Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maslahi gani...? ya mchezaji kutaka kiwango kikubwa kama ndo anasajiliwa ilhali ni kuongeza tu mkataba..!? hakuna kitu kama hicho, aende tu huku vyura FC
Real Madrid hajatwaa ubingwa tokea 2012 nae ameacha wachezaji?Mijitu mengine unashangaa wanafikiri kwa kutumia nini?Liverpool leo ni mwaka wa 25 hawajatwaa ubingwa.Cha ajabu nini?.
Waliachwa au waliuzwa?Naona lugha inakupa tabu.Oezil ndio nani?Akina Di Maria na mwenzake Oezil walikuwa ball-boys pale santiago bernabeu?
wewe itakuwa yule mwenyekiti wa usajili......una matatizo wewe mzee...kipi kwani kibaya...mbona hamnuni akisema ana ndoto ya kwenda kucheza madrid......?yale maisha yake na ana haki ya kudai kipato chake kiongezekwe.....!!!Hatuhitaji ushauri wa kunyenyekea wachezaji. Wachezaji ni kama wafanyakazi wengine na wana wajibu wa kutimiza majukumu yao.Wana wakala ambao ndio wataongea na klabu kwa niaba yao.Mchezaji anayejithamini na kujua wajibu wake haropoki hovyo bali huwa anaacha kazi za kuboreshwa mkataba wake kwa wakala. Simba hatujazoea kupiga magoti kazi hiyo inafanywa na timu zinazokubali kuwa blackmailed na wachezaji wasiojua wajibu wao.
Akienda Jangwani msianze majungu yenu.Uko sahihi kabisa Mkuu.. Simba in kubwa zaidi ya Mkude.
Inasemekana kwamba jitihada za Jonas Mkude kuongeza mkataba na klabu yake Simba SC upo kwenye utata mkubwa sana.
Inaonekana mkataba mpya wa Jonas Mkude unadai alipwe fedha zaidi ambazo amekuwa akilipwa kipindi aongezapo mkataba.
Hili suala la ongezeko la pesa za kusaini mkataba mpya limefanya viongozi wa simba sc kumuona kama mchezaji huyo ni msaliti na kuwa hana mapenzi na timu hiyo ambayo imemlea tangu ujana wake.
Hanspope alionekana kulalamika kwenye moja ya chombo cha Habari kuwa haiwezekani mchezaji waliomlea na kumkuza wao wenyewe atake kiasi kikubwa cha pesa ili aongeze mkataba.
"Kama ataki kucheza simba basi aende huko Yanga SC ambapo watamlipa hizo pesa... Mchezaji amejaa tamaa ya pesa sana" Alisema Hans Pope
.................................................................................
Simba ndio mnao haribu soka la Bongo. Mnasindwa kujua kuwa sasa ni wakati wa kubadilisha soka kutoka la Burudani kuwa la kulipwa..
Kumbukeni kuwa hawa vijana hawana kazi, wameamua kufanya soka kuwa ni kazi. Inapaswa kazi yao iheshimiwe kama kazi yako wewe inavyoheshimika....
Yule ni mchezaji wa kumtegemea sana kwenye kikosi chenu kwa sasa (zaidi ya kichuya) cha kushangaza mnamchukulia kama kapuku fulani hivi... Yaani iweje Mavugo alipwe pesa ndefu zaidi yake.. Ukizingatia yeye ndiyo mwenye kiwango zaidi ya huyo Mavugo.
Igeni waingereza pale. Ona salary ya Rooney! Kipindi anafanyiwa salary increment yeye ndiye alikuwa dependable player.
Huwa mnajifanya viburi sana. Eti ohh acha aende simba ni kubwa kuliko yeye. Hilo si sawa kabisa.
Inaonekana bado hamjajifunza mpaka leo.
1. Tangu Yondani asepe hamkuwahi pata mlinzi mwenye hadhi yake....
2. Tangu Tambwe asepe hamjawahi pata striker mwenye hadhi yake na ubora wake.
3. Tangu Messi "Singano" asepe hamjawahi pata winga wa kulia mwenye uwezo kama yeye (licha ya kuwa Kichuya anajaribu kuwasahaulisha....
4. Tangu Kessy asepe hamjafanikiwa kumpata mbadala wa huyu kijana. (Mnatudanganya kuwa Bokungu ameweza)
5. Tangu akina Barthez na Dida wasepe pale hamjawahi pata walinda milango wenye ubora sawa na wakudumu kwa kitambo kirefu....
Simba acheni kiburi cha kujiona kuwa mnauwezo wa kuwaacha wachezaji wenu muhimu na kujidai kuwa mna uwezo mzuri wa kuwa replace.
Huwezi kusikia hilo suala kwenye Karne hii... Ukizingatiza tabia ya hawa Jamaa wa Simba dhidi ya wachezaji wao....
Hata hivyo! Pale wanacheza tu... Ila wanamalengo ya kuichezea Yanga kwa ajili ya Mafanikio...
Ndio maana wengi wakiwa kwenye form pale simba hupenda sana kukimbilia Yanga ambapo wanajua kuwa ni mahala pekee ambapo mchezaji unaweza pata Mafanikio...
Kweli ana haki ya kudai aongezewe pesa lakini lazima kiwango kiendane na uhalisia. Habari za ndani ni kwamba Simba wamemfikishia milioni 60 anataka 80.Mkataba uliopita alisaini kwa milioni 40.Hivyo anadaiwa ongezeko la asilimia 100.Natumaini unafanya kazi nenda kwa muajiri wako kesho udai ongezeko la mshahara wako kwa asilimia 100 halafu rudi hapa utuambie amekupa jibu gani.wewe itakuwa yule mwenyekiti wa usajili......una matatizo wewe mzee...kipi kwani kibaya...mbona hamnuni akisema ana ndoto ya kwenda kucheza madrid......?yale maisha yake na ana haki ya kudai kipato chake kiongezekwe.....!!!
Watu wanaropoka tu humu JF hawajui undani... mchezaji atake fedha nyingi kama ndo kwanza unamsajili inaingia akilini!?Kweli ana haki ya kudai aongezewe pesa lakini lazima kiwango kiendane na uhalisia. Habari za ndani ni kwamba Simba wamemfikishia milioni 60 anataka 80.Mkataba uliopita alisaini kwa milioni 40.Hivyo anadaiwa ongezeko la asilimia 100.Natumaini unafanya kazi nenda kwa muajiri wako kesho udai ongezeko la mshahara wako kwa asilimia 100 halafu rudi hapa utuambie amekupa jibu gani.