Jopo la vigogo wa CCM lamwekea kambi Dk Slaa

Jopo la vigogo wa CCM lamwekea kambi Dk Slaa

Josh Michael

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
2,523
Reaction score
87
MAOFISA wa CCM kutoka makao makuu na wengine wa chama hicho mkoani hapa wameweka kambi kwenye Jimbo la Karatu kuratibu zoezi la uandikishaji wapigakura katika serikali za mitaa na baadaye kushuhudia uchaguzi huo.

Habari za uhakika toka ndani ya CCM mkoani hapa zimebainisha kuwa jopo la viongozi hao wa CCM, linaongozwa na katibu wa mkoa, Mary Chatanda ambaye amehamishiwa Arusha hivi karibubni kuchukuwa nafasi ya Mohamed Mbonde aliyehamishiwa Mkoa wa Shinyanga.

"Ni kweli kuna viongozi wetu wapo Karatu... kama unavyojua nia yetu ni kuhakikisha tunalitwaa Jimbo la Karatu mwakani," alisema kiongozi mmoja wa CCM.

Kiongozi huyo alifafanua kuwa katika kuhakikisha jimbo hilo ambalo tangu mwaka 1995 mbunge wake ni Dk Slaa linarejeshwa CCM. Wameamua kuanza kuweka nguvu kwa kupata viongozi wa serikali za mtaa na vijiji.

"Tuna imani tukiwa na viongozi wa mitaa na vijiji tutakuwa tumepiga hatua moja muhimu kuelekea kutwaa Jimbo la Karatu," alisema kiongozi huyo.

Hatua hiyo ya CCM kuwapeleka Karatu maafisa wake imekuja takriban miezi mitatu baada ya kuwatuma maafisa kadhaa toka makao makuu ambao pia walikuwa wameweka kambi Karatu, ikiwa ni kujiandaa kulitwaa jimbo hilo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu ambaye anatoka Chadema, Lazaro Maasai alisema jana kuwa wana taarifa za CCM kuvamia wilaya hiyo, lakini wamejipanga kushinda.

"Ni kweli wapo viongozi wengi wa CCM na wameanza kucheza rafu zao ila wataondoka kwa aibu Karatu,"alisema Lazaro.

Mwenyekiti huyo alisema Chadema ina uhakika wa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo wa serikali za mtaa na hatimaye kushinda tena mwaka 2010.

Wilaya ya Karatu ni wilaya pekee mkoani Arusha ambayo inaongozwa na upinzani na CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali bila mafanikio kujaribu kuishika wilaya hiyo. Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005, CCM ilitumia zaidi ya Sh50 milioni jimboni humo, lakini ilishindwa.

Akizungumza na Mwananchi, Dk Slaa alidai kuwa amepata taarifa hizo na kueleza kuwa wanachofanya CCM ni vurugu.

"Ni kweli kuna viongozi Karatu na wamekuwa wakisababisha vurugu kwani kuna vitongoji vipya vitano wameshinikiza viwepo bila utaratibu, lakini tunapambana nao," alisema Dk Slaa.

Alisema licha ya CCM kuongeza nguvu Karatu, bado ana imani kuwa Chadema itashinda kwenye uchaguzi huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu, Ahmed Mshamu alisema hali ya uandikishwaji Karatu inakwenda vizuri ingawa kuna malalamiko mbalimbali.

"Ni kweli kuna malalamiko kuwa kuna chama kimeweka kambi huku na mambo ya vituo, lakini sio vurugu na yote tunayafanyia kazi," alisema Mshamu.

Mkurugenzi huyo alisema kuwepo kwa kundi ambalo linahamasisha wanachama wake kujiandikisha, si makosa na halmashauri haiwezi kuingilia.
 
nimeisikia hiyo ila mi naona wanapoteza muda tu...Dr.Slaa is a heavyweight politician hawamuwezi
 
Wanajisumbua tu maana hata waje na pesa zao za mafisadi watapata patupu
 
Watu wa Karatu sio sawa na wa Ukonga ambako wanakumbatia mafisadi; hawa waMbulu wameamka kweli kweli HAWADANGANYIKI!!!
 
