Jokate Mwegelo ameipaisha Kisarawe, ni zaidi ya Mkuu wa Wilaya

Kwa interest zako,watu wafanye kazi anasifiwa mkuu wa wilaya.ongeza juhudi za kuhongwa ili utoe sifa
 
Yaani..huko insta ndio usiseme mpaka nikawa najiuliza amekuwa waziri au??
Kuna wapumbavu wanasifia mtu kutimiza majukumu yake kwa kodi zao!

Akina Mwalimu wangekua wanaita mikamera kwenye kila tukio la kutekeleza majukumu yao sijui ingekuaje!

Nadhani tungekua na maktaba ya picha ya Taifa!
 
Zilikuja nyuzi nyingi humu za bwana Sabaya... mwisho wake tunaujua. Am just saying!!
 
Kazi anayopiga huyu dada+uzuri/ urembo wake... aiseee she's so blessed [emoji120]
 
Sio rahisi. Mama anabadilisha watu vituo. Bila shaka atapelekwa Ilala kama sio Dodoma mjini.

Tuache majungu wakuu. Kama mtu anachapa kazi tumpe pongezi zake.
Siyo majungu mzee, ukiona mtu anatumia sana media kujitangaza jua kuna shida hapo, huyu mdada kila anachofanya lazima aite macamera, hata akikarabati choo cha shule macamera! Kuna wakuu wa wilaya wanafanya vizuri kuliko yeye ila sababu siyo watu wa macamera hatuwajui!!
 
Tena kama hayo maendeleo yangekuwepo yamkini yangetokana na upendeleo ulosababishwa na ukaribu unasemekana kati yake na mwendazake.?! Unapolinganisha na Wilaya nyingine.

Kwamba kila ushirikiano au msaada wa kiufundi au kama fedha ulipatikana kirahisi pale ulipohitajika sababu watoaji waliogopa kushitakiwa kwa mwendazake kuwa wanamkwamisha bidada? Ambapo wangeweza kutumbuliwa?!

Inahitaji tafakari!
 
Nilichogundua watu wengi ni kama wachawi tu, Yafaa kumpongeza, kisarawe ikivutiwa kiwanda kimoja kikawekwa pale pata mahali pazuri mno,HONHERA JOKATE PAMOJA NA UZURI WAKO IPO SIKU NITAKUJA KUKUSALIMU.
 
Manerumango pashakuwa town? Kazi Mzumbwi pakoje now? Lami ishafika Manerumango?
 
Atawadanganyeni wachache tu msio na Fikra pana. DC Jokate Kipindi cha Hayati Rais Dkt. Magufuli wala alikuwa hana muda na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Baada ya kuona Hayati Rais Dkt. Magufuli hayupo tena duniani na kuwa na wasiwasi na Cheo chake hicho sasa ameamua Kujipendekeza kwa Rais Mstaafu Kikwete ( ambaye ndiye Mshauri Mkuu wa Rais Samia ) ili ampiganie asimuondoe katika hiyo nafasi aliyonayo ya DC na ikibidi hata apandishwe kwa Kuteuliwa kuwa Mbunge.

Sasa wenye Fikra pana tumeshaanza kupata hisia kuwa katika Mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya ( ambayo muda wowote yanatangazwa ) kwa Kitendo cha DC Jokate Kujikomba kwa Rais Mstaafu Kikwete sasa hatotolewa hapo Kisarawe sana sana atahamishwa tu kwenda Wilaya nzuri zaidi au hata kuteuliwa kuwa Mbunge.

Ukita Uteuzi sasa Jipendekeze kwa JK.
 
Kwa mtu wa aina yake hata ukimpongeza ni sawa tu, binafsi sikutegemea kama angestahili ofisi yoyote ya umma.

Itoshe tu kusema amejitahidi.
 
Mtu anapongezwa kwa kufanya kazi zake?

Postman akifikisha barua au mzigo mahali husika tunahitaji kumpongeza?
Kwa mahali nchi hii ilipofika, ukiona mtu Serikalini ametekeleza majukumu yake mshukuru tu Kwa kweli..

Maana wengine hawatekelezi na cha kuwafanya hatuna.
 
Jokate yupo smart kichwani hadi kiutendaji,,mama hawezi kumpiga chini,tetesi ni kwamba anaenda wilaya ya temeke
Jokate yupo smart kichwani hadi kiutendaji,,mama hawezi kumpiga chini,tetesi ni kwamba anaenda wilaya ya temeke
Temeke hapawezi kabisaa,miongoni mwa wilaya zinazotaka uwe na maamuzi haswaaaa,Maana kwanza kuna viwanda vingi,bandari,wavuja jasho wengi,Wanafunzi wazazi wanaotegemea huduma Zaid za serikali kuanzia elimu, afya na maj.
Usafiri mkubwa ni daladala ,huku ni mtu ana nauli ya kwenda na kurudi tu humuelezi kitu.
Kila siku kusolve migogoro n.k
Jokate anaziweza wilaya ambazo bado Zina ushamba mwingi ili aweze waleta wasanii washangae shangae,event za kisanii Zaid kama mialiko kedekede,pichapicha nyingi.
Wilaya za watendaji weziwezi na wafanya biashara wabishi wabishi haziwezi

Wilaya za kazi na kusolve matatzo yanayotegemea viongozi wa serikali badoo ana ile ya kutaka kumridhisha kila mtu,Abaki tu kisarawe ama ateuliwe viti maalumu
 

Umekuza sana vitisho... huku uhalisia mkuu wa wilaya ya temeke wa sasa hivi hana competence yeyote ya kumzidi jokate.. kuanzia elimu mpaka mafanikio waliyoyaleta kwenye wilaya zao..

Yaani sehemu aweze muandishi wa habari ambays hata chuo kikuu hajafika, ashindwe binti mjanja mjanja mwenye degree na masters ya udsm + exposure ya kueleweka
 
Si tunamlipa mshahara kwani Ni ajabu ?
 
Gondwe naona umeandika gazeti, jiandae kwenda kisarawe then Jokate aje Temeke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…