Jonh Momose Cheyo ni Mwenyekiti wa chama chake toka mwaka 1993 (miaka 26) lakini siyo CCM wala msajili mwenye shida naye

Kwahiyo kwa mantiki hayo unataka mbowe mwenyekiti wa CHADEMA awe mwenyekiti wa maisha?
 

Msajili Apunguze Mahaba Atende Haki Kwa Vyama Vyote Ili Vistawi Kama Picture Ya Hilo Ua!!!😅😄😃🤣😂😁
 
Demokrasia ni kufuata katiba ya chama bora iwe inaruhusu ushindani. Lakini kwa ujumla Tanzania hata kama katiba inaruhusu ushindani kuna mizwenge chungu mbovu kuanzia CCM (wanasema BABALAO) hadi vivyama vidogo, achilia mbali CDM. Malalamiko tunayo yasikia ni kuwa Mwenyekiti haondoki madarakani bali ukiamua kula nae sahani moja wakati wa uchaguzi basi utakuwa na shida. Tuone mwakani kama kuna mtu ataamsha pua yake apeleke jina lake ili ashindanishwe na Magufuli. Tumemsikia Mzee Sumaye amesema yake na kuna waliomjibu, lakini je kuna aliemtishia aodoe jina au analia kura za hapana tu, ambacho ni kitu kizuri.
 
huko chadema hakuna demokrasia kwa kitu cha mwenyekit!

hapo unajaribu kupindisha maneno tu ukweli unauju na utegemee mbowe atapitishwa kwa wajumbe kuulizwa wanaofiki mbowe aendelee kuwa kuwa kiongozi waseme ndio, wajumbe wanamuogopa mbowe wote watasema ndio

hapo kungekuwa na secret ballot wagombea wapambanie nafasi
 
Ukisoma kitu kisome kwa umakini, mimi nimesema "Demokrasia ni kufuata katiba ya chama bora iwe inaruhusu ushindani". Sasa hapo nimepindisha nini. Ushindani si kuchukua fomu tu, bali ni mchakato mzima pamoja na upigaji kura. Waastarabu hupiga kura za siri, ukinihakikishia kuwa CDM hawana kura za siri nitakubaliana nawe. Issue yangu sio Mbowe bali ni kupata mwenyekiti kwa kufuata katiba ya chama na utawala bora. Kama CDM hawafanyi hivyo basi hakuna Demokrasia. Najua CCM wanapotoka awamu ya kwanza ya Raisi kwenda awamu ya pili hawana ushindani na ukijaribu watakutoa tu, haya tumeyaona kwa uwazi zaidi Dodoma kwa kiti cha Raisi wa Zanzibar.
 
Sasa iko wapi? Tunasikitika uongozi wa nchi kukosa kukaa Airport kuisubiri bombardier.
leo tuko busy na kifo cha ali mufuruki na kesho gwaride la uhuru wa tanganyika na tanzania bara(!). kwanza bombardier bado. phd zilizoenda canada hazitoshi, inatakiwa reinforcement!
 
Jonh Momose Cheyo ni Mwenyekiti wa chama chake toka mwaka 1993 (miaka 26) lakini siyo CCM wala msajili mwenye shida naye.

Unadhani ni kwa nini?

View attachment 1285471
Mkuu kuna jibu jepesi hapo...
1. Mti wenye matunda...
2. JMC na chama chake ni sawa na joka la kibisa ambalo haliumi wala halitishii ugali wa wenyewe wanalichezea watakavyo...
 
Kwani waziri mkuu mstaafu kupigiwa kura za hapana haikuwa demokrasia?
 
Kwani waziri mkuu mstaafu kupigiwa kura za hapana haikuwa demokrasia?
Kama katiba yao inaruhusu hicho kitu basi hakuna shida lakini pia nafikiri ni utawala bora kwa yeyote apitae bila kupingwa kupigiwa kura ndani na nje ya vyama. Hii ingepunguza ushenzi tunaofanyiwa na walio madarakani.
 
Mkuu ninecheka kabla ya kuanza ku comment.

Umenikumbusha hadithi za Cheyo, misemo inayoenda kusahaulika sasa ya 'mzee wa mapesa', chama chake cha UDP na kisa cha wanyama walaku nilichokishuhudia chaneli ya wanyama ya Nat geo.

Chama hicho miaka iliyopita, kiliwahi kuingia kwenye mgogoro wa kinyang'anyiro cha madaraka, kati ya huyo mzee Cheyo na jamaa mmoja sasahivi ni marehemu aliyejulikana kwa jina la Jidulamabambasi!

Jamaa huyo niliyemtaja, alifuata 'demokrasi' akampindua uenyekiti mzee Cheyo!

Wee, ebanee! Kwa kuwa tu mkuu umesahau kadhia hiyo!

Mzee Cheyo alighadhabika 'akasara'.
Moto uliwaka, nyasi kupukutika na jamaa yule kuishia kufukuzwa uanachama.