Najua CCM wanaweweseka sana kuona jinsi gani Dr.Slaa alivyo makini Hongera Dr Slaa
 
naona wazi kabisa sisiemu wamekosa shabaha
 
Yaani kupiga kambi kwa CCM pamoja na kununua wapiga kura, kuchangisha pesa, Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba mwaka 2005 walichangisha pesa nyingi sana walimbulia patupu
 
MAOFISA wa CCM kutoka makao makuu na wengine wa chama hicho mkoani hapa wameweka kambi kwenye Jimbo la Karatu kuratibu zoezi la uandikishaji wapigakura katika serikali za mitaa na baadaye kushuhudia uchaguzi huo.......
Umetoa wapi utumbo huu wa samaki? Jaribu kuweka source ya mazagazaga unayokopi....!
 
Ni haki yao kuweka kambi, ndiyo demokrasia hiyo watakuja CUF, CCM TLP and others as well what is wrong with that?
 
Umetoa wapi utumbo huu wa samaki? Jaribu kuweka source ya mazagazaga unayokopi....!

He (Josh Michael) is the source, au we mpaka uone `The Guardian!Na hii ishu siyo utumbo, UNLESS KAMA WE NI MGENI HAPA NCHINI.hII KITU INAJIELEZA YENYEWE na iko clear BILA HATA CHENGA!..We ndo wale waliotumwa hapa JF nini?
 
PakaJimmy,
Kila mtu anayekupinga au mwenye mawazo tofauti katumwa? akh!
i. wewe umetumwa na nani?
ii. usifikiri kwakuwa wewe umetumwa kila mtu anatumwa?
iii. CCM wana haki,CUF wana haki kama CHADEMA wanaona kuna kambi hakuna kulalamiika ni kupamabana ndiyo demo-kurahisisha.
 
He (Josh Michael) is the source, au we mpaka uone `The Guardian!Na hii ishu siyo utumbo, UNLESS KAMA WE NI MGENI HAPA NCHINI.hII KITU INAJIELEZA YENYEWE na iko clear BILA HATA CHENGA!..We ndo wale waliotumwa hapa JF nini?
Umeshakuwa msemaji wa JM sio? Unapoki habari ni vema kuonyesha umekopi wapi,zaidi Ta'adabu!
 
"Ni kweli kuna viongozi wetu wapo Karatu... kama unavyojua nia yetu ni kuhakikisha tunalitwaa Jimbo la Karatu mwakani," alisema kiongozi mmoja wa CCM.

Kiongozi huyo alifafanua kuwa katika kuhakikisha jimbo hilo ambalo tangu mwaka 1995 mbunge wake ni Dk Slaa linarejeshwa CCM. Wameamua kuanza kuweka nguvu kwa kupata viongozi wa serikali za mtaa na vijiji.

CCM ineshindwa kuleta maendeleo ya kweli katika nchi hii, kazi yao kubwa iliyobaki ni kuhakikisha inatumia michezo michafu ili ishinde chaguzi. watambue kuwa wananchi wa karatu si wa kuhongwa na kuhongeka, wapeleka hivyo vijesenti vyao lakini watambue kuwa mwisho wa siku watashindwa uchaguzi.

Mi naona wasipeleka viongozi tu wapeleka mpaka ofisi kuu huko karatu huenda wakapata 3% ya kura.
Naomba kuwasilisha hoja!
 
Nadhani CCM na Serikali yake wanapaswa kumshukuru sana Dr Slaa. Amewaamsha kwa mambo mengi tu.
 
Nadhani CCM na Serikali yake wanapaswa kumshukuru sana Dr Slaa. Amewaamsha kwa mambo mengi tu.
Kwahiyo aachwe awe "Mgombee pekee" mpaka milele..don't bring us back to the dooms days...lazima apate upinzani tusikie other side of him...
 
Back
Top Bottom