Kimsingi hakuna aliye juu ya sheria, hayo ya kusema sijui kuna asiyeweza kishitakiwa hata akistàafu, ni siasa tu hizo. Tatizo watu wamekariri tu katiba badala ya kuielewa.
"The Constitution is the supreme being in the country's set up and NO ANY subject should be deemed to supersede its
sanctity". Na hii ndo maana hata rais anawajibika kuongoza kwa kuifuata Katiba.
Kwa nchi yeyote ya kidemokrasia i.e. ambayo viongozi wake huchaguliwa na wananchi kwa njia ya kura na pia kuweza kuondolewa kwa njia hiyo, kwa mantiki yoyote ya kisheria na misingi ya utawala bora, viongozi wake automatically wanakuwa hawana kinga yoyote inayowalinda kwa makosa wanayofanya wakiwa chini ya kiapo.
Hivyo katiba kusema rais hawezi kushitakiwa ktk nchi kama yetu ni uongo wa mchana kweupe na hii ina-qualify kuleta kutangazwa kwa Constitutional Crisis kwa sababu katiba yetu inaitambulisha nchi yetu kama Democratic State ila cha kushangaza ktk utendaji (Execution) ina-assume the role of Constitutional Monarchy, wakati hii ya mwisho sio katiba yetu.
Mwisho, mahakama zetu ziache unafiki (Double Standard) ktk kutafsiri katiba, waache kuwafanya wengine waonekane miungu watu wakijificha kwenye kichaka cha watu kushindwa kutafsiri katibà ipasavyo hali inayowafanya washindwe kuwajibika kwa wananchi wanapokuwa madarakani.
Kiukweli hakuna kitu kinachoitwa Presidential Immunity hasa ktk katiba ambayo inaundwa ktk misingi ya kidemokasia kama yetu na kama ipo basi hiyo katiba ni "quid quid voverat atque promiserat".
NB: Ninakiri, mimi ni Layman, lkn elimu ni bahari.