Jonas Mkude: Kinachowaangamiza Simba ni kiburi, Jifunzeni kutokana na haya

Jonas Mkude: Kinachowaangamiza Simba ni kiburi, Jifunzeni kutokana na haya

Umemsikia Messi akilalamika au unasoma magazeti ya udaku na kujaribu kulinganisha mambo?Leta source ya habari inayo qoute Messi akisema haongezi mkataba kwa sababu anataka pesa zaidi.Elekeza nguvu zako kwenye timu yako.
 
Maslahi gani...? ya mchezaji kutaka kiwango kikubwa kama ndo anasajiliwa ilhali ni kuongeza tu mkataba..!? hakuna kitu kama hicho, aende tu huku vyura FC


Kwa kawaida, kama ulikuaa hujui. Mchezaji inapotokea anaongeza mkataba kwa lugha nyingine ni kwamba msaada na uwezo wake bado ni mhimili kwa klabu.

Hivyo basi kwa kuwa soka ni Kazi kwake (Tofauti na sisi Mashabiki tunaoona kuwa not burudani) ni lazima dau liongezeke.

Unataka kusema kama aliongeza mkataba ulio isha kwa mil 40 basi huu mkataba mpya aongeze kwa mil28...?
Hii haipo duniani... na haijawahi kutokea kabisa... Itakiwa mara ya kwanza hapa Bongo.
 
Asepe tu simba IPO na itaendelea kuepo
Tumemkuza toka team ya watoto simba b sasa kama anona simba aimlipi asepe tu
 
Real Madrid hajatwaa ubingwa tokea 2012 nae ameacha wachezaji?Mijitu mengine unashangaa wanafikiri kwa kutumia nini?Liverpool leo ni mwaka wa 25 hawajatwaa ubingwa.Cha ajabu nini?.

Liverpool's imekuwa ikipoteza players muhimi kwa kipindi hiko.

Kama unataka mafanikio
Unauzaje Torres?
Unauzaje Suarez?

nao wako kama Simba SC tu. wanapoteza wachezaji muhimu ikiwa wanasaka ubingwa.

Timu yenye kusaka ubingwa inakuwa na haiba ya kuvutia wachezaji (mfano Yanga hapa afrika mashariki).

 
Barcelona wamemuuza Sanchez,ambaye walimnunua kutoka Juve na timu zote hizo zikatwaa ubingwa.
 
Liverpool wamemuuza Torres na Suarez ndio sababu hawajachukua ubingwa kwa muda wa 25 years?Are you serious?
 
Hatuhitaji ushauri wa kunyenyekea wachezaji. Wachezaji ni kama wafanyakazi wengine na wana wajibu wa kutimiza majukumu yao.Wana wakala ambao ndio wataongea na klabu kwa niaba yao.Mchezaji anayejithamini na kujua wajibu wake haropoki hovyo bali huwa anaacha kazi za kuboreshwa mkataba wake kwa wakala. Simba hatujazoea kupiga magoti kazi hiyo inafanywa na timu zinazokubali kuwa blackmailed na wachezaji wasiojua wajibu wao.
wewe itakuwa yule mwenyekiti wa usajili......una matatizo wewe mzee...kipi kwani kibaya...mbona hamnuni akisema ana ndoto ya kwenda kucheza madrid......?yale maisha yake na ana haki ya kudai kipato chake kiongezekwe.....!!!
 
Acheni ubahili, kama mkono wako mfupi then utaishia kushika vikombe vya chai rangi tu.
 
Inasemekana kwamba jitihada za Jonas Mkude kuongeza mkataba na klabu yake Simba SC upo kwenye utata mkubwa sana.

Inaonekana mkataba mpya wa Jonas Mkude unadai alipwe fedha zaidi ambazo amekuwa akilipwa kipindi aongezapo mkataba.

Hili suala la ongezeko la pesa za kusaini mkataba mpya limefanya viongozi wa simba sc kumuona kama mchezaji huyo ni msaliti na kuwa hana mapenzi na timu hiyo ambayo imemlea tangu ujana wake.

Hanspope alionekana kulalamika kwenye moja ya chombo cha Habari kuwa haiwezekani mchezaji waliomlea na kumkuza wao wenyewe atake kiasi kikubwa cha pesa ili aongeze mkataba.

"Kama ataki kucheza simba basi aende huko Yanga SC ambapo watamlipa hizo pesa... Mchezaji amejaa tamaa ya pesa sana" Alisema Hans Pope

.................................................................................

Simba ndio mnao haribu soka la Bongo. Mnasindwa kujua kuwa sasa ni wakati wa kubadilisha soka kutoka la Burudani kuwa la kulipwa..

Kumbukeni kuwa hawa vijana hawana kazi, wameamua kufanya soka kuwa ni kazi. Inapaswa kazi yao iheshimiwe kama kazi yako wewe inavyoheshimika....

