenye nyumba waliokuwa wamepanga?

Alifanya nini mkuu tuambie wengine hatujui
 
Huyo mal**a Amber walianzisha petition asicheze tena kwenye Aquaman 2.
 
Wanakula starehe zote zinaisha wanaamua waamie kwenye unga.
By the way Hollywood wanadai kuna mengi na stress ambazo watu wanshindwa zimudu

Nilihuzunika sana niliposikia my favorite actor wa Kwenye “Friends” Chandler Bing (Matthew Perry) ni mwathirika wa drugs[emoji174]
 
Back
Top Bottom