Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo amewapongeza Wanafunzi, Walimu na Uongozi mzima wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya furaha ya kuona Shule ya sekondari ya Wasichana iliyopewa jina lake Jokate Mwegelo Girls, imepata ufaulu mkubwa katika matokeo ya kidato cha nne ambapo divisheni one zipo 73, divisheni two 9, divisisheni three 4 na hakuna divisisheni four wala zero.
Shule hiyo ilipewa jina la Jokate wakati akiwa Mkuu wa Wilaya Kisarawe ambapo alianzisha programu ya tokomeza zero na ilipata mafanikio makubwa ikiwemo kuendesha harambee iliyofanikisha ujenzi wa Shule hiyo.
Jokate kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii ameandika; “Wow, sio kwa DIVISON ONE hizo, Mabinti wetu wamefanya jambo kubwa ikiwa ni form four ya kwanza tunawapongeza sana, hongereni sana uongozi mzima wa Wilaya ya Kisarawe na Mkoa wa Pwani kwa kuendeleza kazi njema hii kwa viwango vya juu na hasa Mbunge wangu wa siku zote wa Jimbo la Kisarawe Mhe Jafo 🙏🏽”