Jordan Rugimbana alimkosea nini Hayati Magufuli?

Jordan Rugimbana alimkosea nini Hayati Magufuli?

Aliponzwa na mdomo wake,Lissu mdomo wake hauna break,nawwza sema ndio mtanzania pekee asiyeogopa mtu kwa kizazi hiki

..aliponzwa na ujasiri wake, na rekodi yake ya muda mrefu ya kusimamia ukweli.

..Watz wengi walikwisha salimu amri na kukubali kila hila na ulaghai wa Magufuli. Lissu alikataa ndio maana wakajaribu kumuua.
 
Sidhani kama walitegemea kama angefika hospitali akiwa hai. Hauwezi kufanya mission kama hiyo alafu watu wengi kiasi hicho wawe involved.

Kama kuna maelezo RC alipata itakuwa ni baada ya mambo kwenda mrama na jamaa kufikishwa hospitalini.

Siku ile sidhani kama kuna mtu yeyote angemsikiliza jiwe, wabunge wa CCM walilia machozi hadharani, yaani ni kama roho wa Mungu alishuka pale Dom, kila mtu alipambana kuokoa uhai ya Lissu.

Kama haijapangwa haijapangwa tu, hata ufanye nini.
Ile ilikuwa ni mision ya mauaji. Nadhani walikuwa wameambiwa hakikisheni anakufa kwa risasi nyingi kabisa. Lakini Mungu alivyo mkuu wakajikuta wanaweweseka na kushindwa kutimiza lengo. Na baada ya muda Magufuli ndiye anakufa.
 
Rugimbana mtu smart sana, alikuwa kiongozi wa mbio za mwenge. Kabla ya kuwa DC Morogoro mjini tayari alikuwa na project na wafadhili wa China kule Chamanzi
 
Tarehe 7 Sept 2017
Tundu Lissu anapigwa risasi mkoani Dodoma

October 2017
Jordan Rugimbana mkuu wa mkoa wa Dodoma anatumbuliwa.

Jordan ni mtoto wa Kamisna wa kwanza wa jeshi la magereza nchini. Baba yake alifariki kwa ajali kama sikosei enzi za Nyerere. Nyerere aliwachukua baadhi yao na kuwalea kama wanae.
Huyu alikuwa kada mtiifu wa UVCCM.

Kuna mwaka akawa kiongozi wa mbio za mwenge. Ghafla nyota yake ikawaka na kukwaa ukuu wa wilaya kadhaa kama vile Mwanga,Kinondoni na kuwa RC Dodoma.

Kipindi Tundu Lissu anapigwa risasi yeye ndio alikuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya inzi na usalama mkoa. Inasemekana kuna maelekezo toka juu hakuyafata kuhusiana na kumtibia na kumsafitisha majeruhi Lissu.

Baada ya kutumbuliwa akajifungia ndani akijiikita kufanya shughuli zake binafsi ikiwemo kusimamia ujenzi wa makumbusho ya kabila lao huko Karagwe.

Wanoko wakamfikishia taharifa hayati Magufuli kuwa yule bwana uliyemtumbua anajenga makumbusho kijijini kwao. Magufuli akaupiga stop ule mradi ambao ulikuwa hautumii fedha za umma bali wananchi na wafadhili. Na akamwambia amefungiwa mbinguni na duniani kamwe atalamba asali maishani mwake.

Huu ni mwaka wa nne wenzake akina Chalamila na Kafulila n.k wanatumbuliwa na kurudishwa, yeye yupo tu anacheza bao kijiweni.
 
Back
Top Bottom