Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 87
MAOFISA wa CCM kutoka makao makuu na wengine wa chama hicho mkoani hapa wameweka kambi kwenye Jimbo la Karatu kuratibu zoezi la uandikishaji wapigakura katika serikali za mitaa na baadaye kushuhudia uchaguzi huo.
Habari za uhakika toka ndani ya CCM mkoani hapa zimebainisha kuwa jopo la viongozi hao wa CCM, linaongozwa na katibu wa mkoa, Mary Chatanda ambaye amehamishiwa Arusha hivi karibubni kuchukuwa nafasi ya Mohamed Mbonde aliyehamishiwa Mkoa wa Shinyanga.
"Ni kweli kuna viongozi wetu wapo Karatu... kama unavyojua nia yetu ni kuhakikisha tunalitwaa Jimbo la Karatu mwakani," alisema kiongozi mmoja wa CCM.
Kiongozi huyo alifafanua kuwa katika kuhakikisha jimbo hilo ambalo tangu mwaka 1995 mbunge wake ni Dk Slaa linarejeshwa CCM. Wameamua kuanza kuweka nguvu kwa kupata viongozi wa serikali za mtaa na vijiji.
"Tuna imani tukiwa na viongozi wa mitaa na vijiji tutakuwa tumepiga hatua moja muhimu kuelekea kutwaa Jimbo la Karatu," alisema kiongozi huyo.
Hatua hiyo ya CCM kuwapeleka Karatu maafisa wake imekuja takriban miezi mitatu baada ya kuwatuma maafisa kadhaa toka makao makuu ambao pia walikuwa wameweka kambi Karatu, ikiwa ni kujiandaa kulitwaa jimbo hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu ambaye anatoka Chadema, Lazaro Maasai alisema jana kuwa wana taarifa za CCM kuvamia wilaya hiyo, lakini wamejipanga kushinda.
"Ni kweli wapo viongozi wengi wa CCM na wameanza kucheza rafu zao ila wataondoka kwa aibu Karatu,"alisema Lazaro.
Mwenyekiti huyo alisema Chadema ina uhakika wa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo wa serikali za mtaa na hatimaye kushinda tena mwaka 2010.
Wilaya ya Karatu ni wilaya pekee mkoani Arusha ambayo inaongozwa na upinzani na CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali bila mafanikio kujaribu kuishika wilaya hiyo. Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005, CCM ilitumia zaidi ya Sh50 milioni jimboni humo, lakini ilishindwa.
Akizungumza na Mwananchi, Dk Slaa alidai kuwa amepata taarifa hizo na kueleza kuwa wanachofanya CCM ni vurugu.
"Ni kweli kuna viongozi Karatu na wamekuwa wakisababisha vurugu kwani kuna vitongoji vipya vitano wameshinikiza viwepo bila utaratibu, lakini tunapambana nao," alisema Dk Slaa.
Alisema licha ya CCM kuongeza nguvu Karatu, bado ana imani kuwa Chadema itashinda kwenye uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu, Ahmed Mshamu alisema hali ya uandikishwaji Karatu inakwenda vizuri ingawa kuna malalamiko mbalimbali.
"Ni kweli kuna malalamiko kuwa kuna chama kimeweka kambi huku na mambo ya vituo, lakini sio vurugu na yote tunayafanyia kazi," alisema Mshamu.
Mkurugenzi huyo alisema kuwepo kwa kundi ambalo linahamasisha wanachama wake kujiandikisha, si makosa na halmashauri haiwezi kuingilia.