Jokate Mwegelo ameipaisha Kisarawe, ni zaidi ya Mkuu wa Wilaya

Jokate Mwegelo ameipaisha Kisarawe, ni zaidi ya Mkuu wa Wilaya

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
JM.jpg
Salaam Wakuu,

Natumia nafasi hii kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa kuipaisha Kisarawe, Kielimu na Kiuchumi.

Wakati anateuliwa nilimbeza sana na kumuona kama kapendelewa. Wengine Walidiliki kusema kwamba ni Nyumba ndogo ya mtu fulani ndo maana kateuliwa. Ila kafanya kazi Vizuri hata zaidi ya Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wapenda Kiki.

Kisarawe ni moja kati ya halmashauri tisa za mkoa wa Pwani.Imeanzishwa tarehe 1 Julai 1907.Wilaya ya Kisarawe inapakana na Wilaya ya Mkuranga kwa upande wa Kusini-mashariki na Wilaya ya Morogoro upande wa Magharibi.Mashariki-Kaskazini kuna Jiji la Dar es Salaam, Kaskazini Wilaya ya Kibaha na Kusini Wilaya ya Rufiji. Lakini Utafikiri Kisarawe ndo Mkoa kumbe ni Wilaya tu kati ya Wilaya 9.

Pamoja na kukuta watu wa Pwani ni Wavivu, kwa muda mchache aliokaa Kisarawe, ameitambulisha kimataifa. Kisarawe imekuwa Maarufu. Kisarawe imekuwa maarufu zaidi hata ya Mkoa wa Pwani. Utendaji wake wa Kazi, umefanya Kisarawe kufunika Wilaya nyingine za Pwani.

Kuna baadhi ya Mambo ambayo ameyafanya na yanaonekana.

Elimu

= Wanafunzi walikuwa watoro na Shule za Kisarawe zilikuwa Zinafanya Vibaya, lakini sasa Zinafanya Vizuri.

= Wilaya ya Kisarawe aliikuta inauhitaji wa madawati 1166 ambapo kwa sekondari uhitaji ni 484, na 642
kwa shule ya msingi. Kafanyia kazi

= Alikuta Wilaya ina uhitaji wa shilingi milioni 124 kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo 113 Mashuleni, kafanyia kazi

= Alikuta Wilaya inauhitaji wa ofisi za Walimu za kisasa katika shule 14 ambazo zinagharimu shilingi milioni 880. Kafanyia kazi

= Alikuta Wilaya haina Maktaba, zinajengwa.

= Alikuta Kisarawe ina matatizo ya Maji. Kwa muda mfupi tatizo la Maji limepungua.

= Huduma za afya zimeboreka hasa huduma ya Mama na Mtoto. Ujenzi wa Wodi ya Upasuaji.

= Huduma ya Umeme imeboreka nk.

Ameweza kufanya mambo ya Maendeleo bila kuwasumbua vyama Pinzani wala kujenga Chuki kwa Wananchi. Hajihusishi na Ufisadi. Ana heshima kwa Kila mtu na ni msikivu.

Jokate ni Mfano kwa Viongozi wanaoteuliwa sasa.

Natamani angepewa Wilaya ya Kinondoni akamalize Migogoro ya ardhi.

Shule.jpg
 
Back
Top Bottom