mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,916
- 8,630
Mjadala ulipoanza ulionekana kinachozungumziwa ni vipengele vya mkataba lakini ghafla katikati ya mjadala yakazuka mengine yote uliyoyaainisha Dini Utaifa Rangi and so on and so forth !!Hakuna anayepinga uwekezaji kwa sababu ya utaifa/ uraia ama dini yake anayependa kuwekeza Tanzania.
Kinachopingwa ni vipengele tata vilivyomo kwenye mkataba wa uwekezaji.
Zito Kabwe alipinga kwa nguvu uwekezaji wa kuchimba dhahabu Buzwagi, na tunakumbuka alivyotimuliwa bungeni akidaiwa kuwa kasema uongo. Hakupinga uwekezaji kwa sababu wawekezaji walikuwa ni wazungu,bali alipinga ubovu wa mkataba uliosainiwa na aliyekuwa Waziri wakati ule Mh. Karamagi.
Mradi mkubwa wa ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere wanajenga waarabu wa Misri, kilichoangaliwa ni uwezo na gharama nafuu siyo asili yao.
Kwa sasa mjadala hauna nguvu tena kwa sababu watu wameshakubali kutawanywa na wametawanyika kweli kweli !! 😅😅🙏🙏
Sasa mjadala mkuu ni SIMBA DEI 🙏🙏😂😂