Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JOHN INNISS MSWAHILI WA NEW YORK
Nimemfahamu John Inniss miaka ya 1980 mwishoni kwa kutambulishwa na Bi. Riziki Shahari miaka hiyo yeye mwanafunzi Columbia University, New York ambako ndiko "Waswahili," hawa wawili walijuana.
John Innis ambae nikipenda kumwita kwa jina lake la utani "Mtembezi," alikuwa anakisema Kiswahili kiasi ukitoa ile "accent" ya Kimarekani utadhani kazaliwa Kariakoo.
Basi alipokuja Dar es Salaam tukakutana.
Mtu mstaarabu na muungwana sana.
Juu ya ulemavu wake alikuwa anajimudu vizuri akitembea bila ya msaada wa mtu.
Mungu akajaalia kuwa wenyeji wake Dar es Salaam mimi ni ndugu zangu pale Mission Quarter alipofikia.
Katika kufahamiana huku tulizungumza mengi na hivyo ndivyo alivyonihadithia maisha yake kwa yale yaliyomfika Vietnam akiwa askari Marine Corps na akapoteza mkono na mguu katika umri mdogo sana wa ujana.
Naamini nilikuwa nikimstaajabisha vile nikiwafahamu rafiki zake kutoka Dar es Salaam aliojuananao Marekani katika 1960s.
Aliniuliza kama namfahamu Abdul Nanji.
Nikamtajia hadi mtaa aliozaliwa na historia yake kama mwanachama wa Chipukizi Club na akina Badrin na Hussein Shebe.
Badrin alihamia Marekani miaka hiyo ya 1960 miaka ambayo Vita Vya Vietnam vilikuwa vimepamba moto.
Mazungumzo yetu yalikuwa yakistawi kwa kweli na mini nikistarehe sana kumsikiliza anavyokimwaga Kiswahili tena cha ndani kabisa.
Alikuwa haishi kunishangaza.
Innis ananambia, "Mohamed jana nilikwenda kwa Mita."
Huyu Mita ni katika vijana wa Kidaresalaam na alikuwa JWTZ.
John Innis Mtembezi anaendelea, "Zamani kila nikikutana na Mita hapa Dar es Salaam mazungumzo yetu makubwa ni mambo ya jeshi na silaha mpya.
Safari hii nikashangaa Mita kanishikilia na mambo ya biashara na miradi yake."
Nikamwambia, "Mita wewe utaweza kucheza ngoma na mzigo kichwani?"
Kashangaa vipi Mita atakuwa mwanajeshi na hapo hapo mfanya biashara.
Tabu kuamini semi kama hii ya "ngoma na mzigo kichwani," inatoka kwenye kinywa cha Mmarekani aliyejifunza Kiswahili kama lugha ya pili.
Mtembezi akifahamiana na Prof. Sengo ambae kama yeye ni bingwa wa Kiswahili.
Basi akaniuliza hali yake nk. nk.
Innis akanishangaza kupita kiasi.
Katika kumsifia Dr. Sengo kuhusu ujuzi wake wa lugha akaniambia, "Mimi Dr. Senior ni nyakanga wangu."
Hapa alinimaliza.
Hakuna kijana wa kiume Mswahili asiyelijua zimwi hili.
Nyakanga heshima yake kwenye kumbi ni kubwa mno kwa wali wake.
Nyakanga ndiye mwalimu wao wa kuwafunza yale ambayo baba wala mjomba hawezi.
Huyu ndugu yetu alikipenda Kiswahili na akajua hadi mila zetu.
Da Ummie pole sana na nakuomba tuwekee yale mahojiano yako na John Inniss.