Jonas Mkude kasimamishwa kwa utovu wa nidhamu

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Huyu mwamba sijui ana shida gani kwa kweli, siku ile wanaenda Zimbabwe wenzake wamevaa jezi juu na tracks chini wengine vibukta vyeusi sare yeye kapigwa yale mashati ya maua ya Hawaii na kipensi cheupe.

Kule Zimbabwe wanasali na Balozi yeye hajafunga macho anakuna nungunungu zake kichwani. Tukirudi kwenye uchezaji I am glad hatakuwepo kwa kweli, sijawahi muona Mkude akifanya sliding tackle hata siku moja yeye ukabaji wake huwa ni kunyanyua mguu na kukita.

Sioni anything special kwa huyu bwana labda kuwe na watu kama Kotei na Fraga wa kumsaidia ila akiwa na Muzamiru siku hiyo utacheka maana hata pasi hajui kupiga.

Ana kitete cha mguu, anakimbia kama ana majipu miguuni, pasi zake nyingi za nyuma hajui kupiga penetration passes kabisa
siku ya mechi ya Tunisia nilifurahi sana Fei Toto alipoingizwa badala yake. Atulize kichwa ule usela mavi wake unakera sana.

 
Mechi na Tunisia fei alicheza na mkude.
 
Simba yangu tunavurugana wenyewe
 
Nilikua siamini hii taarifa hadi nilipoenda kwenye page ya simba na kuikuta
Imeandikwa kimakosa sana
 
Nilikua siamini hii taarifa hadi nilipoenda kwenye page ya simba na kuikuta
Imeandikwa kimakosa sana
Kwamba Mkude kasingiziwa au? Unajua hata TFF kazenguana nao mara ngapi kambini team ya Taifa? At least atapata muda kutosha ku chill na masela wake wa Kawe anaowanunuliaga konyagi na bangi
 
Nilikua siamini hii taarifa hadi nilipoenda kwenye page ya simba na kuikuta
Imeandikwa kimakosa sana
Taarifa ina makosa mengi sana. Najiuliza ulazima wa kumsimamisha mcheza jiningali timu ina mechi nyingi tu kwa muda mfupi.
 
Simba nao siku hizi wanayumba sana, mambo kama haya kwa kipindi hiki wangeyaacha kwanza wafocus ktk mechi muhimu, wanaweza kuona wanajenga kumbe wanabomoa. Angepigwa bench muda sahihi wangetoa taarifa sio sasa hata ukiisoma hiyo taarifa wamerudiarudia tu
 
Siku zote huwa naamini wanamichezo wa Tanzania wana vipaji halisi, ila kinachowaghalimu ni nidhamu ya kimaisha, ukikosa nidhamu ya kimaisha hata uwe una ubora wa kiasi gani uwezi kufanikiwa!

Tazama nchi ndogo kama Burundi ina wachezaji waliofanikiwa sana kuliko sisi watanzania ni kwasababu warundi wana nidhamu sana ya kile wanachokifanya.

Pia hata majirani zetu Uganda, wachezaji wengi wa Uganda wamefanikiwa kutoka nje ya nchi na kufanya vyema kwasababu ya nidhamu, waganda kiukweli wana nidhamu sana. Sijui watanzania kilichotulemaza ni nini? Vijana wengi wa Tanzania hawana nidhamu kabisa!! Hili ndio tatizo kubwa.

Mkude ni mfano wa aina ya vijana wengi walioko nchini.
 
Taarifa ina makosa mengi sana. Najiuliza ulazima wa kumsimamisha mcheza jiningali timu ina mechi nyingi tu kwa muda mfupi.
Ndiyo maana hawajasema kosa lake ila naomba nikukumbushe kitu, kipindi Mkude akiwa captain unajua kisa cha kutolewa?

Team wakati ina struggle financially kila siku alikuwa anatishia kuicha Simba kwenda Yanga waliokuwa na mahela ya Manji mbaya zaidi alikuwa anashawishi na wenzake kina Ajibu na kina Ndemla.

Huwezi jua this time kafanya nini, what if ana incite rebellion kambini what if anatembeza maneno ya fitna kambini, avumiliwe tu? Naamini kafanya kitu kibaya sana lakini itavuja tu tutajua maana kama ni mambo yake ya kuchelewa kambini au mazoezini au kwenda akiwa kalewa konyagi yashazoeleka hayo.
 
Huyu mwamba sijui ana shida gani kwa kweli,siku ile wanaenda zimbabwe wenzake wamevaa jezi juu na tracks chini wengine vibukta vyeusi sare yeye kapigwa yale mashati ya maua ya hawaii na kipensi cheupe...
Huyu aliendika nae afukuzwe kabisa, lugha dhaifu sana, lugha ya hovyo.

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…