Yule ni mchezaji wa kumtegemea sana kwenye kikosi chenu kwa sasa (zaidi ya kichuya) cha kushangaza mnamchukulia kama kapuku fulani hivi... Yaani iweje Mavugo alipwe pesa ndefu zaidi yake.. Ukizingatia yeye ndiyo mwenye kiwango zaidi ya huyo Mavugo.

Igeni waingereza pale. Ona salary ya Rooney! Kipindi anafanyiwa salary increment yeye ndiye alikuwa dependable player.

Huwa mnajifanya viburi sana. Eti ohh acha aende simba ni kubwa kuliko yeye. Hilo si sawa kabisa.

Inaonekana bado hamjajifunza mpaka leo.

1. Tangu Yondani asepe hamkuwahi pata mlinzi mwenye hadhi yake....

2. Tangu Tambwe asepe hamjawahi pata striker mwenye hadhi yake na ubora wake.

3. Tangu Messi "Singano" asepe hamjawahi pata winga wa kulia mwenye uwezo kama yeye (licha ya kuwa Kichuya anajaribu kuwasahaulisha....

4. Tangu Kessy asepe hamjafanikiwa kumpata mbadala wa huyu kijana. (Mnatudanganya kuwa Bokungu ameweza)

5. Tangu akina Barthez na Dida wasepe pale hamjawahi pata walinda milango wenye ubora sawa na wakudumu kwa kitambo kirefu....

Simba acheni kiburi cha kujiona kuwa mnauwezo wa kuwaacha wachezaji wenu muhimu na kujidai kuwa mna uwezo mzuri wa kuwa replace.

Alafu kama mchezaji umemlea wewe basi unastahili kumjali kuliko yule aliyelewa na mtu mwingine kwani huyu ulomlea niwako, iweje sasa afe njaa wakati wewe ndo umemlea na iweje mgeni anufaike kwa matunda ya mzawa wakati mzawa anasota anahangaika kila kukicha kuilisha familia yake, SIMBA niwapumbavu tena wapumbavu sana. huwezi sema huyu tumemlea so asiombe hela kwahiyo wanataka acheze bure na asajiliwe bure wakati wanatumia hela ndefu kusajili wapumbavu wenzao! Simba nimapunguani sana!
 
Huwezi kusikia hilo suala kwenye Karne hii... Ukizingatiza tabia ya hawa Jamaa wa Simba dhidi ya wachezaji wao....

Hata hivyo! Pale wanacheza tu... Ila wanamalengo ya kuichezea Yanga kwa ajili ya Mafanikio...

Ndio maana wengi wakiwa kwenye form pale simba hupenda sana kukimbilia Yanga ambapo wanajua kuwa ni mahala pekee ambapo mchezaji unaweza pata Mafanikio...

Mwambie kuna mchizi mmoja alikuwa anaitwa Said Maulid SMG, alikuwa huko matopeni kama mnakumbuka baada ya kwenda Yanga mambo yake kila jicho liliona!
 
wewe itakuwa yule mwenyekiti wa usajili......una matatizo wewe mzee...kipi kwani kibaya...mbona hamnuni akisema ana ndoto ya kwenda kucheza madrid......?yale maisha yake na ana haki ya kudai kipato chake kiongezekwe.....!!!
Kweli ana haki ya kudai aongezewe pesa lakini lazima kiwango kiendane na uhalisia. Habari za ndani ni kwamba Simba wamemfikishia milioni 60 anataka 80.Mkataba uliopita alisaini kwa milioni 40.Hivyo anadaiwa ongezeko la asilimia 100.Natumaini unafanya kazi nenda kwa muajiri wako kesho udai ongezeko la mshahara wako kwa asilimia 100 halafu rudi hapa utuambie amekupa jibu gani.
 
Kweli ana haki ya kudai aongezewe pesa lakini lazima kiwango kiendane na uhalisia. Habari za ndani ni kwamba Simba wamemfikishia milioni 60 anataka 80.Mkataba uliopita alisaini kwa milioni 40.Hivyo anadaiwa ongezeko la asilimia 100.Natumaini unafanya kazi nenda kwa muajiri wako kesho udai ongezeko la mshahara wako kwa asilimia 100 halafu rudi hapa utuambie amekupa jibu gani.
Watu wanaropoka tu humu JF hawajui undani... mchezaji atake fedha nyingi kama ndo kwanza unamsajili inaingia akilini!?

Kapewa 60 hataki maana yake nini, aende huko Quality Plaza, Simba hakuna fedha
 
Halafu kinachoshangaza wapenzi wa mgongo wazi ndio wana kiherehere na usajili wenu kuliko hata wenye timu. Sijui wasiwasi wa nini?
 
Ndio maana sifatilii hii ligi ya kijinga. Angalia mashabiki walivyo na akili fupi.
 
Back
Top Bottom