Jokate Mwegelo ni kati ya wajasiriamali 30 wanaofanya vizuri- Forbes Africa

Jokate Mwegelo ni kati ya wajasiriamali 30 wanaofanya vizuri- Forbes Africa

Yale yale ya kina Jackline Mengi, kibiashara kinaanzishwa jana - leo kinatambuliwa na Forbes africa.

- Anafanya biashara gani serious ?

- Kampuni yake inaitwaje ?

- Kaajiri watu wangapi na ulipaji kodi wake ukoje ?

UJINGA MTUPU na vikampuni vya mfukoni kama WEUSI hata ofisi hakuna

- Kama Forbes wataendelea kumwamini MFONOBONG NSHEHE ( Forbes Africa Under 30 ) wanaweza kupoteza wasomaji makini, maana amekuwa MTUNZI tu wa STORI na mpenda RUSHWA i think

Nimecheka sana kuhusu weusi
 
Angetajwa Mkenya poa tu ila kwa kuwa ni Mtz acha tupovuke tu.
Jokate ana biashara gani na ofisi ziko wapi? Kuna vijana wengi wako under 30 wana hela kuliko Jokate, nimeanza kutilia mashaka data za hiki kijarida. Jokate huyu anayehangaika maofisin kutafuta deal za u MC na promo awe entrepreneur?
 
Maandiko yao mengi siku hizi yako kibiashara, Unampa chochote mwandishi anakuandika kama SORT OF PROMOTION ili na wewe uitumie hiyo title kuingiza chochote. Kama hawa forbes Africa ndo matapeli haswaa
Nakuunga mkono aisee,na kuna taasisi zinaitumia Forbes kama marejereo yao kitu ambacho ni ujinga mara 100
 
Nimecheka sana kuhusu weusi
Ila huo ndo ukweli mkuu, Ukiambiwa 'WCB Wasafi' ni kampuni huwezi hata kubisha - maana unaona kabisa wako professional na ni legal entity na mpaka kodi wanalipa, lakini ukiona anatumia nguvu nyiingi kusema sijui nini ni kampuni unajua kabisa ni mbabaishaji
 
Nakuunga mkono aisee,na kuna taasisi zinaitumia Forbes kama marejereo yao kitu ambacho ni ujinga mara 100
Ni kweli. Kuna watu wengi wanaliamini sana hilo jarida bila kujua linaweza kuwa manipulated. Mfano kuna jamaa fulani wa Kenya alipotajwa tu - akaanza kuitumia hiyo TITLE kuuza vitabu vyake vya ujasiriamali. Pia mtu huwa akitajwa anakuwa katangazika sana maana hilo jarida linasomwa na kuaminika na wengi duniani. Ingawa kwa sasa pia jingine la Bloomberg ( US ) huwa linaandika pia - la muhimu ni kulinganisha taarifa
 
Jokate ana biashara gani na ofisi ziko wapi? Kuna vijana wengi wako under 30 wana hela kuliko Jokate, nimeanza kutilia mashaka data za hiki kijarida. Jokate huyu anayehangaika maofisin kutafuta deal za u MC na promo awe entrepreneur?

Kweli mkuu,kwenye malikia wa nguvu clouds nimeona wadada kibao wanapiga biashara huyo jokate hagusi, kuna mmoja anatengeneza mbolea kutokana na uchafu, mwingine pampas n.k
 
Ule mkataba wake wa mabilioni na wachina wa kidoti brand ulienda wapi mpaka akaishia kuwa m/kiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Kisarawe?
 
Back
Top Bottom