Mzee Momose cheyo ni dikteta aliye mfano hai wa udikteta uliopo kwa vyama vyote vya kisiasa nchini Tz, hata kukitaja Ccm sitaki kwa sababu ndani yake kuna figisu na fitina za kufa mtu.

Kumbuka mzee Mrema alivyokabidhi kijiti cha uenyekiti kwa shingo upande huku akilalamikia kuchezewa 'mchezo mchafu'

Nilitaka nimtolee mfano wa kuigwa r.i.p James Mapalala mwanzilishi wa CUF, lakini naye hakutoka kidemokrasia, alitoka kwa mtindo wa 'kotapini', kugongwa kwa nyundo na kisha kuchomoka.

Kinachomsaidia Cheyo ni 'ndiyo mzee' yake kwa Ccm, kawa branch ya Ccm, kama ilivyo Cuf na Nccr ya Mbatia na sasahivi bado kidogo Chadema, maana viongozi wa ngazi za juu wote wanajisundia Ccm kwa kutuona raia tunaowaunga mkono, sote ni wapumbafu!

Tangu aingie madarakani rais Magufuli, Cheyo akachukua likizo, hakosoi chochote, kazi yake ni kuunga tu mkono juhudi na kusaini vitabu vya wageni kwenye dhifa za kuapishwa viongozi wateule wa kitaifa.

Sasa kuunga mkono juhudi ndiyo lengo la vyama vya upunzan? Kwanini asirejee tu Ccm likaeleweka moja kama walivyofanya wazee wenzake?

Hawa 'wamiliki' wa vyama vya siasa nchini, huwalinganisha na nilichokishuhudia Nat geo channel!

Porini kuna baadhi ya wanyama mfano fisi na simba, wanaelewa kwa kutokuelewa eti kuwa wao wana hatimiliki toka kwa mnyaziMungu ya kukamata, kuua na kula wanyama wenzao, bila ya wao kuwindwa na kuliwa!

Linapofika suala la wao kuwekwa kati ili sasa nao waliwe, hutoa sauti za miungurumo ya ajabu ajabu kutisha na uoga, wakipiga kelele huku wengine wakitoa hadi uharo wa vinyesi ili tu 'kusevu', lakini janja hiyo huwaga haiwasaidii, huishia kuliwa huku wakilalamika.

Tukiachana na huyo Cheyo, kwani ndani ya Ccm utasema kuna demokrasia?
Ndani ya Cuf kuna demokrasia?
Ndani ya Nccr kuna demokrasia?
Ndani ya Chadema kuna demokrasia?
Na ndani ya hivyo vyama vingine utitiri vya magenge kuna demokrasia?

Kila mwenyekiti wa chama hapo alipo anatamani kukaa maisha kwenye hicho cheo, ilimradi tu anaendelea kuopoa maburungutu ya ruzuku kujaza tumbo lake.

Ukitaka ujitokeze kumdemokrasi mwenyekiti, waalah atakuua au kukufanyia figisu yoyote ya kishenzi, ilmradi tu yeye abakie pale daimadumu.

Yaani ni ubinafsi, ubinafsi, ubinafsi wa kinyama uliopitiliza, usiofaa kuigwa.
 
Jonh Momose Cheyo ni Mwenyekiti wa chama chake toka mwaka 1993 (miaka 26) lakini siyo CCM wala msajili mwenye shida naye.

Unadhani ni kwa nini?

View attachment 1285471
eti democrasia ni vipindi vya miaka mmoja au miwili au minne au mitano mitano ,oh hapana ,ni makubaliani ya kundi LA watu linaloamini pamoja(itikadi) na malengo yanayofanana namna likavyojiongoza ,lakini kwa kuwa wanadamu wanakuwa na mambo binafsi,tamaa na maono binafsi ni ambo jema kuwa katiba ambayo ni lazima ifuatwe, hivyo basis watu waweza kuwa tawala kifalme ambapo kiongozi ni lazima awe wa ukoo fulani na mzaliwa was namna gani ama mwanamume au mwanamke na ama mzaliwa was kwanza au was mwiisho na akisha chukua madaraka kitakachomtoa ni kifo( UK),wengine kipngozi anachaguliwa vipindi vikisha basis(USA) na wengine kiongozi kuchaguliwa bila ukomo alimradi anaowaongoza wanaamini ana uwezo wa kuwavusha na katiba inaruhusu(germany) sasa ubaya wa mh,Cheyo uko wapi ?KATIBA si inaruhusu?
 
Membe ameahidi kuchukua fomu 2020. Katibu anasema kuwa sio desturi na tamaduni.

Lakini sisi wanademokrasia tunataka membe na wenzake wachukue fomu tukutane dodoma pale machinjioni.

Katibu asikinasibishe chama na cdm.
 
SISI TUNA SHIDA NA CHADEMA KWA KUWA MWAKA 2015 CHAMA HIKI KILISHINDA UCHAGUZI LAKINI WAKAPINDUA MATOKEO NA KUMPA MTAWALA(firauni)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…